Mkopo Tafadhali: upate riba 15%

Mkopo Tafadhali: upate riba 15%

GreenCity

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2012
Posts
5,905
Reaction score
4,664
Habari wana JF.
Mimi ni kijana ninayeanza ujasiliamali, na hivi karibuni nimeanzisha biashara ya M-pesa na nafaka hapa Iringa. Napata wateja wengi sana kuliko uwezo wa mtaji wangu, nahitaji kujitanua zaidi. Hivyo naomba ushauri wa jinsi ya kupata Mkopo (toka kwa mtu binafsi au taasisi) wa haraka kuanzia laki mbili (200,000) kwa riba isiyozidi 15% kwa mwezi. Nina dhamana inayohamishika kama friji, computer, radio (disc changer), TV, n.K (kwa Iringa)
pia nina eneo/nyumba (Mbeya).
 
Mkuu umekosa saccos ya kukupa mkopo? 15% kwa mwezi ni kubwa sana....
15% kwa mwezi. Kwa mwaka ni 180%. Ukikopa 1,000,000/- kama mkopo ni wa mwaka mmoja unatakiwa urudishe shilingi 2,800,000/- which is very very expensive.
 
nenda pride utapata kwa masharti nafuu bila dhamana.
 
"Unaweza kukopa fedha kwa ajili ya maskini yeyote kati yenu, kati ya watu wangu, hivyo ni lazima si kitendo dhidi yake kama walaji riba. Wala kuongeza juu yake faida yoyote" (Biblia, Kutoka 22:25)

"Usichukue faida yoyote ya ndugu yako, ama ya pesa au chakula au kitu kingine chochote ikawa umechukua riba" (Biblia, Kumbukumbu la Torati 23:19)

"Na kama mnawakopesha wale tu mnaotumaini watawalipeni, je, mtapata tuzo gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi wenzao ili warudishiwe kima kilekile!". Biblia (Luka 06:34)

"... faida na kuchukua riba - Je, ndo ataishi? Hapana, lazima wafe, lakini kwa sababu yeye kashiriki katika maovu hayo, atakuwa katika adhabu na kifo. damu yake atakuja juu yake ". (Biblia Ezekieli 18:13)

Waislamu huchinja na kutoa Swadaqah ya kondoo mwanamke akijifungua. Hii pia imetajwa katika Biblia.

"Na siku yake ya kujisafisha ikifika, ikiwa ni mvulana au binti, atachinja kondoo mwenye umri kwa sadaka ya kuteketezwa ... (Mambo ya Walawi 00:06 Biblia)
 
Mkuu umekosa saccos ya kukupa mkopo? 15% kwa mwezi ni kubwa sana....

mkuu saccos nyingi nimeambiwa natakiwa niwe mwanachama kwanza! By the way naitaji si zaidi ya laki 5 na nitaitumia si zaidi ya miezi 3. Lengo ni kuwahi kununua mzigo kabla ya kuisha OCTOBER.
 
15% kwa mwezi. Kwa mwaka ni 180%. Ukikopa 1,000,000/- kama mkopo ni wa mwaka mmoja unatakiwa urudishe shilingi 2,800,000/- which is very very expensive.

mkuu saccos nyingi nimeambiwa natakiwa niwe mwanachama kwanza! By the way naitaji si zaidi ya laki 5 na nitaitumia si zaidi ya miezi 3. Lengo ni kuwahi kununua mzigo kabla ya kuisha OCTOBER.
 
“Unaweza kukopa fedha kwa ajili ya maskini yeyote kati yenu, kati ya watu wangu, hivyo ni lazima si kitendo dhidi yake kama walaji riba. Wala kuongeza juu yake faida yoyote” (Biblia, Kutoka 22:25)

“Usichukue faida yoyote ya ndugu yako, ama ya pesa au chakula au kitu kingine chochote ikawa umechukua riba” (Biblia, Kumbukumbu la Torati 23:19)

“Na kama mnawakopesha wale tu mnaotumaini watawalipeni, je, mtapata tuzo gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi wenzao ili warudishiwe kima kilekile!”. Biblia (Luka 06:34)

“... faida na kuchukua riba - Je, ndo ataishi? Hapana, lazima wafe, lakini kwa sababu yeye kashiriki katika maovu hayo, atakuwa katika adhabu na kifo. damu yake atakuja juu yake “. (Biblia Ezekieli 18:13)

Waislamu huchinja na kutoa Swadaqah ya kondoo mwanamke akijifungua. Hii pia imetajwa katika Biblia.

“Na siku yake ya kujisafisha ikifika, ikiwa ni mvulana au binti, atachinja kondoo mwenye umri kwa sadaka ya kuteketezwa ... (Mambo ya Walawi 00:06 Biblia)

nawe Zomba nakushukuru pia! Ila hapa ni biashara zaidi mkuu, naogopa sana kutafsiri biblia ila kabla ya kufanya hili nilimwomba Mwenyezi Mungu aniongoze pia!
 
Huna haja ya kutafsiri, ni Kiswahili hicho.
"... faida na kuchukua riba - Je, ndo ataishi? Hapana, lazima wafe, lakini kwa sababu yeye kashiriki katika maovu hayo, atakuwa katika adhabu na kifo. damu yake atakuja juu yake ". (Biblia Ezekieli 18:13)
 
"Unaweza kukopa fedha kwa ajili ya maskini yeyote kati yenu, kati ya watu wangu, hivyo ni lazima si kitendo dhidi yake kama walaji riba. Wala kuongeza juu yake faida yoyote" (Biblia, Kutoka 22:25)

"Usichukue faida yoyote ya ndugu yako, ama ya pesa au chakula au kitu kingine chochote ikawa umechukua riba" (Biblia, Kumbukumbu la Torati 23:19)

"Na kama mnawakopesha wale tu mnaotumaini watawalipeni, je, mtapata tuzo gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi wenzao ili warudishiwe kima kilekile!". Biblia (Luka 06:34)

"... faida na kuchukua riba - Je, ndo ataishi? Hapana, lazima wafe, lakini kwa sababu yeye kashiriki katika maovu hayo, atakuwa katika adhabu na kifo. damu yake atakuja juu yake ". (Biblia Ezekieli 18:13)

Waislamu huchinja na kutoa Swadaqah ya kondoo mwanamke akijifungua. Hii pia imetajwa katika Biblia.

"Na siku yake ya kujisafisha ikifika, ikiwa ni mvulana au binti, atachinja kondoo mwenye umri kwa sadaka ya kuteketezwa ... (Mambo ya Walawi 00:06 Biblia)

Mkuu, saidia huyu kijana...kopesha yeye bure tafadhali!
 
Ndugu GreenCity,

Nakushauri uende FINCA. Hawa nao ni wazuri na wameenea karibia kila wilaya. Riba yao kwa mwenzi ni karibia 3%.

Kwa hiyo laki 5 unayotaka, utalipa 15000 ambayo ni sawa na 75000 kwa miezi 3. Ila kwa kuwa unafanya marejesho kwa week, riba itapungua na unaweza kulipa kama 45000-50000!Nakutakia kila la heri,
 
Last edited by a moderator:
That means Capital+Interest(75,000/=) unarudisha kwa miezi mingapi?

exactly! Nahitaji nitumie kwa miezi 2. Na ukitaka nikupe riba yako kila mwezi its OK, AU ukitaka nikupe the sum of it (total cost plus interest) at the end of the miezi 2, still its OK!
Deal?
 
Ndugu GreenCity,

Nakushauri uende FINCA. Hawa nao ni wazuri na wameenea karibia kila wilaya. Riba yao kwa mwenzi ni karibia 3%.

Kwa hiyo laki 5 unayotaka, utalipa 15000 ambayo ni sawa na 75000 kwa miezi 3. Ila kwa kuwa unafanya marejesho kwa week, riba itapungua na unaweza kulipa kama 45000-50000!Nakutakia kila la heri,

bila shaka unazungumzia ule wa vikundi kaka! Sasa wanataka msipungue watu 5, na kama ni binafsi wanaitaji TIN na Leseni ya angalau mwaka 1 nyuma na dhamana ya biashara yako, N.K
au wametofautiana mkoa na mkoa?
 
Last edited by a moderator:
bila shaka unazungumzia ule wa vikundi kaka! Sasa wanataka msipungue watu 5, na kama ni binafsi wanaitaji TIN na Leseni ya angalau mwaka 1 nyuma na dhamana ya biashara yako, N.K
au wametofautiana mkoa na mkoa?

Sina details zaidi kuhusu masharti yao kwa undani. Ila ukihitaji naweza kuwauliza jama wanaofanyakazi na FINCA.

Hata hivyo, ni muhimu ujipange ili uweze kukidhi vigezo vyao.

Kwa mfano, hitaji la TIN na leseni ya biashara ni muhimu ili wajiridhishe kwamba wanampa mkopo mfanyabiashara. Kama hauko level hiyo basi tafuta wenzio muunde kikundi. Vinginevyo, kila taasisi wana masharti yao na unatakiwa uyatimize kama kweli unataka kukopa pesa zao!!
 
exactly! Nahitaji nitumie kwa miezi 2. Na ukitaka nikupe riba yako kila mwezi its OK, AU ukitaka nikupe the sum of it (total cost plus interest) at the end of the miezi 2, still its OK!
Deal?

Ok mie nipo dsm mbezi huku collateral itakua nini sasa maana ninaweza kukutumia kwa M-PESA,ebu fanya mchakato wa collateral
 
Back
Top Bottom