Coffee
JF-Expert Member
- Jul 16, 2017
- 1,304
- 1,313
Humphrey polepole ama? DohGeofrey, Gregory, gaspar, Humphrey,
Humphrey polepole ama? DohGeofrey, Gregory, gaspar, Humphrey,
.............Nisikudanganye mkuu!zaidi ya tabia za kawaida za kitoto huwezi ku-notes tabia za jina fulani kama ni nzuri au mbaya hadi kwa mtoto wa kiume miaka 14 wa kike 17.Ahsante mwanajamii majina ya kurithisha hapana nilishayakataa kitambo na mke wangu. vipi makuzi yao yapoje hao wa kwako maria &Daniel
Hata maria na Daniel yapo kwenye mitandao.Cha msingi mi naona ni kumwita mtoto jina lenye maana nzuri.Sikushauri sana kutafuta majina mitandaoni ni vizuri majina ya watoto wako ukayatoa kwenye Biblia.
Mimi nina Daniel na Maria,Daniel kwa sababu alifanya kazi ya Mungu kishujaa bila kusita sita na Maria kwa sababu alimleta Mkombozi duniani pia kwa imani yangu {Catholic} alizaliwa siku ya pili ya mwezi Mtakatifu wa Maria.
Hizi tabia za kuita watoto majina sijui Bryan qu sijui brayton au Morin au Melinda huku hujui hayo majina yaliakisi nini ktk maisha ya hao watu ni hatari sana.pia nakupongeza kwa kukataa majina ya kurithi.
Kila mtoto uja na baraka zake toka kwa Mungu. Mungu pekee ndio awezaye kutoa jina bora sana. Nakushauri piga goti na muombe Mungu akupatie jina la Mwanao mtarajiwa.Mambo vipi wanajamii poleni na mvua za kuikaribisha pasaka . me ni mgeni Jukwaani lakini napenda kushare nanyi hili.
Mke wangu ni mjamzito na mtoto atakayezaliwa natarajia Jinsia ya me na umebaki mwezi mmoja tu ajifungue. sasa sitaki majina ya kurithi wala ya kutokea upande mmoja wa mke wangu au kwangu mimi .naomba mnisaidie jina gani zuri zuri litamfanya awe mtoto wa kipekee upande wa Dini ni mkristo pendekeza the best name......
karibuni wanajamii
hili la Gregory. nimelipenda zuri ahsante
Bado una ule ushamba wa miaka ya sitini ya kutafuta majina ya kizungu na kuamini ndiyo bora? Bado unaamini majina ya kiafrika yana mikosi? Bado unaamini kuwa kuna jina la kipagani na jina la kikristo? Laiti ungejua kamba hao kina Gregory ukienda kwao Ulaya utakuta waliishaacha kwenda kanisani siku nyingi. Jina halina uhusiano wowote na dini hizo ni imani potofu. Jiamini na mwite mtoto wako jina la asili ya kwenu.hili la Gregory. nimelipenda zuri ahsante