Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,028
- 144,382
Mimi nafikiri wakati umefika Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa awe anawajibika kwa bunge pia.
Taasisi hii kuwajibika kwa raisi pekee si jambo jema kwa ustawi wa nchi hii.
Taarifa zinaweza kwenda Ikulu lakini pia zinaeweza kufikishwa bungeni.Taarifa nyeti na za siri zinaweza kuwekewa utaratibu maalumu.
Tusijali hata kama tutakuwa nchi ya kwanza duniani kuwa na utaratibu kama huu bali tuangalie mazingira ya nchi yetu na hasa aina ya viongozi tulionao.
Ni imani yangu,utaratibu kama huu ungekuwepo,hizi kashifa zisingekuwepo au zisingekuwa za kiwango hiki.
Pia,sheria ibadilishwe ili taasisi hii isiishie kutoa ushauri tu bali iwe na mamlaka ya kuchukua hatua ili iweze kuepusha majanga kama haya ya Escrow.