Mkopo wa trillion 1 kujenga uwanja wa kimataifa wa ndege Pemba na barabara kilometer 800 Zanzibar pekee, uwiano wa kibajeti upo wapi?

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,824
18,568
Maelezo ya mkopo huo mkubwa kuwahi kutokea kwa Zanzibar yapo mwisho kabisa mwa uzi huu.

Hoja yangu kubwa ni uhitaji wa kujenga kiwanja kikubwa cha kimataifa katika kisiwa cha Pemba wakati tayari upo uwanja kama huo Unguja ambapo ni kilometer 100 tu kutoka Pemba.

Pia kujenga kilometer 800 za lami katika visiwa vya Zanzibar kwa udogo wake manake hata vichochoro vitawekwa lami.

Wakati Zanzibar kwa udogo wake ambao ni kama wilaya ya Moshi vijijini wakipata kilometer 800 za barabara, upande wa bara kwa ukubwa na wingi wa watu ambao ni zaidi ya mara 50 ukilinganisha na Zanzibar, wanapata fedha kujenga kilometer 2000 tu!

Nafikiri kuna upendeleo mkubwa kibajeti kwa namna isiyoakisi uwiano wa ukubwa wa nchi na idadi ya watu (watu milioni 60 dhidi ya 1.5 million).

********************************************

Serikali ya Tanzania na Uingereza zimesaini makubaliano ya mkopo wa bei nafuu wa Euro 400 milioni sawa na Sh1.04 trilioni kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Pemba na zaidi ya kilometa 800 Unguja na Pemba.

Fedha hizo ambazo ni mkopo nafuu kutoka Uingereza, unapitia benki za Deutsche na Citibank kiasi ambacho kinatajwa kuwa kikubwa kuwahi kupokewa kwa Serikali hiyo tangu Mapinduzi.

Hafla ya kutia saini hiyo imefanyika leo Juni 20, 2023 katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Zanzibar kati ya Balozi wa Uingereza nchini Tanzania David Concar na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Akizungumza baada ya kushuhudia utiaji wa saini hiyo, Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Zena Said amesema ni tukio kubwa la kihistoria kwa Zanzibar kugharamia miundombinu muhimu ya kimkakati kwa kiasi kikubwa cha fedha za namna hiyo.

“Hii itanufaisha uchumi wetu watu kutoka maeneo mbalimbali watakuja na kukuza utalii wetu,” amesema
Waziri wa Fedha na Mipango Dk Saada Mkuya amesema kwa mara ya kwanza Zanzibar kupata kiasi hicho kikubwa cha fedha za mkopo kwa mkupuo.

“Hii ni historia tunakwenda kuifungua Zanzibar katika miundombinu ya kuchumi kwa kujenga barabara za hapa Unguja na Uwanja wa ndege wa Pemba ambao utakuwa wa kimataifa,” alisema Dk Saada.

Naye Waziri wa Ujenzi, Mawasilianio na Uchukuzi, Dk Khalid Salum alisema safari hiyo imeanza muda mrefu tangu awamu zilizotangulia na mawaziri tofauti wa Awamu ya Nane hivyo kufikia hatua hiyo ni jambo la kupongeza.

“Zaidi ya kilomita 800 zinakwenda kujengwa hapa Unguja na Pemba hii haijawahi kutokea mara nyingi zinajengwa barabara zenye urefu wa kilometa 200, lakini mara hii tunajenga kilometa hizo tena kwa wakati mmoja,” alisema Dk Khalid.

Naye Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, David Concar alisema katika utekeleji wa mradi huo utafungua fursa za kiuchumi na kijamii kwa taifa na wananchi wa Zanzibar.

Alisema Serikali ya Uingereza itaendelea kushirikiana na Serikali za Tanzania na Zanzibar kuendelea kuitekeleza miradi mingine mikubwa ya kimkakati.
 
Maelezo ya mkopo huo mkubwa kuwahi kutokea kwa Zanzibar yapo mwisho kabisa mwa uzi huu.

Hoja yangu kubwa ni uhitaji wa kujenga kiwanja kikubwa cha kimataifa katika kisiwa cha Pemba wakati tayari upo uwanja kama huo Unguja ambapo ni kilometer 100 tu kutoka Pemba.

Pia kujenga kilometer 800 za lami katika visiwa vya Zanzibar kwa udogo wake manake hata vichochoro vitawekwa lami.

Wakati Zanzibar kwa udogo wake ambao ni kama wilaya ya Moshi vijijini wakipata kilometer 800 za barabara, upande wa bara kwa ukubwa na wingi wa watu ambao ni zaidi ya mara 50 ukilinganisha na Zanzibar, wanapata fedha kujenga kilometer 2000 tu!

Nafikiri kuna upendeleo mkubwa kibajeti kwa namna isiyoakisi uwiano wa ukubwa wa nchi na idadi ya watu (watu milioni 60 dhidi ya 1.5 million).

*************************************

Serikali ya Tanzania na Uingereza zimesaini makubaliano ya mkopo wa bei nafuu wa Euro 400 milioni sawa na Sh1.04 trilioni kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Pemba na zaidi ya kilometa 103 Unguja na Pemba.

Fedha hizo ambazo ni mkopo nafuu kutoka Uingereza, unapitia benki za Deutsche na Citibank kiasi ambacho kinatajwa kuwa kikubwa kuwahi kupokewa kwa Serikali hiyo tangu Mapinduzi.

Hafla ya kutia saini hiyo imefanyika leo Juni 20, 2023 katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Zanzibar kati ya Balozi wa Uingereza nchini Tanzania David Concar na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Akizungumza baada ya kushuhudia utiaji wa saini hiyo, Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Zena Said amesema ni tukio kubwa la kihistoria kwa Zanzibar kugharamia miundombinu muhimu ya kimkakati kwa kiasi kikubwa cha fedha za namna hiyo.

“Hii itanufaisha uchumi wetu watu kutoka maeneo mbalimbali watakuja na kukuza utalii wetu,” amesema
Waziri wa Fedha na Mipango Dk Saada Mkuya amesema kwa mara ya kwanza Zanzibar kupata kiasi hicho kikubwa cha fedha za mkopo kwa mkupuo.

“Hii ni historia tunakwenda kuifungua Zanzibar katika miundombinu ya kuchumi kwa kujenga barabara za hapa Unguja na Uwanja wa ndege wa Pemba ambao utakuwa wa kimataifa,” alisema Dk Saada.

Naye Waziri wa Ujenzi, Mawasilianio na Uchukuzi, Dk Khalid Salum alisema safari hiyo imeanza muda mrefu tangu awamu zilizotangulia na mawaziri tofauti wa Awamu ya Nane hivyo kufikia hatua hiyo ni jambo la kupongeza.

“Zaidi ya kilomita 800 zinakwenda kujengwa hapa Unguja na Pemba hii haijawahi kutokea mara nyingi zinajengwa barabara zenye urefu wa kilometa 200, lakini mara hii tunajenga kilometa hizo tena kwa wakati mmoja,” alisema Dk Khalid.

Naye Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, David Concar alisema katika utekeleji wa mradi huo utafungua fursa za kiuchumi na kijamii kwa taifa na wananchi wa Zanzibar.

Alisema Serikali ya Uingereza itaendelea kushirikiana na Serikali za Tanzania na Zanzibar kuendelea kuitekeleza miradi mingine mikubwa ya kimkakati.
Seen
 
Back
Top Bottom