Mkutano wa CCM Kizota, Novemba 11-13, 2012

Mkutano wa CCM Kizota, Novemba 11-13, 2012

Kurunzi

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
10,197
Reaction score
11,629
Wanaotegemewa kuchaguliwa leo, utaratibu wa zamani ulikuwa ni wagombea wote wa NEC wanapigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu.

Utaratibu wa sasa ni kwamba wajumbe wa NEC wanapatikana kwenye ngazi za chini yaani wilayani na kwenye jumuiya za chama ila bado kuna nafasi nyingine za NEC zitapatikana kupitia huu mkutano mkuu wa chama ambazo ni kumi Tanzania bara na kumi kutoka Zanzibar.

Hivyo mchuano mkali uko kwenye hizo nafasi kumi Tanzania bara ambapo kuna wagombea zaidi ya thelathini.
Alipojieleza January Makamba alishangiliwa, Jk akasema hairuhusiwi...

Alisema anaomba kwa kuwa anaamini kwamba anaimudu na kwamba Mwenyekiti akitakiwa kutoa ithibati atasema kwa kuwa amekuwa mwakilishi wake kwa muda mrefu....

Kupata uongozi wa chama ni fadhila na naomba mnipe fursa ya kulipa fadhila ya kuilipa... Nataka chama kitume ujumbe kwa dunia kwamba kinao vijana wenye uwezo
Membe akiomba kura....

Miaka mitano nilisimama hapa nikapata kura za ushindi, sababu za 2007 bado zipo, niliomba ili nimsaidie m/kiti kukisaidia chama kukieleza duniani.... CCM lazima tuipe sura ya kimataifa... Dunia inajua kwamba CCM ni chama cha kimatafa kimeshiriki ukombozi... Kwa nafasi yangu tuue ndege wawili kwa jiwe moja... Kura zote za ndio tuziweke kwangu

Amesema kwa nafasi yake ataisaidia CCM kupata marafiki zaidi nje ya nchi
- Matokeo ya uchaguzi hadi kesho Novemba 12, 2012
 
Hivi hapo Dodoma wanatizaman vipi hawa jamaa, wale walioshindwa kwa rushwa japo nao walitoa ila ikawa kidogo wakabwagwa, makundi yalivyokamiana kwa kunyukana waziwazi mpaka kufikia hatua ya kutoleana mabastola yakigombea kuongoza ilihali waongozwaji hawajui hata kipi wanafaidika maana maisha ndiyo kwanza yanazidi kuwa magumu.

Watu wanataka madaraka si kwasababu wananchi wanawahitaji ili wawaongoze kuifikia nchi ya ahadi hapana bali ni kwasababu mtu anauwezo wa kunua kila kinachoweza kumfanya awe kiongozi na uwezo huo katika nchi ya watu waliokata tamaa ni PESA!

Wababe wote hawa wanazo ngoja tuone hatma yake, who gonna be the LOSER&WINNER na baada ya hapo what NEXT for the LOSER and the WINNER!
 
Tbc wanarusha mkutano wa CCM unaofanyika Chimwaga ni mkutano wa nane utakaofunguliwa na JK, pia utafanyika uchaguzi wa wajumbe 20 wa NEC

Wanaanza saa ngapi na miye nishuhudie?
 
Huo ni mkutano mkuu wa watoa rushwa!na rushwa ya leo inagawanywa kisayansi zaidi hata takukuru hawezi kuona
 
Tbc wanarusha mkutano wa CCM unaofanyika Chimwaga ni mkutano wa nane utakaofunguliwa na JK, pia utafanyika uchaguzi wa wajumbe 20 wa NEC

Mbona nasikia nafasi ni kumi tu na wagombea ni kama 31 na ndiyo maana watu wanahisi mtifiano utakuwa mkali sana????

Fafanua kuhusu hili la wajumbe hao wanaotegemewa kuchaguliwa leo.
 
Mbona nasikia nafasi ni kumi tu na wagombea ni kama 31 na ndiyo maana watu wanahisi mtifiano utakuwa mkali sana????

Fafanua kuhusu hili la wajumbe hao wanaotegemewa kuchaguliwa leo.

Wajumbe kumi ni kutoka bara na wajumbe kumi ni kutoka zanzibar.
 
Wakuu, mwenye list ya majina ya wagombea nafasi ndani ya CCM atupe!
 
Wajumbe kumi ni kutoka bara na wajumbe kumi ni kutoka zanzibar.

Ok hapo umenyoosha kaka, kwa upande wa Zanzibar wala hakuna shida sana, ngoma ipo bara.

Nausubiri mtanange huo kwa hamu sana, ngoja nijongee kwa tv haraka.
 
kuna mama huwa namuona ITV anaomba msaada wa kutibiwa mguu india!kweli wapo hapo dom huku yule mama akitaabika?
 
Mbona nasikia nafasi ni kumi tu na wagombea ni kama 31 na ndiyo maana watu wanahisi mtifiano utakuwa mkali sana????

Fafanua kuhusu hili la wajumbe hao wanaotegemewa kuchaguliwa leo.
Mkuu utaratibu wa zamani ulikuwa ni wagombea wote wa NEC wanapigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu.

Utaratibu wa sasa ni kwamba wajumbe wa NEC wanapatikana kwenye ngazi za chini yaani wilayani na kwenye jumuiya za chama BUT bado kuna nafasi zingine za NEC zitapatikana kupitia huu mkutano mkuu wa chama ambazo ni kumi Tanzania bara na kumi kutoka Zanzibar.

Hivyo mchuano mkali uko kwenye hizo nafasi kumi Tanzania bara ambapo kuna wagombea zaidi ya thelathini.
 
Kama nilivyoeleza katika thread yangu niliyoitoa wiki mbili zilizopita ni kuwa kuna Mpambano mkali kati ya Mh Bernard Membe (anaewakilisha Kundi la Wapinga ufisadi) na Mh Edward Lowasa(aliye katika kundi la Mafisadi) katika kuwania kuteuliwa kupeperusha bendera ya Chama chetu mwaka 2015. Matokeo ambayo yamejiri hivi karibuni, kwangu mimi naona hadi sasa Scoreboard inaonyesha Lowasa anaongoza 2-1 na sasa ni Half time.

Lowasa ndie aliyetangulia kupata bao baada ya kumsambaratisha vibaya Membe katika chaguzi za NEC wilaya mbalimbali Tanzania. Katika chaguzi hizo, Lowasa alimtimulia vumbi vilivyo bwana Membe kwa kambi yake kushinda kwa ushindi wa kishindo.

Wakati Membe akishangaashangaa, Lowasa alipiga bao la pili fastafasta baada ya Kundi lake lenye nguvu kubwa ya kifedha kutwaa Jumuia zote za chama ie Wazazi, Vijana na Wanawake na kumwacha Membe akin'gaa macho!

Membe, baada ya vipigo hivyo viwili vitakatifu nae alijufutafuta vumbi na kujipatia bao moja ambapo Mwanachama mzoefu na Mwadilifu na anayeuchukia kwa dhati Ufisadi Mh P. Mangula kuchaguliwa kua Makamu Mwenyekiti wa CCM Tz Bara na wajumbe wa NEC. Kwa hakika kitendo cha kuchaguliwa Mangula ni pigo kubwa kwa kundi la Lowasa kwani Mangula ni mtu anayeichukia rushwa kwa dhati na DAIMA haoni aibu kuweka bayana msimamo wake huo. Mwaka 2005 akiwa Katibu Mkuu wa CCM hakusita kusema katika kamati ya maadili ya chama kua JK na kundi lake la akina Rostam hawafai Urais kutokana na matumizi yasio halali ya pesa ! Kutokana na kitendo hicho ccm ilimpotezea kabisa. Alijaribu kugombea Uenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa na kugoma kabisa kutoa rushwa na matokeo yake akashindwa na mhuni Sanga aka Jah People. Akagombea NEC na kuhutubia sera za CCM wakati wenzake wakigawa rushwa nako akaishia kukosa! Hivyo, kuchaguliwa kwa Mangula ni pigo kubwa kwa kundi la Lowasa.

Hapa Dodoma kwa sasa, mpambano huu utaendelea kwa nafasi ya Mwenyekiti. Lowasa na kundi lake wanaonekana hawataki J. Kikwete aendelee kua Mwenyekiti kwani wanaona nae ni mmoja kati ya walioshiriki kuharibu nyota ya Lowasa!. Hotuba aliyoitoa Lowasa mwezi Novemba 2011 NEC-Dodoma ambapo alimwaga mboga na ugali kwa pamoja na kumpelekea mwenyekiti mashambulizi makali ambayo Mwenyekiti alishindwa kabisa kuyajibu yanaonyeshafika kambi hiyo isivyo na imani na Mwenyekiti. Aidha,Kitendo cha Bashe, Freddy na Malisa kutapanya mabango mji mzima wa Dodoma kumkataa JK kuendelea kua Mwenyekiti inaonyesha azma hii ya kumkataa Mwenyekiti ambaye upande wa Lowasa unajua fika yuko upande wa Membe. Hivyo JK akichaguliwa tena kuwa mwenyekiti Lowasa atakua kapigwa bao la pili.

Na jambo kubwa na la mwisho linalosubiriwa kwa hamu KUBWA ni kuona kama Membe atafanikiwa kuwemo katika TOP TEN YA NEC. Kundi la Lowasa limetumia "yale mambo yetu" kuwashawishi wajumbe wa NEC kumsabaratisha Membe. Kundi hilo la Lowasa linaamini hiyo ni kazi nyepesi kama kumsukuma mlevi kwani watakaofanya uchaguzi huo wa NEC ni wajumbe wa NEC ambao 90% ndio waliochaguliwa majuzi na wako kundi la Lowasa. Bashe alitamka wazi kwenye press conference kwamba wanafanya kila njia Membe asipite. Katika kuhakikisha wanafanikiwa wameishatayarisha majina KUMI ya watu ambao wanafaa kuingia kumi bora ambapo jina la Membe halimo na wamekua wakiipitisha orodha hiyo kwa wajumbe mbalimbali wa NEC ili Membe atoswe.

Iwapo watafanikiwa hilo, basi huo ndo utakua MWISHO wa hekaheka za Membe kuelekea Ikulu kama vile Sumaye nae alivyoangukia pua na kuishia kulalama tu! Hoja hapa ni kwamba, kwakua chama makini Chadema kinaendelea kuitimulia vumbi CCM kila kukicha hivyo kumpitisha mtu ambaye hata kwenye NEC ya chama chake tu hakubaliki, Watanzania watamkubalije?Kwa upande mwingine, iwapo Membe atashinda litakua ni pigo KUBWA kwa kundi la Lowasa kwa hoja kwamba 90% ya NEC ni wafuasi wa Lowasa, sasa wamewezaje kumchagua Membe?

Yangu macho, hii imekaaje wadau?
 
its sickening to see those green attire, i nearly vomit when i first tune to TBCCM and found bribe masters throwing a huge party!
 
Wakuu, mwenye list ya majina ya wagombea nafasi ndani ya CCM atupe!

Kwa ninaowakumbuka kuwa idadi ya wagombea wapo 31 nafasi ni kumi. Wengi ni mawaziri na viongozi jambo linaloleta utamu hapo:

January Makamba, William Lukuvi, Bernard Membe, na wengine humo.
 
Back
Top Bottom