Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO unaamini katika uchawi au utendaji kazi?

Day 1 gongs

JF-Expert Member
Oct 5, 2022
340
657
Habari members,

Huyu Mhandisi Nyamo-Hanga tangu amepokea kijiti toka kwa Maharage ameshindwa kuhaminisha umma wa Tanzania ya kwamba anafaa kuendelea kuikalia nafasi hiyo adhimu kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa licha ya kupewa kipindi cha uangalizi cha miezi sita na Mh. Raisi Samia.

Shirika la umeme linakosa mbinu mbadala ya kupata wazalishaji wa dharura (mfano AGGREKO) ili kuondoa kiwango cha mgao uliopo yapata miezi kadhaa na kuelemea kwenye mradi uliojaa habari nyingi za ukweli na uongo (JNHP) kila uchwao.

Ni kwamba kiwango cha kufikiri kwake kidogo au ameridhika na kadhia ya kukosa umeme kwa Watanzania na mapato kwa serikali kupitia kodi, juu ya yote utakuta yupo na safari nyingi za kikazi bila tija yeyote.

Huduma kwa wateja zimezorota sana, hata ile mifumo ya kimtandao (NIKONEKT) nayo imekuwa mazoea kama awali, wateja wakilipia kufungiwa umeme visababu kibao; mara hakuna nguzo, tena mnaenda mbali zaidi shirika halina vifaa kamilifu!

Hivi hizo pesa walizolipa wateja mshaona si lolote? Wateja wanapata shida ya umeme kupata huduma hadi utumie nguvu au upenyeze rupia, hivi ni huduma gani mnatoa ya hivi au hili nalo la kuitiwa waganga?

Watoa huduma wapo na lugha chafu kwa wateja tena kinzani, utadhani ni sehemu ya wanywaji wasiokuwa na muelekea (vilabu), maana kila mtu huku site ni muongeaji. Hii haikubaliki kabisa, hili nalo linataka mganga tuone kwamba unaamini katika kazi au ni utawala gani unasimamia wewe Nyamo-hanga?

Inaelekea nusu ya mwaka wa fedha lakini miradi mingi hujaitolea ufafanuzi namna ya kuipatia materials licha ya kukuta mtangulizi wako na mipango ya kusogeza manunuzi jirani na ofisi yake (HQ).

Je, hili nalo linataka nguvu ya giza kuonesha kwamba wewe ni kiongozi? Kuwa na maamuzi ya kiongozi yenye tija haswa ukizingatia TANESCO ni shirika la kifundi zaidi ya 80%, sasa bila vifaa tutarajie utakuwa na wafanyakazi wengi unaowalipa mishahara na safari kwa kazi ambazo hazina chumo kwa Shirika zaidi ya Hasara.

Rudisha huduma karibu na wateja katika baadhi ya vituo vilivyotolewa na mtangulizi wako (Viwanda na Tegeta wilaya) kwani wananchi wanapata usumbufu mkubwa sana na ndiyo kero zimejaa huko.

Itathmini safu ya wasaidizi wako wengi wao ni weupe mno kiutendaji wamekaa kwa mazoea mno (wanawakandamiza sana watu wa chini yao haswa kwenye maslahi na ukuaji wa kiutendaji) hata masuala ya kulisemea shirika wamekuwa na kigugumizi (weka mhandisi alisemee shirika kwa weledi na si blah blah).

Hitimisho: Usijifungie ofisini na kujificha nyuma ya migongo ya management ya shirika shuka kwenye vituo kutana na wataalamu wakupe chachu za kuboresha utendaji wa shirika hapo utaepuka kuamini katika uchawi kufikia mafanikio na kuelemea katika utendaji zaidi.
 
Kwanza umeme mbona bado unakatika na mvua tele mpaka mafuriko.What is the issue?mafuta yameshuka bei
 
Bado hamjasema, mtasema tu

IMG_20211228_160309.jpg
 
Mimi naona bora tanesco waachane tu na huu mchezo kama kweli lengo lao ni watu wazidi kununua magenereta na mafuta kwa wingi, maana mfano huku kwetu tangu huo mgao uanze sijawahi kusikia jirani hata mmoja akiungurumisha genereta hata kwa mbali tu kama wapo wanaoendelea kununua bado ni wachache, sasa hivi watu ni mwendo wa solar tu na wengine ndio wamemute kabisa umeme ukikatika unaona giza wanatumia torch kwahiyo hao wahuni watafute njia nyingine za kuendelea kutoka kibiashara wananchi nao washachoka
 
Tunamuonea tu!

Tatizo la umeme ni uongozi wa juu na sio hao wasaidizi wanaowekwa na kutolewa kilasiku.

UONGOZI WA JUU NDIO UNAPASWA KUCHUKUA MAAMUZI YA KU-ALLOCATE NGUVU/PESA KWENYE KUTATUA CHANGAMOTO YA UMEME.

Yangu ni hayo tu!

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Back
Top Bottom