Mke wangu

Nyamiobo

Member
Aug 3, 2011
10
1
Jamani wa jamii, naombeni ushauri wa bure

Mke wangu kanicheat kwa wanaume mbalimbali, nilipomwuliza mara ya kwanza ilkataa na kutaka kuapa through bible, baadaye baada ya kumbana na kuleta vithibiti kakubali kuwa kweli alikuwa ananicheat nifanyaje? je na mie nilipize kisasi?
 
No! Usilipize kisasi, utakuwa unaongeza ugonjwa juu ya ugonjwa. Akupe kwanza sababu za kuamua kucheat, yawezekana ana sababu za msingi.. Pole sana..
 
pole.
muulize sababu zinazomfanya alale na wanaume wengne...labda ueanda ukawa chanzo uenda ikawa ni umalaya wake tu na kutokutosheka

wahusishe wazazi/viongozi wa dini katika kumkanya

pole ndg yangu
 
uliapa katika shida na raha, magonjwa na afya, utamchulia poa na madhaifu yake. Kama ameomba msamaha na kukiri kosa Msamehe... kama hajaomba msamaha we muache aendelee na uchechengu wake: ila kamwe msiachane
 
Msamehe tu kaka, kaa nae chini uzungumze nae kwa kituo akueleze nn kilipelekea kukucheat, kisha fanyia kazi hayo mapungufu.. Kila la kheri.. ndoa ni kuvumiliana!
 
Kulipa kisasi haisaidii, tena unaweza kuongeza maumivu. Tatizo sio mkeo kumegwa, bali tatizo ni wewe kujua. Tafuta kwanza sababu ya yeye kwenda nje ya ndo; je hummalizi hamu, anatafuta pesa, upendeleo kazini au privilledge yeyote, au anampenda tu huyo aliyecheat naye. Kama anafuata pesa mpige chini kama unaweza. Kama humridhishi, jitahidi uone kama unaweza jirekebisha, na kama kuna mtu anampenda zaidi yako, nayo inabidi ama umpige chini au ukubali tu kumegewa...
 
No! Usilipize kisasi, utakuwa unaongeza ugonjwa juu ya ugonjwa. Akupe kwanza sababu za kuamua kucheat, yawezekana ana sababu za msingi.. Pole sana..

Sweetlady... Ivi huwa kuna sababbu za msingi zinazomfanya mtu acheat? Ni kama zipi labda?
 
Msamehe tu kaka, kaa nae chini uzungumze nae kwa kituo akueleze nn kilipelekea kukucheat, kisha fanyia kazi hayo mapungufu.. Kila la kheri.. ndoa ni kuvumiliana!

Kwa vyovyote akikaa nae chini, jibu litakuwa 'ni shetani tu alinipitia'. Nadhani jamaa afanye uchunguzi binafsi kujua sababu...
 
Sweetlady... Ivi huwa kuna sababbu za msingi zinazomfanya mtu acheat? Ni kama zipi labda?

Mkuu hata wewe hujui kuwa kuna sababu
au umekaa sana mndenyi mpaka umesahau
Mkuu kulipiza kisasi sio suluhisho utakuwa unaongeza matatizo juu ya mengine
Hebu jaribu kukaa nae ujue sababu za kufanya hivo
 
Kwa kuwa kwa wakati huu akili yako inatawaliwa na hasira na desperation, nakushauri uahirishe kuchukua hatua zozote kwa japo wiki 2 ambapo akili yako itakuwa imetulia zaidi na utafanya maamuzi ya busara. pole sana, najua uko katika wakati mgumu...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom