Mkosamali (MB) kuhamia CHADEMA

Huyu kijana alikuwa Chadema kabla ya kuhamia NCCR-Mageuzi muda mfupi baada ya Kafulila kuhamia huko, sasa inaonekana amegundua kulehakumfai ndiyo maana anataka kuhama. Anyway ana haki ya kufanya hivyo na uchaguzi mdogo ukifanyika tusiogope gharama kwa demokrasia ni gharama. Lakini pia hilo ni tatiz la kikatiba kuzuia wagombea huru

Yawezekana yale yaliyomtoa CDM hayapo tena, lakini kimkakati ni kosa kwa chama kutegemea kujijenga kwa migongo ya watu kama hawa. Kesho akiamua kwenda TLP anaondoka na chama huko kwao na kuibwaga tena CDM kama alivyofanya mwanzoni.
 
Ni sisi wananchi haohao ndio tunaoyataka kwa kukubali katiba mbovu......nchi zingine mbunge anahama chama na kubakia na ubunge wake wala haihitaji by-election
Utaratibu mzuri sana huu kwa nchi masikini kama hii yetu. tatizo ni kuwa hapa kwetu wananchi hatuelewi hasa gharama za hizi chaguzi na hii ni kwa sababu mamlaka zinazohusika na kuandaa na kuendesha shughuloi hizo hazitaki kutuambia gharama hizo. kwa kuwa wanajua kuwa na wao wana ulaji wao humo ndani, basi gharama za kuendesha chaguzi linakuwa ni jambo la siri sana.
 
Hizi chaguzi ndogo gharama zake tunalipia sisi wananchi.....sio fair kuwa kila mbunge akijiskia kuhama chama wananchi tugharimike

Badilisheni sheria, ili mbunge akihama chama abaki na ubunge wake uone jinsi CCM itakavyopukutika. Au la, mbunge anapohama, aliyekuwa wa pili kwenye uchaguzi ndiye anatangazwa mbunge, hii nayo vipi?
 
Mkosamali, "Tekana mwenewachu" pigania yanayowezeka maswala ya kuhama hama hayana mpango! Si kuna tetesi kuwa umetokea cdm wewe! Tulia kama kurudi,rudi 015 usitusumbue wananchi wako na maswala ya uchaguzi mdogo!
NI kwene..natekane, 2015 ni hofi chane. ndamenya niho tusubhiye ulalonka! tekana mwenewachu, 2015 ntiyo kulele!!!
ugomba tuvunagulane amagulu twali twashimye ngne uhaye ubhikozamwali liya shengeo dyo dodoma? hakabhaali mbatia akukuleye bhibhi, tekana, umusi wushise ugend ichadema, natwe abhashingantahe, tulokwambika impuzu tuguhezagile usubhilemeo kandi.
Ngilango ulanyumvishe mwenewachu!
Tugile umwami...umwami ni wu bhuhoro!.....
Nankane wa se bhiheko!!!!!!!
 
hana haja ya kuhama sasa.. Asubiri 2015 ili kunusuru watu wake na vurugu za kampeni zisizo na msingi

Huu ni ushauri sahihi kwa Mheshimiwa Mkosamali. Endelea kushirikiana na viongozi wa CHADEMA, hasa katika misimamo ya hawa wapambanaji wa kweli katika Bunge, na ifikapo 2015, mkubaliane nao kuwa wata kuteua mgombea wa CHADEMA katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2015. Swala la kuchukua kadi ya CDM na kuwa mwanachama ni jambo la kurasmisha tu.
 
inawezekana kule NCCR pamemshinda maana Mbatia mwenyewe haeleweki yeye kila siku anagombana na kuwekeana bifu na wanawake badala ya kuongoza chama yeye kila siku mara Halima Mdee mara Mama Nkya sasa hapo kuna kiongozi au ni boya tu ????

Chadema wana mwenyekiti wa maana?
 
Huku unakotaka kwenda ndio unakwenda kuwa mateka wa Mbowe, si muulize mbunge mwenzako David Kafulila.

Kwanza dogo ubunge wenyewe umeupata kwa bahati tu
 
Young man, it is very important to weigh pros and cons for your decission. It is important to resign and walk out as a gentleman rather than be kicked off in desgrace and coward.

If by joining CDM you will reach the height of your ambition, fulfill your mission to the society then you have no reason to hesitate, do so now. There is no point of economic losses but rather a gain as you will join the fronteirs in a battle field to save much losses.

Best wishes and hard work
 
Bora akabaki nccr mageuzi huku hata uweza uchaga wa mbowe kama vp?akapate ushauri wa kafulila alivyo ambiwa na ka slaa kwamba kafulila ni sisimizi lakini leo ni mbunge.
 
Hizi chaguzi ndogo gharama zake tunalipia sisi wananchi.....sio fair kuwa kila mbunge akijiskia kuhama chama wananchi tugharimike

Na hapa ndipo watakaopata nafasi ya kujadili katika mpya inabidi waangalie sana. By the way, mi sioni function kubwa sana ya chama katika mbunge kutekeleza majukumu yake. May be mtu afanye analysis ya kunishawishi kuwa aina ya chama alichopo mbunge, ina influence ufanisi wake kama mbunge kwa wapiga kura wake. Tunaona variations kubwa kati ya utendaji wa wabunge bila kujali vyama vyao...

Kwa maneno mengine, mbunge akiamua kuhama chama, au kuacha uanachama wa chama chake, basi isimlazimu kuacha na ubunge...
 
Mi nashauri alirudi CHADEMA asipewe nafasi ya kugombea. Hawa ndio viburi, types za akina Shibuda...
 
Nashauri Dogo asubili 2015 manake saiv kushinda akiwa Cdm sio rahisi kiasi hicho. Upepo wa kisiasa saiv haueleweki, Ccm wanakila mbinu ya kushinda uchaguzi mdogo ya kwa pesa, nguvu ya dola wizi vitisho, kuchakachua voters nk. Wafuatiliaji mnajua kilicho tokea chaguzi ndogo za Busana, mbeya vijijini kwa Nyaulawa na alipofariki Fibres Kibure wa Cdm walishinda hizi chaguzi zote kwa ubabe na dhuluma. Kwa hiyo huyu kijana kama anataka kuhama awe na subira mpaka 2015, akikurupuka anaweza kutaga, hayo ndo maoni yangu lakini kama ana uhakika wa 100% na anajua anaweza kuhama na kushinda basi go ahead vinginevyo atulize ball.
 
Daaa kila Mtu ana akili zake lkn ni vyeema Mtu ukakaaa mahala ambapo utapata aman ya Moyo wako na ukafanya kazi vile ulivojaaliwa.Ushauri atulie na kuyamaliza na Mwenyekiti wake ikishindikana kabisa basi ndio afanye Uamuzi huo

we mbona hueleweki?
 
halafu huyu dogo hadi muda huu kalifanyia nini taifa na jimbo lake tangu kuwa mbunge? Sikuwahi kumsikia bungeni. Nimewasikia machali na kafulila tu. Sasa hata akihamia cdm ataleta tija gani?
 
Hivi haiwezekani awe mwana-mageuzi akiwa pale pale ili kutuepushia gharama za kuanda uchaguzi mwingine mdogo, tume ni ile ile ya magamba ana uhakika gani hawataweza kuchakachue kiti kimagambike
 
NI kwene..natekane, 2015 ni hofi chane. ndamenya niho tusubhiye ulalonka! tekana mwenewachu, 2015 ntiyo kulele!!!
ugomba tuvunagulane amagulu twali twashimye ngne uhaye ubhikozamwali liya shengeo dyo dodoma? hakabhaali mbatia akukuleye bhibhi, tekana, umusi wushise ugend ichadema, natwe abhashingantahe, tulokwambika impuzu tuguhezagile usubhilemeo kandi.
Ngilango ulanyumvishe mwenewachu!
Tugile umwami...umwami ni wu bhuhoro!.....
Nankane wa se bhiheko!!!!!!!

Duh, ni kitu gani tena hiki ? Sasa naamini Tanzania inaelekea kubaya... Yaani mtu mzima anaamua kumwaga ki-banjamulenge hapa tena bila aibu !!
Ni kitu gani hiki kama siyo Ukabila ?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom