Mkurugenzi wa NHC amkera Sabodo.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkurugenzi wa NHC amkera Sabodo..

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by ngoshwe, Sep 13, 2011.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145


  [​IMG]  Bw. Nehemia Mchechu


  Pengine inatafsiriwa kana kwamba Bw. Nehemia Mchechu, Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba (NHC) ameonekana kana kwamba anajitafutia umaarufu wa haraka katika nyaja ya uongozi na hasa kupitia vyombo vya habari kwamfano:

  Alitumia waandishi kuwapa semina yenye kugharimu mamilioni ya Fedha za shirika kuwafundisha waelewe shirika ikwemo kumtumia Mjomba Mpoto kwenye matangazo.

  Sasa amekuwa akionekana katika vyombo vya Habari hasa TBC 1 akitangzana mikakati ya shirika nk kwa kutumia fedha za shirika hilo ambalo mpaka hivi sasa limejikita zaidi kujenga na kukarabati nyumba maeneo ya mjini na kukosa kuwafikia wanyonghe walio wengi.

  katika Gazeti la Mwanachi leo tarehe 13 Septemba, 2011, Bw. M.R.J. Sabodo ameandika makala ya malalamiko na kuhoji uhalali wa maswali ambazo NHC limeandaa kwa ajili ya kuuliza wapangaji wake. Maswali hayo mengi yanaoekana hayana mantiki yoyote ya kuboresha huduma za shirika hilo la Taifa. Kwa maoni ya Sabodo, ni ya kibaguzi na hata alipoongea na Mhe.

  Waziri Mkuu nae ameshangaa kuona maswali kama hayo. Ukiyasoma maswali hayo utaona yanataka kuwaanika wapangaji wake kihali na kiuchumi. Maswali hayo yanataka kujua pamoja na mengine yanataka kujua taarifa binafsi za wateja (utaifa,uasili wa wapangaji kwa kuuliza "wewe ni mtanzania wa asili ipi (ulaya, asia, mweuisi nk) (originality), makazi yao, unahudumiwa na Benki gani, shule wanazosoma watoto, nk.

  Kwa maoni ni kuwa Kama wao NHC wanataka kukusanya mapato zaidi, waweke mfumo unaoeleweka, hizi taarifa wanazotaka wapangaji watoe ni taarifa ambazo kimsingi zilipaswa kuwa sehemu yan mkataba wa pango na sio sasa wakati tayari mkataba unaendelea. Huu ni uelewa mdogo wa Mkurugenzi wa NHC, hizi taarifa hajui zinaweza kutumiwa vibaya dhidi ya wapangaji?

  Kuna madai kuwa Mkurugenzi huyu alipatikana kimagumashi tu na hakuna uhakia kama anajua jinsi gani mashirika ya umma yanapaswa kuendeshwa.

  Kuna madai kuwa pale NHC sasa kuna mikataba mingi ya hovyo ya wajiriwa toka ndani na nje ya nchi walioletwa na Uongozi mpya, na mingi itakuja kuwa mzigo kwa taifa...tusipoangalia, badala ya kufufua shirika, Shirika litaangamia kwa Mipango ya Kusadikika ya Huyu Mkurugenzi wa sasa.
   
 2. M

  Mutu JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2011
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Duh kumbe mkurugezi poa sana ..ukiuliza kwa lipi soma hapo juu.. !
   
 3. T

  Tsidekenu Senior Member

  #3
  Sep 13, 2011
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 141
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  hahaaa wanalo, kaza buti kaka. mi nakuaminia kazi unaiweza! huyo sabodo sijui nani, just ignore him!!!
   
 4. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,431
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  safi nehemia wabongo mmezoea vya bure tena inaelekea upo kenye nyumba wala hulipi kodi na utatoka tuu
   
 5. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2011
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 743
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  big up Nehemia sawazisha
   
 6. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Sasa habari hii inakaaje kwenye chit chat? Si ipelekwe jukwaa linalostahili?
   
 7. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2011
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Bebii...ambaye amepanga na halipi kodi ni nani? kama hujui Mustafa jafar sabodo ni nani; nakushauri ufuatilie thread wanaujua wachangie kisha ndio utupie ya kwako....
   
 8. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,431
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  nimemwambia alieleta mada huyo ngoswe sijui
   
 9. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  labda kashindwa kujua ipo jukwaa gani pengine ungetusaidia iende jukwaa gani..
   
 10. bi mkora

  bi mkora JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 262
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nadhani swala lililojadiliwa hapa ni maswala yakuingilia taarifa binafsi za kibenki na kijamii pamoja na ubaguzi, samahani naomba unielekeze swala la kutokulipa kodi limeainishwa wapi hapa???
   
 11. bi mkora

  bi mkora JF-Expert Member

  #11
  Sep 13, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 262
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jukwaa la nyumba na makazi lipo humu??
   
 12. bi mkora

  bi mkora JF-Expert Member

  #12
  Sep 13, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 262
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  google who z sabodo.
   
 13. k

  kashwagala Senior Member

  #13
  Sep 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimependa uliposema "inaonekana hajui jinsi mashirika ya umma yanavyoendeshwa",mashirika yapi hayo unayoyazungumzia mkuu?kwani yote yashakufa na NHC ndo inafufuliwa....sijakuelewa kabisa mkuu.Nakubaliana na mbunge Kafulila aliwahi kusema...wanaopenda neno la mtu huyu anatatafuta umaarufu wamefirisika kifikra,akaongeza kuwa kama watu wanatafuta umaarufu kwa manufaa ya wengi basi umaarufu huo unakubalika.

  Mimi sikuungi mkono kabisa kwa thread yako iliyojaa chuki binafsi,kwani Sabodo si kama binadamu yeyote tu anayeweza kutoa maoni yake ambayo hayana mashiko?Sioni ubaya wowote kwenye hayo maswali na kama wewe ni mpangaji wa NHC ukitendewa ndivyo sivyo si utaratibu wa kudai haki kwenye vyombo husika unafahamika?

  Nafuatilia vipindi unavyovisema,mimi binafsi vinanipa moyo sana na kuwa kwa mipango ya mshkaji kama itatekelezeka nishaanza kuona dalili za kumiliki House ya mkopo au kupanga kwenye ka apartment ka NHC maana huku uswahilini baba wenye nyumba wanatukamua mpaka basi.Tuache hizo jamani....
   
 14. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #14
  Sep 13, 2011
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Sabodo anawaza NHC aliyounda Nyerere na school of thought behind its making. Its true kwa style ya Nehemia wa TZ wengi hawataweza kukaa ktk nyumba zile. School of thought ya Nehemia ni tofauti. I agree with NHC changing its face,however,since it was established (its Act) was to offer affordable nice housing than Nehemia aanze na kubadilisha Act kwanza. Watu kama Sabodo wajue kabisaa kuwa shirika ni la Kibepari na anayekaa ndo lazima awe na hela.

  Kwa kuwa ana mpango wa kujenga na kuuza nyumba kwa wapangaji wake lazima awe na data zao. Wanasema nyumba zinakaliwa sana na wahindi ni lazima ajue kama ni kweli kwa maeneo gani na atasawazishaje tofauti hizo. Lazima ajue km tenants wana uwezo wa kuja kununua nyumba anazojenga. Kama ningekuwa yeye ningefanya hivyo.

  Mianya ya rushwa na kulangua nyumba imepungua sana NHC ndo maana watu hasa staff wanalalamika sana.
   
 15. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #15
  Sep 13, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145

  Yani unataka tukuamini kwamba NHC itafufuka kwa Mchechu kufahamu origin ya wapangaji wake? anataka kujua wahindi ni wangapi, wazaramo ni wangapi na wakurya ni wangapi? hiyo ni kazin ya taasisi ya takwimu kutokana na sensa zinazofanyika, na bila shaka hao ndo wanaweza kumsaidia kuwajua wapangaji wake.

  Kwamba mpangaji X anasomesha watoto wake shule ya saint kayumba B itawaqsaidia nini NHC? Huyu mchechu hatafuti umaarufu aliouzungumza kafulila, huyu anatafuta umaarufu wa bei chee!! Na sidhani kwamba wananchi wanamuamini kiasi hicho, sana sana anajaribu kufunika mashimo ya makando kando ya fedha za EPA kwani benki aliyokuwa akiiongoza ndio ilitumika kutorosha fedha za EPA, hakustahili kuwa mkurugenzi kwenye shirika la umma hata kama linaelekea kaburini.

  Katika hili mzee sabodo yuko sahihi kabisa.
   
 16. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #16
  Sep 13, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Naona watu mnajaribu kupaka rangi upepo.

  Sheria ya kutaka shirika lijue origin ya wapangaji wake haiwezi kuanzishwa ndani ya nchi hii kwa wakati huu ndugu yangu, hayo ni mawazo ya kijima kabisa wala hakuna chembe ya ubepari hapo.

  Wao NHC wajenge nyumba, waziweke sokoni kwa zile za kuuza na pia waweke utaratibu wa kupangisha kwa bei ya soko kwa zile watakazzoamua kuzipqangisha.

  Mbona huku uswahilini tunaishi nyumba za kupanga na tunalipa kodi kubwa kuliko hiyo ya NHC na wenye nyumba wetu hawana muda wa kufahamu watoto wetu wanasoma wapi na kwamba tumetokea wapi??

  Tusiwe wepesi kuvutika na mawazo ya hovyo kiasi hiki, Mchechu atafute mbinu nyengine ya kuinua kipato cha NHC sio hii ya kuulizana maswali ya kitoto, mi ningekuwa mpangaji wao nisingeyajibu hayo madodoso yao.
   
 17. mchapa shughuli

  mchapa shughuli JF-Expert Member

  #17
  Sep 13, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 524
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 80
  piga kazi mchechu nhc lazima iende kisasa tupate nyumba za kutosha..moto huo huo
   
 18. P

  Patrick Nyemela JF-Expert Member

  #18
  Sep 13, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sabodo ameingia kwenye harakati ya kutetea wahidi akidhani NHC ina mpango wa kuwafukuza kwenye nyumba baada ya kuulizwa uraia. Nehemiah kaza buti sabodo anamatatizo yake nakumbuka miaka ya 2001 aliwahi kugombana sana na NHC akitaka ubia kwa nguvu pale upanga ambako alitaka kujenga jumba la cinema. Baada ya kupigwa chini akaanza kuichafua kupitia magazeti.

  Nehemiah kaza buti na kazi yako nzuri inaonekana na hakikisha wahidi wanalipa kodi stahili pale upanga na mji waache chokochoko maana tayari nyumba zote za mijini wamekalia wao, sisi wamatumbi lazima tupate makazi bora pia na tutapata kupitia kodi hizo.

  By the way Nehemiah muangalie sana muhindi anajiita Rajpar anafanya shughuli za meli, yeye ndiye anayeleta chokochoko na kumtumia sabodo kama msemaji wao. NHC kaza buti mpaka kieleweke nataka kuwaona wahidi nao wakiishi kufuatana na uwezo wao, kwanini nao wasiende kule tandika, ubungo au manzese kama NHC mna nyumba huko.
   
 19. k

  kamalaika Senior Member

  #19
  Sep 13, 2011
  Joined: Mar 16, 2007
  Messages: 187
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  ha ha ha . kwa kuuliza mtoto anasoma wapi. una account bank gani. maisha yangu binafsi anayatakia nini? Kama nimejinyima namsomesha mtoto wangu shule ya bei mbaya sitakiwi kuishi kwenye nyumba za NHC?
   
 20. P

  Patrick Nyemela JF-Expert Member

  #20
  Sep 13, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Unatakiwa kuishi katika nyumba hizo lakini ujue maswali hayo yanalenga kujua kipato chako na uwezo wa kumudu ongezeko la kodi. Ni vizuri ukajua siku zote hawa jamaa wa NHC wakitaka kupandisha kodi huwa na migogoro mingi na wengi wa wapangaji wao hujiita masikini. sasa taarifa hizo sitawazaidia sana.
   
Loading...