Yuko wapi mwanasiasa nguli wa CHADEMA Joseph Selasini Shao?

Yuko wapi mwanasiasa nguli wa CHADEMA Joseph Selasini Shao?

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
45,208
Reaction score
36,987
Ukimya wake una maana gani kisiasa baada ya kurejea Chadema akitokea NCCR-MAGEUZI, tofauti kabisa na makelele ya wanasiasa wengine wanao tangatanga kama vile mpayukaji Peter Msigwa, anae roporopoka tu kila uchwao angalau awatulize wasio muelewa kuhusu undumilakuwile wake kisiasa?

Ukimya wa J.Selasini una kishindo au ujumbe gani katika siasa za chadema na Tanzania kwa ujumla?

Katika vita baridi ya maneno inayoendelea baina ya viongozi wa kitaifa wa chama hicho juu ya masuala ya matumizi holela ya pesa za chama hiko, J.Selasini anaweza kua na nafasi gani kwenye hilo?

Je, hiyo inaweza kua njia rahisi zaidi ya kupita yeye na hatimae kuutwa uenyekiti wa chadema taifa?

Je, vita ya panzi ndani ya chama hicho inaweza kua furaha ya kunguru? 🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom