Ethical Ninja CEH
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 3,695
- 5,032
Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
Ok,ni wakarimu sana karibu wapo wamejaa tele
Mbeya is the best aisee. Watu hawajapashtukia tu.
Makanisa mengi na maovu mengi,hii sijaielewa vyema huko mbeya.
Utitiri wa makanisa kwa uchunguzi wako;Lakini umeshawahi kusikia mtu analazimishwa kuingia kwenye hayo makanisa?Au unasema tu kujifurahisha
Wakuu,wana jf karibuni mbeya
karibu Chunya mkuu
Chunya ipi mkuu,ya makongolosi au ya mkwajuni ktk hospitali ya mwambani? Mkuu kote huko nimefika,nashukuru sana kiongozi
Tatizo lenu ndio hilo, badala ya kusoma upande wa pili wa shilingi nyinyi mmeng'ang'ania na agano tu. Mimi ndio nakwambia kwenye uislam hakuna dhehebu linaloitwa shia.
Kwasababu Mbeya ni lango!!
hiyo ndiyo sababu kubwa. wakoloni wa kijerumani waligawa maeneo kwa wamishionari ili wasijekugombana. mbeya walipewa moravian wakati iringa na sumbawanga walipeewa RC. sasa moravia hawabrainwash sana waumini wao hivyo wengi kuwa open minded. mi nililelewa moravian ila sasa nina kanisa langu.Sababu kuu ya wingi wa madhehebu kwa mkoa wa mbeya ni kukosekana ama udhaifu wa madhehebu makubwa ya kikristo yaani Roman Catholic, Lutherani na Anglican. Haya madhehebu yalichelewa sana kufika mbeya na kukuta wenzao wa Moravian wameshatawala eneo kubwa sana la huko mbeya. Kanisa la Moravian linashabihiana sana na makanisa ya kilokole yaani kipentekoste. Makanisa ya kipentekoste hujulikana kwa wachungaji wao. Hivyo wengi walioshika dini sana mbeya walijikuta wanaanzisha makanisa yao mahali wanapokua. Hali kama hii haipo kwa mikoa ambayo ni ngome ya makanisa makubwa mfano. mwanza - RC, Songea - RC, Sumbawanga - RC, Arusha - Lutheran, Dodoma - Anglican, Bukoba - RC.
Pia wanyakyusa wana vipaji sana hasa uimbaji. Kama unyakyusani ingekua ngome ya RC tusingewasikia sana wakitoa nyimbo au kuwa wachungaji kila sehemu wanapokua. Madhehebu hayo mengine (ya kilokole) yanathamini sana nyimbo na ni sehemu kubwa sana ya ibada zao, ndio maana vipaji hivyo hukua kirahisi kwa mkoa wa mbeya.
Ni sawa na kuuliza hivi; Tanzania ina Makabila takribani 125 lakini zaidi ya 50 Asilimia ya makabila hayo yanapatikana mkoa wa Mara, je MARA NDIKO KULIJENGWA MNARA WA BABERI?