Mkutano wa CHADEMA Arusha - Nov 29, 2013

Mkutano wa CHADEMA Arusha - Nov 29, 2013

Lema aishangaa CCM

Na Grace Macha, Arusha

Godbless LemaMBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), ameeleza kushangazwa na jitihada za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutaka Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe asichukuliwe hatua zaidi kwa madai ya kukinusuru chama kisisambaratike.

Lema alitoa kauli hiyo juzi wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kilombero.

Alisema kuwa CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani kinachowanyima CCM usingizi, walipaswa kufurahia kusambaratika kwao, lakini cha kushangaza viongozi wa chama tawala wamekuwa wakiwaasa wasimfukuze Zitto.

“Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wanalia wakitaka tupatane. Mbunge wao wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba naye analia kuwa CHADEMA tumefanya vibaya, tumrudishe Zitto.

“Sisi tunawauliza tukifanya vibaya ni faida kwao, kwanini wanalia. CCM wanalalamika CHADEMA hatuna demokrasia, ni chama cha kibabe, tumemwonea Zito, kwamba tutapasuka. Hivi tukipasuka wao wataimarika sasa wanalia nini badala ya kufurahi?” alihoji Lema.

Chanzo: T Daima

This is interesting.Lema kawapa ukweli.
 
CCM wanajua zitto ni nguzo yao imara sana katika mkakati wao wa kuisambaratisha chadema hivyo wanajua mkakati wao utakwama kwa kias kikubwa sana maana hawaoni mtu mwingine mzito ndani ya chadema wanayeweza kumteka. Akipatikana na hatia afukuzwe tu na uanachama ili ccm wamchukue.
 
Mijadala hii kuhusu mgogoro wa CHADEMA kwani si umeshafungwa ama?
 
Labda bado wanahitaji "chalenji" jamani...mechi hainogi kama kuna timu moja tu uwanjani....labda yawe mazoezi.

Hata hivyo kufa kwa CDM kutawanyima posho za kwenda kuimarisha chama maana watakosa sababu.

Kuwepo kwa CDM ni ajira na faida kwa wengine.
 
Lema ni Jembe hanaga mipasho kama huyo Zitto Mchumia Tumbo.
 
zito ajieleze kwenye chama ajibu tuhuma zinazomkabili yeye ni kiongozi ametuhumiwa na chama chake na wala yeye siowakwanza kupewa tuhuma huo ni utaratibu mbona kelele nyingi mapovu yanawatoka bila mipaka hebu muacheni ajibu tuhuma zake hivi mtu akiwa na dini yake basi asiguswe akitoka kanda yake yeye asituhumiwe kumbe ndio maana chama chetu acha zamani hakishughuliki na kurekebisha viongozi kwa sadadu ya dini na ukanda wanapotoka ama kweli kazi ipo. tujifunze mfumo mzuri na sio nganjera hazisaidii.chama chochote ni zaidi ya Fulani yeyote yulu na hilo tulitambue wote watu tunapita lakini nchi iko palepale je unajua kutatokea nini pale yeyote atakapokuwa hayuko.ZITO JIBU TUHUMA KWA KUFUATA UTARATIBU WA CHAMA CHAKO huko nje yako mengi ya kweli na uongo pia
 
Wewe akiri zako zitakuwa matakonii, zitto unamlinganisha na huyu mla bangi, gombaa na n.k

Tatizo la Zitto anashindana na Watoto wa Mjini.Wenzake wamekujilia Mjini wakati yeye kafika kwa Treni akiwa na Mfuko wa Rambo kutokea Kigoma.Hata Sugu tu anamzidi Ujanja.
 
Magaziti yenye mlengo wa kisiasa ni mabaya sana-nakumbuka Genocide ya Rwanda jinsi media zilivyokahamasisha!!
 
Lema aishangaa CCM

Na Grace Macha, Arusha

Godbless LemaMBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), ameeleza kushangazwa na jitihada za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutaka Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe asichukuliwe hatua zaidi kwa madai ya kukinusuru chama kisisambaratike.

Lema alitoa kauli hiyo juzi wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kilombero.

Alisema kuwa CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani kinachowanyima CCM usingizi, walipaswa kufurahia kusambaratika kwao, lakini cha kushangaza viongozi wa chama tawala wamekuwa wakiwaasa wasimfukuze Zitto.

“Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wanalia wakitaka tupatane. Mbunge wao wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba naye analia kuwa CHADEMA tumefanya vibaya, tumrudishe Zitto.

“Sisi tunawauliza tukifanya vibaya ni faida kwao, kwanini wanalia. CCM wanalalamika CHADEMA hatuna demokrasia, ni chama cha kibabe, tumemwonea Zito, kwamba tutapasuka. Hivi tukipasuka wao wataimarika sasa wanalia nini badala ya kufurahi?” alihoji Lema.

Chanzo: T Daima

gazeti la udaku hilo
 
Tz daima ni la mbowe mbowe ni chadema hivo tz ni gazzeti la kuwatetea chadema haliandiki kwa weled
 
Wewe akiri zako zitakuwa matakonii, zitto unamlinganisha na huyu mla bangi, gombaa na n.k

Wewe nawe akili zako zitakuwa zimechanganyika na majimaji ya chini mbeleni, toka lini ukasikia Lema ana urafiki na watu wa CCM kama huyo Zitto wako?
 
Back
Top Bottom