Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,897
- 942
Mbunge wa Jimbo la Hai, Mhe. Saashisha Mafuwe tarehe 05 Septemba, 2023 katika Mkutano Mkuu wa Jimbo la Hai Aliwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM ambapo Mgeni rasmi alikuwa ni Makamu Mwenyekiti wa (CCM) Bara Ndugu Abdulrahman Kinana
Mkutano Mkuu Maalum wa Jimbo la Hai ulilenga sana kwa Mbunge wa Jimbo la Hai, Mhe. Saashisha Mafuwe kusoma Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jimbo la Hai ambao ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama, Serikali na Wabunge.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndugu Abdulrahman Kinana, ameziagiza kamati za siasa za CCM, kuwafuatilia na kuwachukulia hatua wanachama walioanza kupitapita kusaka ubunge na udiwani.
"Nataka nitumie fursa hii kuziagiza kamati za siasa za CCM nchi nzima, zikisaidiwa na kamati za maadili nchi nzima, kuwafuatilia wale ambao wameanza kuzungukazunguka kutafuta ubunge, udiwani, uenyekiti wa mtaa au kitongoji kuanzia sasa" - MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndugu Abdulrahman Kinana
Katika Mkutano huo, Mhe. Saashisha Mafuwe alipata nafasi ya kuwasilisha mbele ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Jimbo la Hai miradi mbalimbali ya Elimu, Afya, Miundombinu, Uchumi iliyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
Mhe. Saashisha Mafuwe amemshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumpa maneno mengi ya kusema kwa kupitia miradi ya maendeleo aliyoipeleka ndani ya Jimbo la Hai.
Aidha, Mhe. Saashisha Mafuwe amemshukuru Ndugu Abdulrahmani Kinana, Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara kwa kukubali kuwa mgeni rasmi tarehe 05.09.2023 kwenye Mkutano Maalum Mkuu CCM wa Wilaya ya Hai wa kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Vilevile, Mhe. Saashisha Mafuwe amewashukuru sana Kamati ya Siasa Wilaya ya Hai kwa maandalizi, Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya, Viongozi wa Dini na Mila, Viongozi wa Mila kwa Daraja la Umangi waliomvalisha ngozi ya Mbelele.