Mimi kwanza naomba kuchukua fursa hii, kuwapongeza CCM kwa mkutano wao mkuu ambao tumepata fursa ya kuungalia live kupitia runinga.
Nimeguswa sana na kauli hii ya Mwenyekiti wa CCM kuwa "Ndani ya CCM, kuna nyoka mwenye ndimi mbili!", na kusisitiza huwezi kuona ndani kuna nyoka na wewe ukamuachia tuu!.
Swali kwa wana CCM, wapenzi na washabiki wao,
"jee nyoka huyu mwenye ndimi mbili ni nani?!.
"Jee ni lini CCM, iligundua kuwa inafuga nyoka ndani ya nyumba yake?!.
"Tangu walipogundua kuwa ndani nyumba kuna nyoka, walifanya nini kumuangamiza nyoka huyo?!.
"Jee kama ni kweli nyoka huyo yupo, na ikitokea ameisha totoa vitoto kibao, sasa CCM itafanya nini?!.
Na swali la mwisho, hili ni kwa wengine wote wenye matumaini ya mabadiliko 2015, leo ni 2012, CCM imeishamshtukia nyoka ndani ya chama chao, wanaanza kujipanga kumuangamiza, hivyo kuisafisha nyumba yake, hivyo kufikia 2015, nyumba ya CCM itakuwa ni safi iliyotakata!, bado 2015, mna matumaini ya mabadiliko?!.
Nawatakia ufuatiliaji mwema wa Mkutano Mkuu wa CCM.
Wanabodi,
Tulijuzwa kuugua kwa waziri wetu mstaafu Mhe Edward Lowassa wa kuomba waliomba na wakumtakia afya njema wachache wasio jali afya za wengine hasa waliowaongoza kama viongoz walikejeli
Ashukuriwe aliyemjalia afya njema na kurejea salama nasi tumtakie afya njema na katika harakati za siasa. Yuko Dodoma katikati ya wajumbe kwa kuchelewa hakupenda kukaa mbele.
.
Wanajamvi tutambue uwepo wa Mtanzania mwenzetu mwanasiasa mwenye malengo ya kuendelea kuwatumikia wananchi
Kwenye mkutano wake wa mkutano mkuu Dodoma amesema "CCM ni chama kikubwa hakina mbadala KWA SASA japo kuna ndugu zetu (CDM) wanajaribujaribu ila kwa sasa hawawezi labda kwa badae"
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.