Dar: Afungwa Jela maisha kwa kumlawiti Mtoto

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Mahakama ya Mwanzo Kinondoni, imemhukumu Charles Deus, kifungo cha maisha gerezani kwa kosa la kumlawiti mtoto mwenye umri wa chini ya miaka 16.

Hukumu hiyo imesomwa na na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kinondoni, Rahim Mushi, akisema mahakama imejiridhisha kuwa mshatakiwa amefanya kosa ilo.

“Kutokana na kifungu cha sheria, kifungu namba 154, kifungu kidogo 1A na 2; ni kosa kumlawiti mtoto mwenye umri nchini ya miaka 16 na ukipatikana na hatia, adhabu yake ni kifungo cha maisha bila kupunguziwa adhabu,” amesema Mushi.

Hakimu huyo amesema kuwa mshatikiwa alionyesha kuwa lengo la kuikimbia kesi hiyo, kwani mdhamini wake alipohudhuria, ilibidi asomewe mashtaka na kufugwa kifungo mpaka pale mshitakiwa atakapopatikana.

Hakimu Mushi amehoji iwapo mshitakiwa hakuwa na nia ya kuikimbia kesi hiyo, kwanini hakuaga kama anasafiri kwenda sehemu fulani ili mahakama ifahamu pale alipo, badala yake yeye aliondoka bila kutoa taarifa na hivyo haikujulikana sehemu alipo.

Hakimu huyo alimuuliza mshtakiwa kama ana lolote la kuiambia mahakama hiyo, ndipo Charles alimjibu kuwa anaomba apunguziwe adhabu kwa kuwa ana familia na wazazi wazee wanaomtegemea

Hata hivyo Hakimu Mushi amemueleza kuwa sababu alizozitoa hazijitoshelezi kupunguziwa adhabu na kama hajalidhika na hukumu anaweza kukata rufaa.

Inadaiwa mshtakiwa alikamatwa katika Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga alipokua kwenye shughuli zake.

MWANANCHI
 
Inadaiwa mshtakiwa alikamatwa katika Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga alipokua kwenye shughuli zake.
emoji419.png
emoji375.png
 
Back
Top Bottom