Mkurugenzi Mkuu Idara ya Usalama wa Taifa awajibike kwa Bunge pia

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,985
Mimi nafikiri wakati umefika Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa awe anawajibika kwa bunge pia.

Taasisi hii kuwajibika kwa raisi pekee si jambo jema kwa ustawi wa nchi hii.

Taarifa zinaweza kwenda Ikulu lakini pia zinaeweza kufikishwa bungeni.Taarifa nyeti na za siri zinaweza kuwekewa utaratibu maalumu.

Tusijali hata kama tutakuwa nchi ya kwanza duniani kuwa na utaratibu kama huu bali tuangalie mazingira ya nchi yetu na hasa aina ya viongozi tulionao.

Ni imani yangu,utaratibu kama huu ungekuwepo,hizi kashifa zisingekuwepo au zisingekuwa za kiwango hiki.

Pia,sheria ibadilishwe ili taasisi hii isiishie kutoa ushauri tu bali iwe na mamlaka ya kuchukua hatua ili iweze kuepusha majanga kama haya ya Escrow.
 
Tatizo naona raisi aliyepo madarakani haaminiki lakini mlolongo wa mkurugenzi wa UT kuripoti bungeni utahatarisha usalama wa Taifa. After all wabunge wenyewe ndio hao akina Livingston Lusinde. Tumpunguzie madaraka raisi ndio suluhisho
 
Mkuu awajibike kwa bunge mbalo majority hawana integrity, hawaweki maslahi ya nchi mbele? yani Tanzania bado sana kufika level hizo...
 
Iwe na uwezo wa kuchukua hatua ipi !? Ya kukimbilia mahakamani !? Au kutumia nguvu kuzima matukio !? Nadhani hujui ni kwa nini bunge ni taasisi pana. Ila rais yuko mmoja tu.... Hawakukosea waliopanga hivyo
 
Tatizo naona raisi aliyepo madarakani haaminiki lakini mlolongo wa mkurugenzi wa UT kuripoti bungeni utahatarisha usalama wa Taifa. After all wabunge wenyewe ndio hao akina Livingston Lusinde. Tumpunguzie madaraka raisi ndio suluhisho

Kwani taarifa kama ya Esrcrow ingefikishwa bungeni haya yangetokea?Taarifa hizi naamini zilifika Ikulu ila ndio hivyo tena.

Hivi taarifa kama za uhujumu uchumi zikifishwa na TISS bungeni kuna ubaya?
 
Hivi taarifa kama ya Esrcrow ingefikishwa bungeni haya yangetokea?Taarifa hizi naamini zilifika Ikulu ila ndio hivyo tena.

Hivi taarifa kama za uhujumu uchumi zikifishwa na TISS bungeni kuna ubaya?
Kani si imefikishwa bungeni na ndo maana hayo yametokea? Hivi kila taarifa wanayopata Idara ya Usalama wa Taifa ikipelekwa bungeni nchi itakalika kweli? Mie naamini kuwa hawa jamaa wana taarifa nyingi na nyeti. Maadili ya kazi yao ndo yanayosababisha kuwe na amani wakati wote vinginevyo hali ingekuwa mbaya sana
 
Kaka Salary Slip, leo u ekunywa gongo nini? Je mawazo hayo ulipeleka kwenye tume ya Warioba au ulimfikishia mbunge wako ili akusemee bungeni?
 
Kaka Salary Slip, leo u ekunywa gongo nini? Je mawazo hayo ulipeleka kwenye tume ya Warioba au ulimfikishia mbunge wako ili akusemee bungeni?
Dr Slaa kaharibu sana vijana wengi. Yawezekana ubongo wa Salary Slip umeathiriwa na kilevi cha gongo na bangi
 
Naona Salary Slip unataka kupolitisize shughuli za Idara ya Usalama wa Taifa. Vipi nafasi ya CAG, TAKUKURU na Polisi?

Najua kuna taarifa ambazo haziwezi kuwekwa public kupitia bunge.Lakini kwa mfano TISS wakagundu njama za uhujumu uchumi au huu ufisadi na kuzipeleka taarifa hizo bungeni kuna ubaya gani?

Kama taarifa zinapelekwa serikalini ni kwanini sasa hizi hujuma hazizuiliki?

Tatizo ni moja tu nalo ni kuumpa mtu mmoja madaraka ya karibu kila kitu!

Siamini kama kili kitu kinachofanywa na TISS kinapaswa kuwa siri hata bunge.
 
Mkuu Salary Slip hakuna usalama wa Taifa nchini bali kuna usalama wa Mafisadi. Taifa lenye taasisi ya kusimamia usalama wa Taifa kamwe haliwezi kuwa na madudu kiasi hiki miaka nenda miaka rudi.
 
Last edited by a moderator:
Najua kuna taarifa ambazo haziwezi kuwekwa public kupitia bunge.Lakini kwa mfano TISS wakagundu njama za uhujumu uchumi au huu ufisadi na kuzipeleka taarifa hizo bungeni kuna ubaya gani?

Kama taarifa zinapelekwa serikalini ni kwanini sasa hizi hujuma hazizuiliki?

Tatizo ni moja tu nalo ni kuumpa mtu mmoja madaraka ya karibu kila kitu!

Siamini kama kili kitu kinachofanywa na TISS kinapaswa kuwa siri hata bunge.
Kwani wewe shida yako ni TISS kupeleka hizo taarifa bungeni au taarifa kufika bungeni? Funguka Mkuu ueleweke vinginevyo yaonekana bado upo gizani
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom