Mkosamali (MB) kuhamia CHADEMA

nafikiri intelijensia yake imemuambia ccm watashinda kesi ya uchaguzi kwa kutumia mahakimu wao na mwanachama wao james mbatia aliyopo nccr mageuzi...bora ahame sasa hivi..

Swala la kesi ya uchaguzi ndilo lilomwondoa G.Lema NCCR' Hii ni baada ya chama kushindwa kusimamia vizuri kesi yake,nadhani ndo kinachoelekea kutokea kwa Mkosamali!
 
Naomba niulize maswali kadhaa kwa Mkosamali.

1. Sababu gani hasa zilizomfanya ahame chadema mwanzoni?

2. Sababu gani zinazomfanya arudi chadema na wala si kwenda chama
kingine cha upinzani au hata ccm?

3. Tatizo lililopo ndani ya chama chake suluhisho pekee ni kuhama?

Awe makini, isijekuwa anafata umaarufu wa chama. Atapotea kama wengine walivyopotea.
 
Tunahitaji kuwa na katiba inayosustain vyama vingi.Hii ya sasa ni ya chama kimoja.
 
Mimi akili yangu inashindwa kuelewa mantiki kwamba uchaguzi mdogo ni gharama. Hayo ni maneno ya wana magamba kwani wanajua chaguzi ndogo zinazidi kuwapunguzia umaarufu.

Hivi Mkosamali akitoka na uchaguzi mdogo ukafanyika ndio tutapata maji? umeme wa uhakika? barabara zitajengwa? Nchi hii inahitaji kujengwa upya hivyo suala la gharama sio issue sana. Afterall kugharimia chaguzi ndogo ni bora kuliko kulipa Dowans.

CDM endeleeni kumshawishi huyo dogo atoke huko; chaguzi ndogo zina manufaa zaidi kwa CDM katika harakati za kujenga chama. CCM wanafahamu moto wa CDM hivyo hawataki kupambana tena kabls ya 2015.

Dogo kama huna amani huko na hawakujali usipoteze muda, tii dhamiri yako na utoke haraka sana.
Asante Mbalinga

Wanaosema uchaguzi ni gharama hawana sababu kubwa ya msingi zaidi ya kusema ni matumizi mabaya ya pesa za wananchi. Gharama za uchaguzi zinapandishwa na CCM wenyewe, Nec ilitoa estimate ya gharama ya Igunga kama sikosei 40mil. lakini wenyewe wakatumia more than 3bil sasa wanapolia gharama wanahoja gani.

Kila uchaguzi unaotokea una opportunities zake si ushindi tu wa ubunge kama wengi tunavyodhani kuna elimu ya uraia inatolewa vyama vinazidi kujitambulisha na kueleza sera zake, vile vile chama kinajipima kama bado kiko hai ama la nk nk. Kwa hiyo unapoongelea gharama jaribu pia kupima hasara iwapo vyama hasa vya upinzani hata chama tawala kwa miaka mitano kitakaa bila uchaguzi wowote wa nje, hata mashuleni ingawa kuna mitihani ya mwisho lakini huwa kuna mazoezi/test katikati.

Wanaosema Mkosamali asubiri hadi 2015 ndio ajitoe nafikiri hawamtakii mema kwanza kwanini wasimshauri asitoke kabisa?, mimi nafikiri huu ndio wakati mzuri kwake maana hadi uchaguzi mkuu 2015 tayari atakuwa amekijua chama tofauti na wale wanaosubiri washindwe kwenye kura za maoni(Shibuda) ndipo wakimbilie vyama vingine. Big up Mkosamali chagua chama chenye vision unachoona kinaweza kukufikisha ulipodhamilia si mradi chama.
 
mh czani sana kama kuna la msingi hapo ila kama kuchuja na kuamua mwenyewe its ok ila kama ni tamaa za kuhamia chama zitamkosti cos chadema hata kama ulikuja na yako sisi huwa letu ni moja hatuogopi mtu kwa hiyo kama atakuja lazima afuate utaratibu wa chama.
 
Hii ni Hatari kwa CCM , ninaanzakuwahurumia CCM kama uchaguzi ukitokea Mwingine basi watakuwa Bankrupt, Juzi juzi wametumia 3 billion huko Igunga. Sasa ukiitishwa uchaguzi mwengine si watafilisika au wataifilisi Nchi yetu, ingawa Wameshaifilisi lakini wataimaliza na kuifanya hata hiyo Mishahara yao wasiweze kujilipa. Hii ni Hatari kwetu sisi walipa Kodi.
 
Nitumie nafasi hii kuwaonya CDM na huyu bwana, kama wanahitaji matatizo na migogoro na pia kufirishiwa katika chaguzi zisizo za lazima basi wakubali upuuzi huo.

CCM wao wanatumia fedha za wizi wanazoiba kutoka serikali kufanyia kampeni sijui CDM wao wanazitoa wapi?
 
Huyu dogo jimbo lenyewe alishinda kibahati baada ya Magamba kumteua jambazi kuwa mgombea halafu cdm wakamweka mzee aliyechoka. Akijiuzulu na ubunge wake ausahau.
 
haina maslahi kwa mwananchi wa kawaida zaidi ya maumivu ya vurugu za uchaguzi.Tulia Muda utafika na kutimiza malengo yako.
 
halafu huyu dogo hadi muda huu kalifanyia nini taifa na jimbo lake tangu kuwa mbunge? Sikuwahi kumsikia bungeni. Nimewasikia machali na kafulila tu. Sasa hata akihamia cdm ataleta tija gani?
inaonekana bunge ulikuwa unalifuatilia kupita taarifa ya habari tu!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom