Mke wangu wa ndoa ame-hack simu yangu

Mke wangu wa ndoa ame-hack simu yangu

Ulifunga ndoa ya halali au mlibebana tu kivyenu?
Kama kweli mlifunga ndoa na hichi kitu uko serous nacho anzia kanisani kwa kuwapata wakuu wako na kulifikisha swala hilo mezani na baada ya hapo Wazazi pia wanahusika kabla hata hujataka kwenda huko unakokufikiria.
 
Ah ah ah unaogopa if anachepuka? Uhiii wew huchepuki? Kama unagawa mkia wake na yy lazima agawe kipoch manyoya. Kama mchezo tunaita draw.
Mwanamke haruhusiwi kuchepuka, ulisikia wapi kwenye historia ya Dunia hii mwanamke mmoja akaolewa na zaidi ya mwanaume mmoja? Ila sisi Masheikh mpaka sasa tunaoa hadi 4 teh teh teh!
 
mpeleke mahakamani kwanini aingilie uhuru wako...mimi ni Mwanasheria nitafute nina kuhakikishia tutashinda hiyo kesi saa 2 asubuhi na fidia atakulipa na itakuwa fundisho kwa wengine wanaotunyima raha...

ukishaolewa kaa nyumbani tulia kama unaenda kazini nenda kwa amani mambo ya kupekuana pekuana kama nimeona mpepelezi sitaki
Sawa kabisa mkuu, hasa hawa kina nanihii humu ndani cjui kama kweli wameolewa!
 
Yap, especially kukiwa na vimambo vya siri siri, vitabia visivyoeleweka n.k wewe na mkeo hakuna siri kati yenu hata kama umetumia rafiki ako pesa kumshirikisha mkeo haimaanishi ndio kuomba ruhusa katika story tu unamwambia dah flani ana shida unaeongeza na chumvi kalala njaa siku ya tatu leo kaniomba hela ya kula nimemrushia elf 20. Ukishamwambia hivo kuna ubaya? Saa ngapi ataanzisha kesi hapo, Ila ukishafanya siri akigundua ye mwenyewe ndo timbwili linaanza na kupekuana kunaanzia hapo
Hata nikituma pesa kwa mchepuko pia nimtaarifu?
 
Hata nikituma pesa kwa mchepuko pia nimtaarifu?
Good na ndio hicho mkeo anachofatilia, wewe unatuma hela kwa michepuko mkeo kutumia hela kuhonga huko siijui voda siijui tigo unajitia inakuuma acha ubinafsi or tulia kama unanyolewa na mkeo nae afanye yake
 
Sawa kabisa mkuu, hasa hawa kina nanihii humu ndani cjui kama kweli wameolewa!
Siku nyingine ukihitaji ushauri wa wanandoa tu tuma thread zako kwanza pm, na kama ushafanya maamuzi yako umeomba ushauri wa nini sasa?
 
kumfanya mke ajue kila kitu sawa na kuuza ramani ya vita kwa adui wewe!!
Na mkeo akishajua kuwa umemgroup kama adui lazima akusaliti sabab hakuna namna nyingine.
Atendelea kuwa adui yako kwa siri halaf atakuwa Na protector wake na maisha yatasonga raha burudani.
 
Alichofanya mkeo ni kosa. Mpo kwenye ndoa lakin kujua taarifa bila ruhusa yako si jambo zuri. Kemea hiyo tabia. Ikijenga miziz litakuwa tatizo kwako. Kama wewe ni mfanya biashara linaweza kusababisha uhusiano wako na wateja zako ukaharibika. Nina experience amini hilo.
Ninakuhakikishia kipindi mkeo atakubaliana na wewe uwe na siri zako na mambo yako naye ameamua kuwa na siri zake na mambo yake.
Unawezafurahia mkeo amekupa uhuru unaoutaka kumbe loooh! Mwanamke ni zaidi ya umjuavyo.
 
Yes mwanaume ndo kicha cha family kuna vitu unatakiwa kusimama kama mwanaume na kuna vitu vya kushirikiana kma familia mwanaume aondoe kwanza tatizo.
Mmmh!
Tunaomba tafsiri ya neno kichwa cha familia.
Miaka ya sasa unaendekeza mfumo dume?
 
Mwanamke haruhusiwi kuchepuka, ulisikia wapi kwenye historia ya Dunia hii mwanamke mmoja akaolewa na zaidi ya mwanaume mmoja? Ila sisi Masheikh mpaka sasa tunaoa hadi 4 teh teh teh!
Hahahaaa. ... mkisikia wake kuchepuka vinawauma kwelikweli,
Ila wanaume kuchepuka ni urijali.
Hahahaaa. .... ukigawa game nje lazima na yeye agawe game nje tuuu sabab hakuna namna nyingine
 
Nilichogundua ni kuwa watu wengi wamechangia bila hata kuelewa maana ya kuhack a.k.a udukuzi. Kwakweli hata muwe mke na mume lkn hakika kila mtu ana privacy. Kitendo alichofanya mkeo ni sawa na kukuchungulia kila unavoenda chooni, je ni sawa??? Kwakweli amekudhalilisha sana, ina maana hata mawasiliano yako na mama yako anataka ajue kila kitu???? Mkuu, mkeo amekukosea pakubwa sana.
Kwa tulio kwenye ndoa tunaelewa fika kuwa si kila kitu mwenza wako lazima ajue maana vingine akijua hata kama ni vya kawaida vinaweza kuleta vurumai ndani ya ndoa
 
Sawa kabisa mkuu, hasa hawa kina nanihii humu ndani cjui kama kweli wameolewa!
Wewe huna ndoa umeamua kutunga tu,
Na kama unawatoto huyo ni mzazi mwenzio tu na mlishachokana so unatafuta uhalali wa kubwagana,
Na kama kweli una ndoa basi ni ndoa changa Wewe mwenyewe akili changa na uliingia kwenye ndoa fasheni.

Huna hata chembechembe za kufaa kuwa mume bora labda bora mume.
 
  • Thanks
Reactions: nao

Weee, ishia hapo hapo! Kama ningekuwa bora mume, mke wangu angekuwa anahaha kupiga magoti mpaka sasa akiomba msamaha? Anajua fika nikiamua kumshtaki wenzie wanabeba mumewe, na alishakiri kuwa kama cpo kwenye maisha yake na yeye hayupo duniani. Ila kutokana na michango yenu (siyo wewe) nimeamua nisimshtaki na ndio kwanza tumemaliza kujadili tatizo husika kama wanandoa na kufikia muafaka wa kumsamehe baada ya kukiri kosa lake tena akisema wazi ilitokana na wivu wake uliopindukia!
 
Hahahaaa. ... mkisikia wake kuchepuka vinawauma kwelikweli,
Ila wanaume kuchepuka ni urijali.
Hahahaaa. .... ukigawa game nje lazima na yeye agawe game nje tuuu sabab hakuna namna nyingine
Ukweli mchungu.... Unauma kuliko kristapen 😀
 
Weee, ishia hapo hapo! Kama ningekuwa bora mume, mke wangu angekuwa anahaha kupiga magoti mpaka sasa akiomba msamaha? Anajua fika nikiamua kumshtaki wenzie wanabeba mumewe, na alishakiri kuwa kama cpo kwenye maisha yake na yeye hayupo duniani. Ila kutokana na michango yenu (siyo wewe) nimeamua nisimshtaki na ndio kwanza tumemaliza kujadili tatizo husika kama wanandoa na kufikia muafaka wa kumsamehe baada ya kukiri kosa lake tena akisema wazi ilitokana na wivu wake uliopindukia!

Sasa unachotaka ushauri ama kitu gani? Kama umekiri amekupigia magoti kukuomba msamaha utakacho ni nini? Leo jumatatu Fanya uwahi mahakamani kama ulivyozamilia umetuchosha kwa ubishi bana.
 
Aisee we jamaa unajua maana ya ndoa, wewe umeshakamatika kuwa mpole tu, ana haki ya kujua mambo yote. Kwanini unapokuwa na wasiwasi wa mawasiliano unapoenda kuchukua kibali polisi kwa ajili ya kufuatilia mawasiliano si huwa wanaomba cheti cha ndoa??, kuwa mpole weka mambo sawa
 
mkuu pole sana, hapa hakuna atakaekuelewa, hii taasisi ya NDOA ni ngumu mno.... ni watu wawili pekee mnaoweza kuamua mustakabali wa hiyo ndoa......utakachoamua na kukisimamia ni wewe mwenyewe.....maisha yako amani yako.....
 
Back
Top Bottom