Ndugu wana JF,
Mimi ni kijana mwenye mke na nnamtoto kwa sasa, nilianza mahusiano na mke wangu akiwa ndo amemaliza chuo, maisha yaliendelea ila ugomvi wa hapa na pale kwenye Mahusiano yetu umekuwa wakawaida hadi tumeoana.
Tatizo kubwa lililokuwa linatugombanisha ni mahusiano yake ya nyuma na watu wake(ex-boyfriends)kuwa alikuwa ana penda sana kuwasiliana nao.
Nilipo gundua nilimkataza nae akadai hamna chochote kinacho endelea rofauti na urafiki.
Tumeishi hivyo kwa muda hadi sasa ni mwaka mke wangu amekuwa mwajiriwa selikarini-leo hii nimeingia kwenye ugomvi baada ya wife kunifuata na kuniambia ex-wake flani anashida anaomba amkope wife hela.
Mimi alipo niambia nikaweka sababu tabia ya mawasiliano na ma-ex nilisha mkataza, ila Leo kaniambia hawezi acha kumsaidia kwani kwake huyo mtu ameshakuwa ni kama ndugu kwani hata ndugu zake wana mfahamu na na anawasiliana nao wote, hivyo mm siwezi kumzuia kumusaidia na hato acha kuwasiliana nae.
Je mimi nifanyeje? Wife ana haki ya kufanya hivyo au hili ni tatizo?