Mkurugenzi wa upimaji na ramani aagiza hati na.56371 kufutwa

Kitomai

JF-Expert Member
May 21, 2009
1,061
281
Mkurugenzi wa upimaji na ramani amemuagiza mpima ardhi wa Manispaa ya kinondoni kufuta upimaji wa shamba na.3797 na 3798 plan na. E'257/108 Kimara Bonyokwa Manispaa ya kinondoni. Agizo hili litolewa kufuatia hukumu ya Mahakama ya Ardhi na Nyumba ya wilaya ya Kinondoni na Mahakama kuu ya Tanzania kuhusu mgogoro wa Mashamba Na. 3797 na 3798 kesi Na.303 ya 2008. Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani amefuta upimaji Plani Na,E'257/108 kwa mjibu wa Sheria ya Upimaji Ardhi Siura 324 Kifungu cha 5 na 17(4). ''Upimaji huu umefutwa kwa sababu ulifanyika kwa udanganyifu na kutozingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa''. Hivyo, amemuagiza Mpima Ardhi wa Manispaa, Manispaa ya kinondoni, ang'oe Mawe yote ya Mashamba hayo na kuwakilisha Hati za kung'oa Mawe (certificate of Removal) kwa Mkurugenzi wa Ramani na kwa kumbukumbu zake. Pia , kumbukumbu zote za upimaji zifutwe kwenye "Survey Registration System". (SRS) baada ya Hati Miliki zilizopo kufutwa na Kamishina wa Ardhi na Usajili kufutwa na Msajili wa Hati. Habari hii imetokea leo tarehe 9 September, 2010.
 
Sawa taaarifa nzuri yenye kuwa na mambo ya kujifunza, lakini unaripoti tu kuwa ramani imefutwa, kulikuwa na nini? What were the facts of the case, ni nani alitaka nini au alifanyiwa nini mpaka ikapelekea kufutwa kwa ramani, maana sio kawaida,nadhani hii itakuwa mara yangu ya kwanza kusikia.

Kawaida ramani zote zinapitishwa na Mkurugenzi, sasa hapa yeye tena anafuta kile alichopitisha, imekaaje hii?
 
1465571860720.jpg
 
Back
Top Bottom