Mkutano wa REDET: Zanzibar Tuitakayo, Ujenzi wa Uvumilivu wa Kisiasa Zanzibar

Shukran mkuu Pasco kwa jibu.

Swali lengine: Je. does Zanzibar want to increase its minority stake to equal partnership?

Zanzibar inataka hata leo kumaitain its outonomy, bahati mbaya huu muungano wetu ni kama ndoa za Katoliki, hazina talaka!.

Origional mambo ya muungano ni 11, tumeyaongeza kwa maujanja ujanja mpaka yamefika 27!. Mambo hayo yanaongezekeka tuu lakini hayapunguziki, hivyo hata hizi juhudi za Zanzibar kutaka kuyaondosha mafuta kwenye mambo ya muungano, its fighting a loosing battle na wataendelea kulia lia sana tuu.
 
Lunch break is over, mada ya uraia wa Zanzibar, iliyowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa ZnZ inaendelea, imethibitishwa bila mashaka kuwa kila Mzanzibari, ni Mtanzania, ila sio kila Mtanzania ni Mzanzibar.

Leo uhuru wa Zanzibar umekumbushiwa, kumbe ule uhuru ni halali kwa mujibu wa sheria na mapinduzi si halali, ila kwa Zanzibar yamehalalishwa.
Zanzibar inaongozwa na serikali De Facto na sio De Jure, ile hii De Facto imeitisha uchaguzi hivyo kuifanya kuwa 'De Facto-De Jure' equals De Jure.

Hoja ya Zanzibar kama ni nchi au si nchi pia umeibuka kiaina.
 
Wachangiaji wamemvurumishia madongo Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, kuwa sheria ya ukaazi ni utata mtupu, kumbe ilipopitishwa bazani, wawakilishi wote wa CUF, walitoka nje!. Kumbe sheria ya ukaazi inawanyima haki Wanzanzibari wote wenye uraia halali wa Zanzibar, wakiwemo Wangazija kumbe sasa sio Wanzibari tena!.

Kumbe Wazanzibari wote wanaoishi nje ya Zanzibar wakiwemo wanaioshi bara, wamepoteza haki zao zote za kiraia eti kisa hajaishi Zanzibar miezi 36 mfululizo!
Wana Cuf, wanataka kuwasha moto humu ndani, madoderetor wa REDET, wanatia maji ili kuepuka kilichotokea kongamano la Mwalimu Nyerere.

Mimi sasa naanza kukasirika, nadhani bora nijiondokee zangu!.
 
Ala! Hamkulijua hilo? Mlidhani inawakomoa machogo peke yao?

Amandla.........
 
Wewe ushaambiwa kuna mambo mazuri,,uvute subira,,Tena unaondoka unakwenda wapi!?? SUBIR TU
 
Wewe ushaambiwa kuna mambo mazuri,,uvute subira,,Tena unaondoka unakwenda wapi!?? SUBIR TU
Nimejiondokea zangu, mada zote 11 ninazo, nitajisomea taratibu tuu ila nitaikosa michango ya wachangiaji na mijadala.

Mod, rekebisha headline, siyo live tena, mkutano leo day one, umeahirishwa. good day. thanks
 
Its the other way round, Watanzania ndio sio Wanzanzibari, lakini Wanzazibari ni Watanzania. Kwa vile Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya JMT, inayojiwala kwa mambo yake ya ndani, then wote tunahaki ya kuchangia kuhusu 'Zanzibar Tuitakayo'.

Kabla ya Muungano, kulikuwa na Tanganyika na Zanzibar, Tanganyika died and Tanzania was born, Zanzibar did not die, it only surendered its outomy to Tanzania and maintained its minority stake kwenye mambo yake ya jikoni na chumbani, sebuleni ni Tanzania.
Tujadili kwa uhuru tuu.
Ni vyema hayo mambo ya jikoni na chumbani wakaachiwa weyewe kuyazungumza na kuyatafutia suluhu. Kimbele mbele cha Watanzania (Wasio Wazanzibari) katika hayo ya jikoni ndiyo kinatuletea usumbufu huu tunaoupata.Hebu waachieni wenyewe.
 
Sasa wewe unasherehekea nini kama mambo yanaongezeka?Jua Zanzibar ina historia chafu, si sehemu ya kuifakamia na kutaka kuweka serekali moja.

Huyo genius wenu Nyerere, alikataa hivyo si kwa kuwa alikuwa ni mjinga bali ameona mbali.Kuifakamia Zanzibar na kuimeza ni kubomoa amani ya Tanzania nzima kwa ujumla.Sifikirii kama wazanzibari nao watakaa tuu, ukizingatia ni waislamu hiyo kesi haitakuwa tofauti na Palestina.

Vita visivyo na mwisho!
 
Ni vyema hayo mambo ya jikoni na chumbani wakaachiwa weyewe kuyazungumza na kuyatafutia suluhu. Kimbele mbele cha Watanzania (Wasio Wazanzibari) katika hayo ya jikoni ndiyo kinatuletea usumbufu huu tunaoupata.Hebu waachieni wenyewe.
Ndugu yangu .... kuvuja, nafuu kwa mchukuzi, naungana nawe kwa asilimia 100%, mambo ya jikoni na chumbani, waachiwe wenyewe, tusiwaingilie kabisa, tatizo hapo mwanzo, Zanzibar ilikuwa ni nyumba ya chumba kimoja, jikoni ndio hapo hapo, chumbani, hapo hapo na sebuleni hapo hapo, ukipakua chakula mbele ya mgeni na watoto wapo, huweza tenga, hiki cha wageni (gesi na mafuta) na hiki cha wote. Mgeni (bara) kala kanogewa mpaka anataka na cha wote.

Sasa nyumba ya Zanzibar imekuwa, sasa kuna jiko linajitegemea na sebule sio chumbani. Kaja tena yule yule mgeni bara, wewe chakula wapikia jikoni, haoni, kwa vile alifaidi, unataka kuamua leo usipakue cha wageni (gesi na mafuta) bali upakue cha wote ili chawageni ukakilie chumbani kwa kujificha, mgeni huyo kama ni mlafi, ujue hapo haondoki mpaka ale kile kinono cha wageni,

Gesi na mafuta hayakuwemo kwenye mambo ya muungano, mgeni bara, kaja mmempakulia bila hiana yoyote, hamkulalakamika hapo mwanzo, mgeni kanogewa, ndio sasa mwataka mwambia mgeni kuanzia sasa kile chakula si cha wageni tena, bali cha wote?!. Its too little too late, madhali mgeni kesha onja, mwache tuu ale na eendelee kula, tena si mafuta tuu, hadi samaki wa bahari kuu ni wa muungano!, tutakuja hadi maji ya bahari ni ya muungano na mwisho kabisa Zanzibar-Mkoa wa muungano!.
 
mwezi Aprili mwaka 2009, Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma ilitoa taarifa yake Bungeni. Moja ya suala ililozungumzia ni suala la utafutaji mafuta zanzibar na walitoa ushauri ufuatao:

"Kumekuwa na maneno mengi kuhusiana na utafutaji wa mafuta eneo la Tanzania Zanzibar. Mjadala ndani ya Kamati pia uligawa wajumbe kutokana na wametoka wapi katika pande mbili za Muungano. Kuna tatizo la msingi kabisa kuwa Taifa limepoteza uwekezaji mkubwa katika utafutaji wa mafuta katika upande za Zanzibar kufuatia mgogoro unaoendelea kuhusiana na suala la mafuta na gesi. Kamati inaamini kuwa Mafuta na Gesi ni suala la Muungano lililo katika Orodha ya Masuala ya 22 ya Muungano kama yalivyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ijapokuwa uhalali wa kuwekwa kwake katika Masuala ya Muungano bado ni mjadala mkubwa sana. Tatizo kubwa lililopo ni kwamba Shirika la TPDC sio shirika la Muungano; Shirika lisilo la Muungano linashughulikia suala la Muungano, suala nyeti kama mafuta na gesi. Kamati inadhani kuwa imefikia wakati mwafaka kwa Shirika la TPDC kuvunjwa na kuundwa Mamlaka ya Mafuta na Gesi Tanzania ambayo itakuwa ya Muungano. Mamlaka hii itakuwa na jukumu la kutoa vibali na kusimamia mikataba ya kugawana mapato ya mafuta (PSAs). Kila upande wa Muungano utaanzisha Kampuni yake ya Mafuta na Gesi kwa lengo la kushiriki katika uwekezaji na biashara. Ushauri huu kama ukitekelezwa utaondoa pia utata wa mgongano wa maslahi uliopo TDPC leo katika suala la kusimamia PSAs".

nimetoa hili katika hansard ya tarehe 29 aprili 2009. Zitto angerudi humu JF kutueleza ushauri huu murua ulifikia wapi katika utekelezaji maana ungekata mzizi wa fitina katika suala la mafuta Zanzibar. Nakubaliana na Kamati kuwa hakuna haja ya kulitoa katika mambo ya muungano. muhimu ni kuhakikisha kuwa Zanzibar inafaidika na mafuta kama yatapatikana huko kwa kuwa na kampuni yao inayomilikiwa na serikali ya zanzibar na kampuni hiyo itakuwa na hisa katika kampuni za mafuta. Bara pia watakuwa na kampuni yao ambayo itawekeza katika makampuni ya mafuta na gesi. Mamlaka ya Mafuta na Gesi watakuwa na jukumu la kusimamia sekta, kusimamia mfuko wa mafuta na kutoa leseni za kutafuta mafuta.
 
naomba nikusifu kwa Falsafa zako. Chakula cha Familia kitabaki katika sahani ya familia. Na Mgeni ni Mgeni atasubiri apakuliwe cha wageni kwa heshima na taadhima. Hayo ya Karume na Seif (ambayo yamewashtua hao wageni) ni bashrafu tuu.
 
Mie naona kwanza tungefix hayo matatizo ya mkataba wa muungano, Tanganyika na Zanzibar wakishamaliza kurekebisha huo mkataba wa muungano ndio tujadiliane kama ni mambo 11 au 1100.

Lakini bila ya kujadili muungano na kuweka clear watu wameungana namna gani, naona kama kelele hizi hazina mwisho.

Au wadanganyika hamtaki kujadili muungano?Ndio mmenogewa na Zenji...

mwezi Aprili mwaka 2009, Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma ilitoa taarifa yake Bungeni. Moja ya suala ililozungumzia ni suala la utafutaji mafuta zanzibar na walitoa ushauri ufuatao:

"Kumekuwa na maneno mengi kuhusiana na utafutaji wa mafuta eneo la Tanzania Zanzibar. Mjadala ndani ya Kamati pia uligawa wajumbe kutokana na wametoka wapi katika pande mbili za Muungano. Kuna tatizo la msingi kabisa kuwa Taifa limepoteza uwekezaji mkubwa katika utafutaji wa mafuta katika upande za Zanzibar kufuatia mgogoro unaoendelea kuhusiana na suala la mafuta na gesi. Kamati inaamini kuwa Mafuta na Gesi ni suala la Muungano lililo katika Orodha ya Masuala ya 22 ya Muungano kama yalivyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ijapokuwa uhalali wa kuwekwa kwake katika Masuala ya Muungano bado ni mjadala mkubwa sana. Tatizo kubwa lililopo ni kwamba Shirika la TPDC sio shirika la Muungano; Shirika lisilo la Muungano linashughulikia suala la Muungano, suala nyeti kama mafuta na gesi. Kamati inadhani kuwa imefikia wakati mwafaka kwa Shirika la TPDC kuvunjwa na kuundwa Mamlaka ya Mafuta na Gesi Tanzania ambayo itakuwa ya Muungano. Mamlaka hii itakuwa na jukumu la kutoa vibali na kusimamia mikataba ya kugawana mapato ya mafuta (PSAs). Kila upande wa Muungano utaanzisha Kampuni yake ya Mafuta na Gesi kwa lengo la kushiriki katika uwekezaji na biashara. Ushauri huu kama ukitekelezwa utaondoa pia utata wa mgongano wa maslahi uliopo TDPC leo katika suala la kusimamia PSAs".

nimetoa hili katika hansard ya tarehe 29 aprili 2009. Zitto angerudi humu JF kutueleza ushauri huu murua ulifikia wapi katika utekelezaji maana ungekata mzizi wa fitina katika suala la mafuta Zanzibar. Nakubaliana na Kamati kuwa hakuna haja ya kulitoa katika mambo ya muungano. muhimu ni kuhakikisha kuwa Zanzibar inafaidika na mafuta kama yatapatikana huko kwa kuwa na kampuni yao inayomilikiwa na serikali ya zanzibar na kampuni hiyo itakuwa na hisa katika kampuni za mafuta. Bara pia watakuwa na kampuni yao ambayo itawekeza katika makampuni ya mafuta na gesi. Mamlaka ya Mafuta na Gesi watakuwa na jukumu la kusimamia sekta, kusimamia mfuko wa mafuta na kutoa leseni za kutafuta mafuta.
 
CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAMMPANGO WA UTAFITI WA ELIMU YA DEMOKRASIA TANZANIA(REDET)MKUTANO WA KWANZA WA HALI YA SIASA ZANZIBAR, ULIOFANYIKA KATIKA HOTELI YA BWAWANI TAREHE 22 HADI 23 DESEMBA, 2009MAJUMUISHO/MAPENDEKEZO YA WASHIRIKI WA MKUTANO1. Washiriki wa Mkutano wa Kwanza wa Hali ya Siasa Zanzibar uliofanyika katika Hotel ya Bwawani Zanzibar kuanzia tarehe 22 had 23 Desemba, 2009, wanatoa pongezi zao za dhati kwa Mpango wa Utafiti wa Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ujumla kwa kuandaa mkutano huu muhimu uliotoa fursa adimu kwa Wanzanzibari kutoka Nyanja zote za maisha kutafakari na kujadili kwa kina hali ya siasa na mustakabali wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.2. Washiriki wa mkutano wanatoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Amani Abeid Karume kwa kukubali kuufungua rasmi mkutano wa Kwanza wa Hali ya Siasa Zanzibar. Aidha, washiriki wanampongeza Mheshimiwa Rais kwa hotuba yake nzuri iliyosheheni kauli zenye busara na hekima katika ujenzi wa uvumilivu wa kisiasa Zanzibar na hotuba iliyoonyesha njia na kutoa dira ya Zanzibar tuitakayo.3. Washiriki wa mkutano wa Kwanza wa Hali ya Siasa Zanzibar kwa dhati kabisa wanatoa pongezi kwa Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dr. Amani Abeid Karume pamoja na Mheshimiwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalimu Seif Sharrif Hamadi kwa kuonyesha ujasiri wa hali ya juu sana, ukomavu wa kisiasa na uzalendo wa kweli kwa kuweka kando tofauti na uasimu wao ili kutanguliza mbele maslahi ya Wazanzibari wote na Tanzania kwa ujumla. Washiriki wanatambua kwamba:  Maridhiano yaliyofikiwa kati ya Rais Karume na Mhe. Maalim Seif yamefungua ukurasa mpya katika historia ya siasa za Zanzibar na pia yanatoa fursa nzuri ya kuanzisha safari salama itakayotuwezesha kupata Zanzibar tuitakayo. Vyama vya siasa, Asasi za Kiraia, washirika wetu wa maendeleo, Wanzanzibari na Watanzania wote kwa ujumla hatuna budi kutambua na kuunga mkono kwa kauli na vitendo azma ya viongozi wetu, Rais Karume na Mhe. Maalim Seif katika kujenga Zanzibar mpya – Zanzibar tuitakayo yenye amani, utulivu na maendeleo kwa wote.4. Mkutano unatambua umuhimu wa historia katika jamii maana tusipojua tulikotoka hatuwezi kufahamu vizuri tulipo na hata tuendako. Katika kuleta Muafaka na maridhiano, kuna haja ya kujenga utamaduni mpya wa matumizi mazuri au chanya ya historia ya Zanzibar na kufuata maadili ya demokrasia Viongozi na Wazanzibari kwa ujumla tuepukane kutumia jinamizi la historia kuwagawa Wazanzibari na kwa maslahi yetu binafsi au ya vyama vya siasa Tuainishe yale mazuri yatokanayo na historia ya Zanzibar ili kuyaenzi na kuyaendeleza kwa faida ya Zanzibar ya sasa na ile tuitakayo. Wazanzibari tukatae katakata kuwa watumwa wa historia.5. Chaguzi huru na za haki ni kigezo muhimu sana katika utekelezaji wa demokrasia na ujenzi wa utawala bora ili kuwapata viongozi wanaotokana na ridhaa ya watawaliwa (wananchi). Washiriki wa Mkutano wa Kwanza wa Hali ya Siasa Zanzibar wanapendekeza mambo yafuatayo: Ipo haja ya kufikiria kuwa na mfumo mpya wa uchaguzi badala ya mfumo unaotumika sasa wa mshindi kubeba kila kitu yaani “the winner takes all” au “first-past-the-post”. Mfumo wa uwiano yaani “Proportional Representation” unaweza kufaa zaidi katika muktadha wa hali ya siasa ya Zanzibar. Kuna haja ya kupitia upya sheria za uchaguzi ili kuwawezesha Wazanzibar wote wenye sifa za kushiriki uchaguzi waweze kutumia haki yao ya msingi kuchagua au kuchaguliwa katika nafasi za uongozi wa kisiasa. Upo umuhimu wa kutoa elimu ya uraia pamoja na elimu kwa wapiga kura. Ushirikiano kati ya serikali, AZAKI na umma kwa ujumla ni muhimu katika kufanikisha azma hii. Mkutano unaipongeza serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuanzisha Daftari la kudumu la wapiga kura. Mkutano unashauri daftari hili lipitiwe upya ili kuondoa kasoro zilizopo na kujenga imani ya wananchi kwa taasisi zilizokabidhiwa jukumu la kuendesha chaguzi.6. Washiriki wanatambua na kuthamini jitihada zote zilizofanywa na vyama vya CCM na CUF, Jumuiya za kimataifa, viongozi wa serikali zote mbili na asasi nyingine katika kuleta muafaka wa kisiasa Zanzibar. Hata hivyo: Mkutano unashauri viongozi na wananchi kwa ujumla kutafakari kwa kina sababu na vikwazo mbalimbali vilivyosababisha kutotekelezeka kwa muafaka wa I (1999); muafaka wa II (2001) na mazungumzo ya muafaka wa III yaliyovunjika mwaka 2008.  Mchakato wa maridhiano ni vizuri ukawashirikisha wananchi wote kuanzia jamii msingi. Hivyo viongozi waone haja ya kuwaelimisha wananchi masuala yanayohusiana na maridhiano. Viongozi wa serikali ikiwa ni pamoja na masheha, na viongozi wa vyama vya siasa waunge mkono kwa kauli na vitendo nia safi na dhamira ya kizalendo iliyokwishaonyeshwa na Mheshimiwa Rais pamoja na Katibu Mkuu wa CUF.7. Washiriki wanatambua umuhimu wa vyombo vya dola na mchango wa vyombo vya habari kwa usalama na amani ya nchi pamoja na utoaji wa haki kwa maendeleo ya nchi na watu wake. Hata hivyo: Vyombo hivi vifanye kazi kwa kuzingatia weledi, maadili na maslahi ya wananchi wote badala ya makundi fulani na maslahi binafsi ya kisiasa hususan wakati wa chaguzi.8. Mkutano unatambua umuhimu na nafasi ya serikali za mseto katika kutatua matatizo na migogoro ya kisiasa. Serikali ya umoja wa kitaifa ni muhimu kwa kuzingatia hali ya siasa ya Zanzibar. Hata hivyo: Tahadhari na umakini mkubwa unahitajika katika kufikia azma hiyo Fursa iliyojitokeza November 5, 2009 kutokana na maridhiano baina ya Rais Karume na Mheshimiwa Maalim Seif inatoa mwanya wa kufikia azma hiyo. Ni vizuri mchakato wa kufikia hali hiyo ukaanza mara moja.9. Mwisho Mkutano unawashauri wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, viongozi wa vyama vya siasa, AZAKI, viongozi wa kiroho, na wanahabari kuuunga mkono jitihada za vingozi katika kutafuta maridhiano endelevu na ya kudumu Zanzibar kwa kila hali ili kujenga Zanzibar mpya yenye amani, utulivu, maridhiano na maendeleo kwa wote. Jukumu la kujenga Zanzibar mpya na Zanzibar tuitakayo ni la Wazanzibar wenyewe na Watanzania wote.
 
[FONT=Arial, sans-serif]UDSM-[/FONT][FONT=Arial, sans-serif](REDET)[/FONT]​

[FONT=Arial, sans-serif]MKUTANO[/FONT][FONT=Arial, sans-serif] WA HALI YA SIASA ZANZIBAR-[/FONT][FONT=Arial, sans-serif]MAJUMUISHO/MAPENDEKEZO [/FONT]​

  1. [FONT=Arial, sans-serif]Washi[/FONT][FONT=Arial, sans-serif]riki wa Mkutano wa Hali ya Siasa Zanzibar wanatoa pongezi kwa (REDET) na UDSM kuandaa mkutano uliotoa fursa kwa Wanzanzibari kujadili na kutafakari hali ya siasa na mustakabali wa Zanzibar.[/FONT]
  2. [FONT=Arial, sans-serif]Washiriki wa m[/FONT][FONT=Arial, sans-serif]kutano wamemshukuru Rais Karume kuufungua na kumpongeza kwa hotuba ya ujenzi wa uvumilivu wa kisiasa Zanzibar [/FONT]
  3. [FONT=Arial, sans-serif]Washiriki wa mkutano, [/FONT][FONT=Arial, sans-serif]wamewapongeza Rais Karume na Maalimu kwa kuweka kando tofauti zao kwa maslahi ya Zanzibari kwa kufungua ukurasa mpya katika siasa za Zanzibar.[/FONT]
  4. [FONT=Arial, sans-serif]Mkutano unatambua umuhimu wa historia katika jamii maana tusipojua tulikotoka hatuwezi kufahamu v[/FONT][FONT=Arial, sans-serif]izuri tulipo na hata tuendako, hivyo wametoa wito kwa Wazanzibari kuepukane kutumia jinamizi la historia kuwagawa Wazanzibari na kuainisha mazuri ya historia ya Zanzibar ili kuyaenzi na Wazanzibari tukatae kuwa watumwa wa historia.[/FONT]
  5. [FONT=Arial, sans-serif]Chaguzi huru na za haki ni kigezo m[/FONT][FONT=Arial, sans-serif]uhimu cha demokrasia na utawala bora katika kuwapata viongozi wanaotokana na ridhaa ya wananchi. Washiriki wanapendekeza mambo yafuatayo:-[/FONT][FONT=Arial, sans-serif]mfumo mpya wa ucha[/FONT][FONT=Arial, sans-serif]guzi badala ya mfumo wa sasa wa mshindi kubeba kila kitu yaani "the winner takes all", watumie Mfumo wa uwiano yaani "Proportional Representation" -[/FONT][FONT=Arial, sans-serif]Kupitia upya sheria za uchaguzi ili Wazanzibar wote wenye sifa za kushiriki uchaguzi , washiriki na kuanzia kwa kutolewe elimu ya uraia. -[/FONT][FONT=Arial, sans-serif]Daftari la kudumu la wapiga[/FONT][FONT=Arial, sans-serif] kura lipitiwe upya ili kuondoa kasoro zilizopo nakujenga imani ya wananchi kwa taasisi zilizokabidhiwa jukumu la kuendesha chaguzi.[/FONT]
  6. [FONT=Arial, sans-serif]Mkutano unashauri[/FONT][FONT=Arial, sans-serif] kutafakari sababu za kutotekelezeka kwa muafaka wa I (1999); muafaka wa II (2001) na mazungumzo ya muafaka wa III yaliyovunjika mwaka 2008. -[/FONT][FONT=Arial, sans-serif]Mchakato wa [/FONT][FONT=Arial, sans-serif]sasa wa maridhiano uawashirikisha wananchi wote [/FONT]
  7. [FONT=Arial, sans-serif]Washiriki wanatambua umuhimu wa vyombo vya dola na mchango wa vyombo vya habari kwa usalama na amani ya nchi pamoja na utoaji wa haki kwa maendeleo ya nchi na watu wake. Hata hivyo:[/FONT][FONT=Arial, sans-serif]Vyombo hivi vifanye kazi kwa kuzingatia weledi, maadili na maslahi ya wananchi wote badala ya makundi fulani [/FONT]
  8. [FONT=Arial, sans-serif]Mkutano unatambua umuhimu na nafasi ya serikali za mseto katika kutatua matatizo na migogoro ya kisiasa. Serikali ya umoja wa kitaifa ni muhimu kwa kuzingatia hali ya siasa ya Zanzibar. Hata hivyo:[/FONT]
  9. [FONT=Arial, sans-serif]Tahadhari na umakini mkubwa unahitajika katika kufikia azma hiyo[/FONT][FONT=Arial, sans-serif]Fursa iliyojitokeza November 5, 2009 kutokana na maridhiano ba[/FONT][FONT=Arial, sans-serif]ina ya Rais Karume na Maalim Seif inatoa mwanya wa kufikia azma hiyo. Ni vizuri mchakato wa kufikia hali hiyo ukaanza mara moja.[/FONT]
  10. [FONT=Arial, sans-serif]Mwis[/FONT][FONT=Arial, sans-serif]ho Mkutano unawashauri wananchi wote wa Tanzania kuwa Jukumu la kujenga Zanzibar mpya yenye amani, utulivu, maridhiano na maendeleo kwa wote. Watanzania wote na Wazanzibari wakiwemo kama sehemu ya Tanzania.[/FONT]
NB. Nime iedit kidogo kupunguza urembo, Redet waliremba sana ili kuyapendezesha haya majumuisho. Hata hivyo majumuisho original nimeyaweka hapa kwenye attachment.
 
Attachments

  • Majumuisho.doc
    49 KB · Views: 92
mkuu Pasco,huwezi kuipanga vizuri hii?? inasumbua kidogo kuisoma,I mean concetration....
 
mkuu Pasco,huwezi kuipanga vizuri hii?? inasumbua kidogo kuisoma,I mean concetration....
Asante Mdau, mwanzo nilitumia PC ya Windows NT 98' nimerekebisha.
Asante pia kwa kunishauri kistaarabu, maana JF kuna wakati inawaka moto, badala ya kushauriwa unajikutwa unatukanwa. Thanks.
 
Back
Top Bottom