Mke wangu anunuliwa nguo za ndani na mwanaume

Bm_boy

JF-Expert Member
Oct 21, 2013
547
347
Wakuu habarini,

Natumai mko poa na zaidi mkiendelea kufuatilia vita dhidi ya dawa za kulevya.

Kwangu mimi nakuja na hili ambalo mpaka sasa silielewi limekaa kaaje, na hili ni baada ya kudukua mawasiliano ya mke wangu na kukuta jamaa akimwambia zawadi yako ipo tayari hivyo watafutane ampatie.

Baada ya siku mbili tatu nikaona kimfuko kipo na chupi nne na brazia mbili, sikuuliza ila nikahisi hii ndio ile zawadi. Nikaamua kudukua mawasiliano yake tena. Nikakutana tena na mawasiliano wakiulizana vipi ameipenda zawadi na je zimemtosha.

Kiumweli ni zaidi ya wiki tatu sasa sijamuuliza au kuonyesha tofauti yoyote kwake, ila bado najiuliza ni sahihi kwa mwanamke tena mke wa mtu kupewa zawadi ya chupi au brazia na mwanaume tofauti na mume/mpenzi wake.

Lakini pia je huyu mwanamke anaweza kuendelea kuwa na vigezo vya kuendelea kuwa mke. La mwisho ni mwanamke/mwanaume anapokuwa anaamua kumnunulia mwenzake nguo za ndani anakua anamaanisha nini?

Natumai mawazo yenu yatanisaidia.

Asante!
 
Muulize ili upate ukweli badala ya kupoteza muda na kuanza kufanya judgements bila information ya kutosha.
 
Wakuu Habarini

Natumai mko poa na zaidi mkiendelea kufuatilia vita dhidi ya dawa za kulevya.

Kwangu mimi na kuja na hili ambalo mpaka sasa silielewi limekaa kaaje, na hili ni baada yakudakua mawasiliano ya mke wangu na kukuta Jamaa akimwambia zawadi yako ipo tayari hivyo wataftane ampatie..

Baada ya siku mbili tatu nakaona kimfuko kipo na chupi nne na brazia mbili, sikuuliza ila nikahisi hii ndio ile zawadi. Nikaamua kudakua mawasiliano yake tena.

Nikakutana tena na mawasiliano wakiulizana vip ameipenda zawadi na je zimemtosha.

Kiumweli ni zaidi ya wiki tatu sasa sijamuuliza au kuonyesha tofauti yoyote kwake, ila bado najiuliza ni sahihi kwa mwanamke tena mke wa mtu kupewa zawadi ya chupi au brazia na mwanaume tofauti na mume / mpenzi wake..!

Lakini pia je huyu mwanamke anaweza kuendelea kua na vigezo vya kuendelea kua mke.

Lamwisho ni mwanamke / Mwanaume anapokua anaamua kumnunulia mwenzake nguo za ndani anakua anamaanisha nn.. ?

Natumai mawazo yenu yatanisaidia Asante.!
Muambie nawewe akununulie.
 
Huenda ikawa wewe ni mmoja kati ya wale wanaume wasiojali mke anahitaji nini na ukamtimizia ndio mana katafuta wa kumnunulia.

Nadhani kwa mawazo yako unajua mke anaridhishwa kwa ngono pekee kumbe hata chupi ya kuvaa ana.
 
Muulize ili upate ukweli badala ya kupoteza muda na kuanza kufanya judgements bila information ya kutosha.
Mkuu unategemea akuambie ni kweli ka nunuliwa.. me niko na ushaidi wa kutosha coz mawasiliano niliyoyapata na ninayo niyasauti.!
 
Hivi Wenzetu mbona Mna bahati namna hii?

Una Akili timamu kweli?

Na hali ngumu hivi ya maisha mkeo ananunuliwa chupi 4 na brazia 2 na Mwanaume mwingine halafu badala ufurahi wewe ni kama unalalamika vile.

Mkulu mwenyewe na ubabe wake wote anaenda kuwaomba Wanaume wengine tena wa Uturuki na morocco misaada kwa ajili ya watu karibu mil. 50

Wewe umesaidiwa chupi 4 kwa ajili ya mtu mmoja tu unachukia?
 
Back
Top Bottom