Mkoa wa Geita umeanza maandalizi ya kujenga uwanja wa kisasa wa mpira

Smkwawa

JF-Expert Member
Feb 18, 2014
651
964
Mkoa wa Geita umeanza maandalizi ya ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu utakaokuwa na uwezo wa kuingiza mashabiki zaidi ya elfu themanini kwa wakati mmoja ili kuondoa changamoto za viwanja kwa mikoa ya kanda ya ziwa.


Serikali imetangaza kujenga uwanja mkubwa wa mpira wilayani Chato, mkoani Geita ili kukuza sekta ya michezo nchini na kuvutia watalii na wawekezaji. Uwanja huo unatarajiwa kuwa wa pili kwa ukubwa baada ya wa Benjamin Mkapa ulipo jijini Dar, lakini huu wa Chato utakuwa wa kisasa zaidi.

Waziri wa Nishati Medard Kalemani amesema hayo wakati akihutubia sherehe za uzinduzi wa Hifadhi ya taifa ya Burigi-Chato na kueleza kwamba uwanja huo utaitwa Chato Stadium na ujenzi wake unatarajiwa kuanza hivi karibuni.!
 
Chato nayo ni Tanzania,Sasa mlitaka uwanja ukajengwe Bunyenzi?
 
Back
Top Bottom