Mkutano wa Dkt. Slaa mjini Kahama - Dec 4, 2013

Mkutano wa Dkt. Slaa mjini Kahama - Dec 4, 2013

Wajinga wanaopotosha kwa kupost mamia na/au maelfu hapa jf kudanganya umma sasa pateni habari kamili.
 
1452339_558673044208406_2063836110_n.jpg
TATIZO NI HICHO KITI USILIE

Na unaionaje hiyo poll inayoendeshwa humu JF kuhusu uamuzi wa kamati kuu CDM? mmepiga pua chini na Zito wenu wengi wanamuona ZZK ni saliti tu. AIBU!!!!!!
 
Dr.slaa amefika hapa Kahama saa 11na nusu,na amepokelewa na bodaboda 5 ambazo walichangiwa sh.5000 kutoka kwa viongozi kadhaa walioambatana na Dr.slaa,hapo awali Vijana wa chadema walionekana wakizunguka maeneo ya kahama stendi kuomba madreva Bodaboda wahudhurie mapokezi ya Dr.slaa lakini hali haikuwa nzuri kwani asilimia 90 ya madreva waligoma kuifanya hivyo.Wakati akielekea eneo la Mkutano Dr.slaa alipokelewa na mabango yanayosema"CHADEMA BILA ZITTO HAIWEZEKANI,TUACHIENI CHAMA CHETU,ENDELEENI NA UBAGUZI WENU",Baada ya kupanda jukwaani Slaa alipokelewa na Mawe,na matusi ya kejeli sana kutoka kwa Wananchi wachache waliokuwepo eneo la Mkutano.
Dr.slaa aliomba Vijana wake wa usalama watulize ghasia za wananchi,kisha akazungumza maneno machache tu kwa kusema Naomba maswala ya Zitto mtuachie sisi tutayamaliza,Mkutano nauahirisha hadi Jumapili jioni hapahapa Kahama.Kwahiyo Mkutano Kahama hadi Jumapili.

cc
Kurugenzi ya Habari.
 
Last edited by a moderator:
Safi sana Dr Slaa. Hakika umeudhihirishia UMMA ya kuwa Chadema sio Zitto bali ni UKOMBOZI wa kweli.

Hata hapa Arusha leo mkutano ulikuwa mkubwa sana na kutokana na speech ya Mh Msigwa, Zitto angetokea bahati mbaya angegombaniwa na kuraluliwa kama Simba aonavyo kitoweo.

Viva Dr Slaa Viva Chadema.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Nashangaa sana wana ccm uchwara na mafisadi kama .......... kung'ang'ania kuipa promo chadema wakati katibu mkuu wetu kinana amedoda vya kutosha mbeya leo na kuishia kufanya mkutano wa ndani na kukagua tazara ambayp imefilisiwa na ccm mafisadi
lazima utakuwa umeibiwa password: cc Mungi, Ben Saanane sweetlady njooni mumusikie katibu mwenezi wa magamba
 
Last edited by a moderator:
Dr.slaa amefika hapa Kahama saa 11na nusu,na amepokelewa na bodaboda 5 ambazo walichangiwa sh.5000 kutoka kwa viongozi kadhaa walioambatana na Dr.slaa,hapo awali Vijana wa chadema walionekana wakizunguka maeneo ya kahama stendi kuomba madreva Bodaboda wahudhurie mapokezi ya Dr.slaa lakini hali haikuwa nzuri kwani asilimia 90 ya madreva waligoma kuifanya hivyo.Wakati akielekea eneo la Mkutano Dr.slaa alipokelewa na mabango yanayosema"CHADEMA BILA ZITTO HAIWEZEKANI,TUACHIENI CHAMA CHETU,ENDELEENI NA UBAGUZI WENU",Baada ya kupanda jukwaani Slaa alipokelewa na Mawe,na matusi ya kejeli sana kutoka kwa Wananchi wachache waliokuwepo eneo la Mkutano.
Dr.slaa aliomba Vijana wake wa usalama watulize ghasia za wananchi,kisha akazungumza maneno machache tu kwa kusema Naomba maswala ya Zitto mtuachie sisi tutayamaliza,Mkutano nauahirisha hadi Jumapili jioni hapahapa Kahama.Kwahiyo Mkutano Kahama hadi Jumapili.

Utakuwa una akili kama ya Ngiri .From the look of the foto hakika hawa si watu wachache .Sijajua una maana gani kutunga uongo wote huu .Kwa sababu ya nini ? Unapingana na picha ? Kwani bodaboda zisipo kuwepo Slaa hawezi kusimama jukwaani ? Katoka Dar bila boda boda hadi Kahama why now bodaboda ziwe muhimu ?
 
Hapa si kibororonyi moshi aiseyee? Kwa wachaga,looh! sasaaa kazi iko tena mbichi kabsa kabsa.
 
Naona kuna mnazi nyuma ya picha!!!! Hii kitu ya kuchaka chua aise!!!
Aisee kahama kuna minazi,unafikiri kungekuwa na watu wengi lazima picha wangeweka mapema tena live,Aisee siasa ya kichadema ya kilaghai
 
Huu ndiyo mkutano wa Dkt. Slaa leo Kahama mjini ambao umeanza majira ya saa 12.15 jioni ambapo watu wamekuwepo uwanjani tangu saa 8 mchana kama walivyotangaziwa.

View attachment 124850
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilibrod Slaa akiwahutubia wanachi wa mji wa Kamaha na vitongoji vyake, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kukagua na kuimarisja uhai wa chama katika mikoa ya Shinyanga, Kigoma, Tabora na Singida, uliofanyika kwenye Uwanja wa CDT mjini Kahama jana. (Picha na Joseph Senga)

View attachment 124852
Katibu Kuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (chadema), Dk. Willibrod Slaa akiagana na wananchi wa mji wa Kahama baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa CDT mjini huo jana, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama katika mikoa ya Shinyanga, Tabora, Kigoma na Singida. (Picha na Joseph Senga)

Well done Kurugenzi.!!! Hii ndio kiboko ya wanafiki
 
Salamu tosha kwa zitto na kina Mwampamba name Shonza salsa wanaisoma namba.
 
Uongo mwingine hauna maana .Gari liko katikati mawe yakawa yanarushwa bila kuvunja kioo cha gari hilo ? Ngojea magazeti kesho tusikie yatasemaje .
 
Salamu tosha kwa zitto na kina Mwampamba na Shonza sasa wanaisoma namba.
 
Hii picha no uwongo,hill eneo ni CDT ambapo hupaki mafuso na kwa population ya kahama hao watu ni wachache sana
 
Kuna magazeti yatakopi ile habari ya yule mwehu kuuza vijarida vyao.

Alafu hawa ndio watetezi wa Zitto.
 
Kwa nyomi hii mutamuua ZZK na makuwadi wake CCM. Leo usingizi mumewaharibia kabisa.
 
Dr Slaa azuhiliki yani ni kama Ronaldo hata ukazeje lazima apite tu, kweli we ndio raisi wa mioyo ya watanzania, kila sehemu lazima umati ambao ujabebwa na costa wala maroli ujae kukusikiliza. Go on Dr!

Huyu mtu yupo kwenye mioyo yetu jamani...
 
Niko kahama watu walikuwa busy na mambo Yao.
Hizo picha ni za upande mmoja tu?
Chadema hapa kahama imejikondea kama mbwa koko.
 
Back
Top Bottom