Mke wangu

Tabia ni kigezo muhimu sana kuliko vinginevyo.Kumbuka kuwa kunguru hafugiki au maji hayasahau kale yake. Good day!!!
 
No! Usilipize kisasi, utakuwa unaongeza ugonjwa juu ya ugonjwa. Akupe kwanza sababu za kuamua kucheat, yawezekana ana sababu za msingi.. Pole sana..

hizo sababu za msingi za kucheat ni zip?......hamna kitu hapo
 
kama anawapata kwanye internet chatting,inaonyesha yupo addicted na internet,alivyonogewa na mmoja,ameona bora aendeleze na wengine.amua maamuzi sahihi,anaweza akaacha kwa kuwa amekubali makosa na anaweza asiache.ndoa siku hizi ni kama maigizo tu.kwa upande wangu mtu akini cheat jamani ni good bye for good,mara moja nitasema bahati mbaya,ila zaidi ya mara moja si bahati mbaya tena
 
Kaka pole sana kama utapata nafasi tembelea pale afrika sana huwa tunakutana pale na kupeana mbinu za kuwaweka sawa hawa viumbe ni kazi ndogo sana hiyo hata mwezi hauishi atakuwa anakuheshimu kupita kiasi.
 
Jamani wa jamii, naombeni ushauri wa bure

Mke wangu kanicheat kwa wanaume mbalimbali, nilipomwuliza mara ya kwanza ilkataa na kutaka kuapa through bible, baadaye baada ya kumbana na kuleta vithibiti kakubali kuwa kweli alikuwa ananicheat nifanyaje? je na mie nilipize kisasi?

Wapendwa, hana hata sababu, kitandani mwenyewe anaridhika na kunipa BIG UP, kimato sio kibaya, tunakaa wkenye nyumba yetu, tuna watoto, tuna kigari cha kutembelea,nimemwuliza sababu ni nini anasema shetani kampitia, hao wanaume anaonicheat nao hawana lolote, yeye ndo anachukua pesa zangu na kwenda kulipia hotel. Wanaume wotw hao kawapata through internet charting, nifanyaje mwenzenu
Mkuu pole sana kwa ukatili uliofanyiwa...! Lakini kwa maelezo yako ya pili, nahisi kama vile hata wewe ulipatikana kwa njia hiyo ya kugharamiwa....! Na kama ndivyo ilivyo, basi nikijua kabisa kuwa ukweli unauma, niseme tu kuwa huo ni hulka yake ....!

Ushauri wa jumla:
Uwelewe tu kwamba, hakuna ndoa iliyowahi kuvuka miaka 5 bila kusalitiwa, na hata hivyo waliosalitiwa wanapata kujua aidha, mapema au baada ya muda, lakini hii huwa ni siri ya wahusika wengi....! Na mengine hubaki bila kujulikana daima...! Si lazima wote wasaliti, lakini mmoja huwa lazima atakuwa amefanya hivyo....! Karibu kila mtu mzima ana donda kubwa sana katika ndoa yake...! Hapa tatizo sio kuibiwa, bali ni wewe kujua kuwa unaibiwa....!

Maamuzi yanayowezekana kwako:
  1. Hata kama mliapa kuvumiliana, kupendana, na kutunzana katika shida na raha, magonjwa na afya; na kamwe hamtatengana hadi kifo kiwatenganishe....! na imeandikwa kwenye misaafu kuwa "samehe sabini mara sabini", "muosha huoshwa", na "msihukumu"...! Lakini misaafu hiyo pia husema; "amwachaye mkewe kwa kosa lolote, isipokuwa la usinzi, na akaishi na mwanamke mwingine, naye atakuwa amezini"....! So, binafsi una nafasi ya kusamehe, na nafasi ya kuamua vinginevyo.....!
  2. Lakini iwapo utaamua kumsamehe na kuishi naye, basi jipange vema katika saikolojia; na umfanye aamini na aone kuwa alichokifanya ni aibu yake mwenyewe kwa kuvua vyupi, na kuwafunulia watu wengine uchi wake....! Kamwe, mbele ya mwenye akili timamu, aibu sio ya msalitiwa, bali ni ya msaliti tu....! Anayechokonolewa ni yeye, na wala sio wewe....! Mfano; mletee story ya kukandiwa na watu mitaani kwa harufu, umajimaji, nk yake....! Ni hapo ataona kuwa anapofanya hivyo, anajiharibu mwenyewe, na kamwe huo mzigo hasaidiwi na mtu yeyote...! Ni hapo ataona kuwa kila anayemtamkia hayo mambo, huwa anataka tu kujithibitishia na alichosikia mtaani na si vinginevyo...! Kama kweli huwa anafanya hivyo consciously, basi ataacha, maana ataona kumbe anachoreka tu....!
  3. Kama umeamua vinginevyo, basi uangalie mambo kadhaa kama vile watoto, na utayari wako kisaikolojia, na kibayolojia....! Kama hana mtoto nawe basi na arudi kwao salama salimin....! Kama ana mtoto nawe, basi muoe mwanamke mwingine, baki kumtunza mtoto wako, lakini kwa kipindi cha transition, adhihirishe kuwa you can sleep with her without having sex in the rest of your life....! Mpe kila kitu, isipokuwa hicho tu....! Let your baby/babies know what happened, and why....! Hapo atabaki na legacy ya kumridhisha wanawe kuwa kufanya hivyo sio tija katika maisha....!
Lakini kwa vyovyote vile, utakavyoamua, jaribu kuwa na "Peace of Mind"...! Otherwise, all the best...!
 
je na mie nilipize kisasi?

kisasi ni cha Muumba..............msamehe na furahia ndoa yako.........si ulisema hadi kifo kiwatenganishe sasa hizi purukshani za nini?
 
Kaa nae chini umuulize ni nini kilimfanya afanye vile, kama yuk tayari kubadilika msamehe muendelee na maisha
 
Wapendwa, hana hata sababu, kitandani mwenyewe anaridhika na kunipa BIG UP, kimato sio kibaya, tunakaa wkenye nyumba yetu, tuna watoto, tuna kigari cha kutembelea,nimemwuliza sababu ni nini anasema shetani kampitia, hao wanaume anaonicheat nao hawana lolote, yeye ndo anachukua pesa zangu na kwenda kulipia hotel. Wanaume wotw hao kawapata through internet charting, nifanyaje mwenzenu
Haya ma internet haya jamani, wanawake tuwe wagumu jamani sio kila akutongozae ndio lazima muonane,au umkubalie looo wengine ndio wamefanya vijiwe vya kutongozana , inasikitisha sana, tatizo ni ulimbukeni tu
 
Msamehe tu kaka, kaa nae chini uzungumze nae kwa kituo akueleze nn kilipelekea kukucheat, kisha fanyia kazi hayo mapungufu.. Kila la kheri.. ndoa ni kuvumiliana!
<br />
<br />
Akikuletea ngoma! Nadhani mtaimba,mtaipiga kisha mtaichezaeee!!!
 
naaka kujua vidhibiti gani ulimuonyesha ndio akakubali..........tuanzie hapo kwanza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom