Dakika hii hapa Dodoma Kikwete amezungumza kuwa, nanukuu tutajenga barabara, zahanati n.k ila hili la sisi CCM kuonekana kukumbatia rushwa litakigharimu chama
Muite Mjeshi Ngwilizi na tume yake yenye wajumbe wabovu na wasio na maadili kama Gosbert Blandes wamfanyie interview Kikwete kuthibitisha ni nani kapokea rushwa, kiasi gani, wapi na tarehe ngapi na kwa kiasi gani akishindwa tu kuthibitisha, Anna Makinda nenda mjengoni kaa katika kiti chako kilichonyanyuliwa juu ukiwa na vazi lako lililonakishiwa kwa vito vya thamani, toa tamko lako la kumpa onyo kali maana kauli ya Rais ni kauli ya nchi kama unafikiri kuwa hivyo ndivyo tunaweza kupambana na rushwa hapa nchini.
Maana mnafikiri kuwa vita dhidi ya rushwa ni kupata picha za CCTV au kumkuta mtu na noti ambazo namba zake zimerekodiwa mapema huko polisi au TAKUKURU. Hizo ni mbinu za zamani sana watu sasa wanatransfer fedha electronically, wewe na Ngwilizi endeleeni kusubili uthibitisho wa kumkuta mtu na noti mfukoni. Tena eleweni kuwa sasa rushwa si lazima iambatane na fedha hata ngono au upendeleo wa nafasi unaweza kutumika kama kihalalishi cha rushwa. Endeleeni sana kuwasikiliza akina Gosbert Blandes Mbunge kilaza toka sekondari ya kilutheri Morogoro aliyekwenda Bungeni na kusema kuwa katumwa na watu wake kuwa Mswada wa sheria ya tume ya marekebisho ya Katiba upite bila marekebisho wakati hata hajafika jimboni kwake, mtu ambaye hana kabisa uadilifu ndiye mnamwona anafaa. Mnaona sifa kumtangaza Tundu Lissu, Maswi, Mnyika au Muhongo kuwa walikurupuka na mnatuletea vi statement mlivyovichagua mnaacha walichowambia kwenye Tume.
Endeleeni na kazi yenu ya kuwasafisha wezi huku tukiwakatisha tamaa wale wanaojitahidi kuchapa kazi na kuonyesha watu kuwa inawezekana tukapata viongozi waadilifu ndani ya Tanzania na hata ndani ya CCM na wakasimamia maslahi ya umma tutaona mtakachovuna!!