Black Sniper
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 35,105
- 60,820
Yaani ni shidaMkuu wanashida kweli hawa wanawake
Yaani ni shidaMkuu wanashida kweli hawa wanawake
Nimeoa nina miezi 5 sasa ila tatizo kubwa ni kwamba mke wangu anapika chakula kidogo mno yani sishibi kabisa na namuachia hela ya matumizi ya kutosha ila sielewi nini kinamsumbua
Mpaka inafika kipindi kabla sijarudi nyumbani nipitie hotelini nile kwanza halafu ndio niende kwangu nimeongea nae sana lakini anaacha siku kadhaa halafu anarudia tena tabia yake ushauri wenu wakuu nimuache au nimfanye nini?
hii ni list of shame jf?Ngoja niwaite hawa wapendwa watoe mawazo yao kwenye huu uzi
Shunie Beef Lasagna witnessj Hajar Sky Eclat mahondaw Miss Natafuta na wanajf wengine bila kumsahau Mama Sabrina
Amesema akimwambia.... Anaacha siku kadhaaa afu anarudi a...Kwahiyo unashindwa kumwambia unakuja kulalamika hapa
Halaf hii hulka ni mbaya sana kwakweli.Lakini Madame hauoni mpaka hapo kama tatizo ni hilo hajasolve chochote?
Maana mwanaume anaanza kula hotelin ndiyo anarudi nyumbani. Hivyo hela bado inatumika vibaya.
Lakini trust me kuna watu wamezoea shida sijui ndiyo uchoyo ..hata kama ana gunia la mchele ndani bado atapika robo kilo na anafamilia.
Haha, Jamaa wala hakuitaji kutumia nguvu sana kumuelekeza mkewe.. Safi sanaHii story inanikumbusha mfanyakazi mwenzangu mmoja, alioa mke akawa anapika chakula kidogo jamaa hashibi. Siku moja jamaa akamwambia kuwa, kesho tuna wageni watatu hivyo pika chakula cha kutosha watakula mchana hapa nyumbani. Bi dada akapika chakula kama alivyoambiwa na mmewe.
Baada ya chakula kuiva akamuuliza mme mbona wageni hawafiki na chakula tayari. Jamaa akamwambia tuendelee kula wako njiani.
Jamaa akaanza kupiga msosi hotpot la kwanza likaisha, akamwambia mkewe lete na kile kingine wakija utapika kingine.
Baada ya kumaliza kula. Akamwambia hiki ndiyo kipimo cha chakula kila siku hakuna mgeni yeyote.
Hivyo nawe unaweza tumia njia hiyo.
Hili laweza kuwa kweli mkuu....Utakuwa na kitambi anataka kipungue ucheze mechi vizuri
Haaaaa hata Mimi nimewaza hivyoHuyu mke atakuwa ni Miss Natafuta bila shaka![emoji1][emoji1][emoji1]
Kubana matumizi gani huko. Na siku zote tunapambania katumbo yetu.Halaf hii hulka ni mbaya sana kwakweli.
Kuna mtu namjua mim hta kukiwa na nyanya kilo moja anataka kupika mchuzi bas amini mungu atatumia mbili tu. Sijui niseme kubana matumizi au vipi.
Za kuambiwa changanya na zako.Haha daaa nini ushauri wako hapo 'vita' unamaanisha nimpige ?
Asante NashukuruMkuu pole sana! Nakushauri kaa naye ukiwa serious mweleze kuwa hushibi, mweleze kuwa unalazimika kula migahawani na yy yupo! Ukiona haachi mwambie sili tena nyumban acha tu niwe nakula migahawani tu chukua hata siku mbili usile nyumban akikuuliza mwambie nimekula huko! Kwa mwanamke anayempenda mume wake atabadilika asipobadilika washirikishe ndg was pande zote mbili.