Mkuu, kwani alikuwa anaifanyia kazi ishu yoyote tata au inayowahusu vigogo?..kwanini upate shaka?
Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi!
Habari zilizopatikana hivi punde ni kuwa Mkemia Ernest Mashimba, PhD amefariki ghafla huko Tanga alikokuwa amealikwa kama mgeni rasmi kwenye mahafari ya darasa la saba.
Mauti yamemkuta hotelini alikokuwa amefikia baada ya kuanguka ghafla, habari ni kuwa kifo chake kimegundulika baada ya dereva wake kumpitia leo asubuhi kwa ajili ya kuanza safari ya kurejea DAR.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa . . . . . . .
Mkuu kuna matukio tata mengi yametokea hivi karibuni, na ukichukulia afya ya mkulu ipo majaribuni. naamini mkemia anaweza akawa mtu muhimu ktk kipindi cha lala salama.
Hivi ile ripoti ya wananchi walidhurika na zile kemikali kutoka machimbo ya dhahabu ya barik yalipaswa kuwa na second testing au?
Doubtful, lakini ametutoka. nadhani postmortem ya kifo chake ifanyike kwa undani zaidi
RIP Ernest Mashimba.
Wafuatiliaji wa mambo, mimi nakumbuka kama Chief Chemist kabla yake au yule wa nyuma zaidi naye alikufa ghafla, na alikuwa anafuatilia issue ya mchele mbovu uliokuwa bandarini? Nina shaka sana na hivi vifo!