Mke wangu ametoa mimba kwa siri

Mke wangu ametoa mimba kwa siri

Pole sana labda niulize kama mna watoto na wangapi? je una simamia majukumu yako kaba baba au mume? unakuwepo pindi familia yako inakuhitaji? sababu pesa sio kila kitu uwepo wako nao pia unachangia.. usijitie BP mkuu watoto mwenyezi mungu ndio anapanga msubiri mkeo apate afya njema kaeni chini myamalize kama watoto inshallah mtapata wengine,huenda ikawa hajui kama alikua na mimba...
Kwakweli nijitahidi kulea familia na tuna watoto wawili
 
1.JAMANI KUMBUKENI KUWA KAPEWA RIPOTI NA DOKTA NA KAMWAMBIA "ALITOA MIMBA" SIO MIMBA ILIHARIBIKA....NADHANI DOKTA ANAJUA ZAIDI KWENYE HILO.
2.PILI HUYO KAUA AKA MUUAJI, SIWEZI KUKAA NAMTU WA NAMNA HIYO KABISA " MTU ANAEUA KITU KISICHOWEZA JITETEA" MALAIKA NI MTU MBAYA SANA....NITAISHI NA JAMBAZI ANAYETUMIA BUNDUKIA BUT SIO MWANAMKE ANAEUA KIUMBE KISICHOJITETE AIJALISHI SABABU YA KUFANYA HIVYO " JAMBZI LIKIINGIA LITAPIGA RISASI WATU WAZIMA KAMWE HALITAPIGA MTOTO AIYEJITETEA " BUT WANAWAKE MMMH!! ROHO ZAO BALAA.
3.HIYO HAIKUWA MIMBA YAKO SO AKILI KIMKICHWA.
4. ILA MIMI NINGEMTIMUA" HAKUNA SABABU YYTE DUNIANI AMBAYE IMEMFANYA ETI AKUAMBIE ANAENDA KUTOA MIMBA KAMA KWELI ILIKUWA YAKO" ULITAKIWA UJUE KWANZA ANA MIMBA ................HUYO SIO WA KUISHI NAE COZ SOON ATAKU---R.i.P
 
Umenikumbusha mbali sana mkuu,kabinti kangu ka miaka 4 kazuri sana,yaani huwa nakaangalia najisemea tu moyoni dah atakae kaoa atakuwa amepata mke bomba kabisa.but you know what?nisingekuwa na huyu binti kama nisingekomaa.miezi sita baada ya kujifungua waifu alinasa tens,hakuwa tayari kuzaa.alipinga vibaya kwa sababu lukuki ili mradi tu aitoe mimba,asizae.baada ya mabishano ya siku kadhaa nikafanya uamuzi sasa kama mwanamme,mume na baba wa familia. nikamwambia fine,PAKI NGUO ZA KUTOSHA UENDE KWA WAZAZI WAKO WAKAKUTOE HIYO MIMBA,THEN UKISHAPONA NIJULISHE NITAKUJA KUKUPA TALAKA MBELE YA WAZAZI WAKO.KUHUSU HUYU MWANETU WA KWANZA NITAJUA LA KUFANYA NITAKAPOKUJA.ili kusisitiza nikampigia simu mama mkwe palepale na kumwambia binti yako anakuja utamsikiliza shida yake.sikutoa maelezo zaidi.kuona hivyo akanywea Leo nina binti wa nguvu,wa ukweli nategemea kuanza kufuga mbwa muda si mrefu
 
Duh! Hiyo ngumu sana kumeza maana.....
Kwa mtazamo wangu huyo mtoto hakua wako mkuu ndio maana aliamua kuutoa huo ujauzito. Hata kama hakua tayar kuzaa kwa muda huo au vyovyote vile angekushirikisha kuwa anataka kuutoa. Ila hukushirikishwa jua mwenye nao alishirikishwa na huo ndio ukawa mwafaka wautoe
 
Halaf mtoa mada ujue umetupa upande 1tu wa story
Hakuna lingine?!... Yaani hakuna mtafaruku kati yenu?!
 
Kwa hili siwezi nikasema lolote aiseeee......
Maana haya mambo hua magumu sana mkuu, hasa nikikumbuka nilivyo kua nachapiwa na nikajua naushahidi ulikuwepo (picha).
Lakini mwisho wa siku niliishia kuendelea kuanae tu....
Hizi Kei bhana.....😀
Unazielewa eeee(kei)...hufurukuti mzee mzima[emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] hatarrrr
 
pole sana ndugu,,kwa prediction ya haraka haraka tu ni kuwa alipata mimba kutoka kwa mchepuko kwa hiyo akaamua kutoa ili isijekuwa soo
 
Mpongeze kwa hilo!, kutoa mimba si kazi rahisi "Nani kama mama!". Ameamua kuua kwa kukusudia, ameamua kumpuuza Mungu wake, mke wako ni jasiri sana kuliko hata wewe; sema tu ana sura laini kuliko wewe!. Mwanamke akiamua kutenda dhambi anatenda bila hata kukuogopa wewe! isipokuwa wewe ukitaka kutenda dhambi utamuogopa mke wako hutomuogopa Mungu!.. ...Nakushauri mpongeze mkeo kwa kutoa ujauzito maana angeamua kukutoa wewe...tungeona a/c yako ya jamiiforum inakuwa DORMANT
Umenifikirisha sana.
 
Pole sana mkuu. Najaribu kuvaa viatu vyako. Sema nashindwa kujua unavaa namba ngapi. Mwanamke huyu ni shida. Mimba haikuwa yako hiyo. Tafakari. Chukua hatua.
 
Kaka anzia alipoishia yeye, Kama katoa mimba we MTOE yeye...Ukichelewa utatolewa na wewe...haina majadiliano dhambi aliyotenda ni kubwa saana

Yawezekana ametenda dhambi kubwa sana, tena isiyo na kifani.
Lakini ukizungumza nae na kutafakari kwamba kwanini katenda dhambi hiyo, lazima utabaini kwamba aliitenda ili kunusuru ndoa yake.
Kuzungumza ni jambo la busara na kusamehe ni sehemu ya maisha kwakua dhambi tuliumbiwa.
 
Back
Top Bottom