Bunge laidhinisha uteuzi wa Noordin Haji kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa (NIS)

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
noodinn.jpg

Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ya Bunge imeidhinisha uteuzi wa Noordin Haji kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Usalama wa Taifa (NIS).

Haji atakula kiapo siku chache zijazo akichukua nafasi ya Philip Kameru ambaye anatarajiwa kustaafu baada ya kuwa madarakani NIS tangu Septemba 2014.

Rais William Ruto, tarehe 16 Mei, alimteua Haji kushika nafasi ya NIS. "Mheshimiwa Rais amewasilisha uteuzi huo Bungeni kwa ajili ya maamuzi ya Bunge, kwa kufuata matakwa ya kisheria yaliyowekwa chini ya Katiba na Sheria ya Usalama wa Taifa," alisema Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei.

Baada ya maamuzi ya Bunge, Haji atarejea NIS ambapo awali alihudumu kama Naibu Mkurugenzi wa Kitengo cha Kupambana na Uhalifu.

Pia soma: Noordin Haji, mteule wa Rais Ruto kwa nafasi ya Mkuu wa Usalama wa Taifa anasailiwa na Bunge mubashara
 
Back
Top Bottom