Mkoa wa Mbeya ndio nchi ya ahadi?

M-bongotz

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,734
405
Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi sana juu ya mkoa wa Mbeya.,nimebahatika kutembea zaidi 75% ya mikoa ya Tanzania lakini ni mkoa wa Mbeya tu ndipo nilipokuta wingi wa makanisa ya watu binafsi pamoja na "maaskofu na manabii" waliojipachika status hizo wenyewe.

"Maaskofu na manabii" wengi tunaowasikia leo hii hapa Tanzania ni watu wenye asili ya mkoa wa Mbeya, kwa uchache tu hebu angalia hawa wafuatao;

Nabii Lusekelo "mzee wa upako"
Mchungaji Mwakasege
Mchungaji Bukuku
Askofu Mwasota
Na hivi karibuni ameibuka "babu" Mwasapile.,list ni ndefu sana...

Ninachojiuliza ni kwamba wingi wa makanisa haya unamaanisha kuwa mkoa huu ndio wenye wacha Mungu sana au ndio ile nchi ya ahadi tunayoisikia tu na pengine Masia akirudi anaweza kufikia Mbeya.
 
hahahahahaha,,,, dah, una fact za ukweli sana ndugu yangu,,,, hii stori kwa upande mwingine inafurahisha sana, na inaonekana kweli hilo suala umelifanyia research.. Big up
 
Na mambo yaajabu na kitatili pia yapo yaliyoanzia Mbeya e.g Kuchuna ngozi....
 
Wanabodi,

Kwanza naomba nieleweke kuwa sina nia mbaya na hayo Makanisa, bali naomba kujua nini hasa chanzo cha mkoa wa Mbeya kuwa na Makanisa mengi ya waumini wa madhehebu ya dini. Pia hata waimbaji wengi wa nyimbo za Injili wanatoka mkoani Mbeya, hivi nini chanzo?

Elimu haina mwisho..
 
Mji ulio na Makanisa mengi umebarikiwa. Mbeya imebarikiwa!!!! Ulitaka Mbeya uwe mji wenye BAR nyingi zaidi kuliko Makanisa na misikiti, kama ilivyo miji mingine????
 
Mji ulio na Makanisa mengi umebarikiwa. Mbeya imebarikiwa!!!! Ulitaka Mbeya uwe mji wenye BAR nyingi zaidi kuliko Makanisa na misikiti, kama ilivyo miji mingine????

Mkuu sukuwa na nia mbaya kabisa kwani mbeya ndio nyumbani,nilitaka kujua sababu
 
Mji ulio na Makanisa mengi umebarikiwa. Mbeya imebarikiwa!!!! Ulitaka Mbeya uwe mji wenye BAR nyingi zaidi kuliko Makanisa na misikiti, kama ilivyo miji mingine????

kuna wachuna ngozi na wapiga nondo, nao wana upako ?
 
Basi kama hiyo ndio sababu nashukuru sana kwa mkoa wetu kubarikiwa kwa hilo hivyo najivuna sana
 
Back
Top Bottom