Mkurugenzi Jiji la Mwanza ashtakiwa TAMISEMI madai ya kuuza viwanja

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,119
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima 'amemshtaki' mkurugenzi wa jiji hilo, Sekiete Yahya kwa Wizara ya Tamisemi ambayo ndio mamlaka yake ya nidhamu, akimtuhumu kuhusika na uuzaji wa viwanja viwili vyenye thamani ya Sh1 bilioni.

Wakati barua ya mashtaka ikitua Tamisemi, Malima ameagiza watumishi wanne wa jiji hilo kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi kwa tuhuma za uuzaji wa viwanja hivyo.

Viwanja hivyo namba 194 na 195 vipo mtaa wa Rwegasore jijini Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza leo Ijumaa Januari 13, 2023, Malima amewataja wanaosimamishwa kazi kwa nyadhifa zao kuwa ni mhasibu wa Jiji, mwanasheria, ofisa manunuzi na ofisa mipango.

Watumishi hao wa umma wanadaiwa kuuza viwanja hivyo vilivyopo mtaa wa kibiashara katikati ya jiji kwa thamani ndogo kulinganisha na bei ya soko.

Amesema walishirikiana kuuza viwanja hivyo bila kufuata utaratibu kinyume cha taratibu na maadili ya viongozi huku mkurugenzi wa jiji akidaiwa kukiuka maagizo ya kamati ya ulinzi Wilaya ya Nyamagana na ofisi ya mkuu wa mkoa.

"Kwa mamlaka yangu nimeelekeza ofisi ya katibu tawala Mkoa wa Mwanza iwasimamishe kazi watumishi wanne ambao ni wakuu wa idara kupisha uchunguzi na tunaandika barua ofisi ya Rais (Tamisemi) kwa hatua kuhusu mkurugenzi wa Jiji," amesema Malima.

Mkuu huyo wa mkoa amesema licha ya suala la maamuzi kuachwa mikononi mwa Tamisemi, mamlaka ya mkoa unaona kuwa kiongozi huyo amekosa sifa za kuendelea kusalia mkoani humo.

Ameagiza idara ya ardhi kuangaliwa upya pamoja na watumishi hao wanne kuchunguzwa endapo wamehusika katika tukio hilo.

Maazimio ya kikao cha Ulinzi na Usalama wilaya ya Nyamagana Septemba 28, 2022 ilikataza kurejesha au kufanya uwekezaji wowote wa viwanja vitano kuanzia namba 191 hadi 196 bila kamati hiyo kufahamishwa.

MWANANCHI
 
Hawa wanaoitwa Wakurugenzi wanajua kutumia fursa.

Juzi tumesikia aliyekuwa DED wa Mtwara pia katupwa mahakamani. Leo wa mwanza?
 
Wahuni wamelivamia taifa. Wengine wanalamba asali, wengine wanalitafuna kama mchwa. Wakipata nafasi ya kubutua wanabutua hasa maana bibi PhD alishaawambia wajipimie tu.
 
Nimekutana na mlalamikaji mdada ametafuta sana kuongea na mkurugenzi ayupo manispaa husika dah haki itendeke nilimuonea HURUMA yule mdada kaachiwa eneo watu Fulani SERIKALINI wanamkwamisha dah noma kweli Hadi mtu AKAMULIWE USAA NDIO ANAJUA JIPU LIMEPONA SIO FAIR INGAWA NILIENDA KUFUATILIA MCHONGO MWINGINE ILA NILISHANGAA SANA YULE DADA ALIVYOLALAMIKa MANISPAA NAENDA KILA SIKU MKURUGENZI YUPO KWENYE VIKAO KWELI !!!!WATU WA JUU WAJITAFAKARI WAJUE KWAMBA WACHINI ANAWEZA KUKUFUKUZISHA KAZI ILA SIKU ZOTE NANI ALIKUWA JUU?!!!KWANINI ASIKILIZI WATU?!!!MWANANCHI AKISHIKA MIKE INA VIELELEZO VYOTE KITAALMU HAUKUFANYA MAJUKUMU YAKO VIZURI YA UTENDAJI WAKIKURUGENZI IM OUT
 
umeandika nini?
 
Hawa wanaoitwa Wakurugenzi wanajua kutumia fursa.

Juzi tumesikia aliyekuwa DED wa Mtwara pia katupwa mahakamani. Leo wa mwanza?
aisaaidii kwa sababu hawafungwi wanahamishwa vituo na pesa zao wanabakia nazo mtu mweusi asome asomavio kuongoza hawezi asome asomavio ujinga utamtoka lakini upumbafu ndio uwatokagi
 
Nimekutana na mlalamikaji mdada ametafuta sana kuongea na mkurugenzi ayupo manispaa husika dah haki itendeke nilimuonea HURUMA yule mdada kaachiwa eneo watu Fulani SERIKALINI wanamkwamisha dah noma kweli Hadi mtu AKAMULIWE USAA NDIO ANAJUA JIPU LIMEPONA SIO FAIR INGAWA NILIENDA KUFUATILIA MCHONGO MWINGINE ILA NILISHANGAA SANA YULE DADA ALIVYOLALAMIKa MANISPAA NAENDA KILA SIKU MKURUGENZI YUPO KWENYE VIKAO KWELI !!!!WATU WA JUU WAJITAFAKARI WAJUE KWAMBA WACHINI ANAWEZA KUKUFUKUZISHA KAZI ILA SIKU ZOTE NANI ALIKUWA JUU?!!!KWANINI ASIKILIZI WATU?!!!MWANANCHI AKISHIKA MIKE INA VIELELEZO VYOTE KITAALMU HAUKUFANYA MAJUKUMU YAKO VIZURI YA UTENDAJI WAKIKURUGENZI IM OUT
Raia wanateseka sana kutokana na ukiritimba wa vongozi kutoshikika.
 
Back
Top Bottom