Mulhat Mpunga
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 27,650
- 16,731
Wanabodi,
Kwanza naomba nisieleweke kuwa sina nia mbaya na hayo Makanisa, bali naomba kujua nini hasa chanzo cha mkoa wa Mbeya kuwa na Makanisa mengi ya waumini wa madhehebu ya dini. Pia hata waimbaji wengi wa nyimbo za Injili wanatoka mkoani Mbeya, hivi nini chanzo?
Elimu haina mwisho..
wewe uliwahi kumuuliza mungu swali gani ?..... na alikujibu nini ?
Sababu kuu ya wingi wa madhehebu kwa mkoa wa mbeya ni kukosekana ama udhaifu wa madhehebu makubwa ya kikristo yaani Roman Catholic, Lutherani na Anglican. Haya madhehebu yalichelewa sana kufika mbeya na kukuta wenzao wa Moravian wameshatawala eneo kubwa sana la huko mbeya. Kanisa la Moravian linashabihiana sana na makanisa ya kilokole yaani kipentekoste. Makanisa ya kipentekoste hujulikana kwa wachungaji wao. Hivyo wengi walioshika dini sana mbeya walijikuta wanaanzisha makanisa yao mahali wanapokua. Hali kama hii haipo kwa mikoa ambayo ni ngome ya makanisa makubwa mfano. mwanza - RC, Songea - RC, Sumbawanga - RC, Arusha - Lutheran, Dodoma - Anglican, Bukoba - RC.
Pia wanyakyusa wana vipaji sana hasa uimbaji. Kama unyakyusani ingekua ngome ya RC tusingewasikia sana wakitoa nyimbo au kuwa wachungaji kila sehemu wanapokua. Madhehebu hayo mengine (ya kilokole) yanathamini sana nyimbo na ni sehemu kubwa sana ya ibada zao, ndio maana vipaji hivyo hukua kirahisi kwa mkoa wa mbeya.
Mungu alie hai anajibu unachouliza, yaani Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo.
Kujua swali gani niliuliza ni private issue..
Mungu wa yesu tena, wakati yesu mwenyewe mnamwita mungu. Hapa ndipo mnapojichanganya.
ni mpango wa Mungu mbeya kuwa na makanisa mengi.kwa africa ni jiji la pili ukiachia mbali lagos.Muugu ana mipango mingi sana na huuu mkoa.mfano kumleta sugu kuwa mbunge,wananchi wake kujitambua na kuikubali CDM.SIO HIVYO WATU WAKE WENGI WANAONEWA SANA.kIBANDA tindikali,Mwangosi aliuwawa,Mwakyembe sumu,ulimboka kucha.vilevile ni mkoa uliye na mbunge kilaza kuliko wote bwana mlugo,alidiriki kusema tanzania na muungano wa tanganyika na zimbabwe.Mipango yake mola haina makosa .home mbeya home
Ukiona hivyo ujue Mafundisho ya Kulipa visasi, kujitoa Muhanga, kuGARISA watu. Yoote haya hayana nafasi huko Mbeya
Karibu sana hapa city pub mzee
Mji ulio na Makanisa mengi umebarikiwa. Mbeya imebarikiwa!!!! Ulitaka Mbeya uwe mji wenye BAR nyingi zaidi kuliko Makanisa na misikiti, kama ilivyo miji mingine????
Unaijua idadi ya waumini ya makanisani hayo?
La msingi wote wakristo tu. Haijalishi madhehebu maana biblia ndio hiyo hiyo.
Je unaweza kutofautisha msikiti wa Shia na Sunni? Au wote kikubwa ni Waislamu tu?
Mimi na wewe tuna roho tofauti ( Roho ikaayo ndani yangu ni tofauti na roho iliyomo ndani yako ).
Wanabodi,
Kwanza naomba nisieleweke kuwa sina nia mbaya na hayo Makanisa, bali naomba kujua nini hasa chanzo cha mkoa wa Mbeya kuwa na Makanisa mengi ya waumini wa madhehebu ya dini. Pia hata waimbaji wengi wa nyimbo za Injili wanatoka mkoani Mbeya, hivi nini chanzo?
Elimu haina mwisho..