Mke wangu amelipiza kisasi,nifanye nini.

Mke wangu amelipiza kisasi,nifanye nini.

hiyo ndo michezo yenu mkuu, wife alikua anaiba kama kawaida ila ameamua kuzuga

ushauri wangu:
1.wote mna makosa samehaneni, then ingawa ni kweli uo mchezo ni mwendelezo usitake kuamini ili upate nguvu ya kumsamehe- yaani danganya nafsi yako

2. tayari mna familia msiwaathiri watoto kisaikologia na malezi ya ukuaji kwaiyo rudianeni alafu iwe siri yenu

3. kijana mwiba gemu muondoe haraka ata kama ni mchapakazi mahiri

nakutakia mwanzo mpya wenye mafanikio
 
Pole mkuu hatakama ukitenda halafu ukatendewa inauma sana pole dhamiria kuto kurudia tena ndio toba ya kweli pia msamehe kaka.
 
Huyo mama alijua kama utakwenda shamba kuchuka maziwa. Hivyo aliamua tu kuingia ndani ya kibanda kile, akijua ukija utamkuta mle ili uumie, na wala hajafanya tendo lolote na house boy, ila alijifanya yuko mle ili uone inavyouma ukitendewa. Dunia imepasuka kwa uzinzi, hivyo kama unaona inauma, basi jua hata kwake iliuma. Suluhisho ni kusameheana na kuanza mwanzo wote kwa uaminifu. Sivyo, wote fungulieni mbwa.
 
mhh hiyo kali kaka, msamehe mkeo ila amekudhalilisha sana, haipaswi kulipiza kisasi, angemwomba Mungu akusamehe maana ipo siku nawe Mungu angekuadhibu kwa kutokuwa mwaminifu. huyo ni mkeo amefanya hivyo, je huyo girl friend wako unamwamina km upo peke yako? naye ndo kwanza anamwingine maana anajua ww una mke so unampotezea tu naye anakukomesha kwa mwingine usikute analala huko huko wakati ww upo na mkeo nyumbani. hujaepuka kitu dawa ni kuwa mwaminifu kwa mkeo naye mkeo atatulia tu. yaani unatia aibu kwa kutokuwa mwaminifu kwenye ndoa yako. endelea tu yaana ukimwi upo njiani unakuita.
 
Mnaowazungumzia ni watu au hayawani wa porini?

Manake within the story nasikia mifugo mara maziwa na kugegedana hovyo hovyo, je mnazungumzia nguruwe?
 
Mtenda akitendewa.........iyo ndo ngangali au jino kwa jino au akuanzae wewe mmalizie

..................hujihisi kaonewa . wakati anafanya yeye alidhani mkewe hatoumi ila alipofanya mkewe yeye anaumi, mm huwa nashindwa kuwaelewa wanaume, inamaana nyinyi ndiyo mmeumbwa na mioyo ya nyama, halafu sisi wanawake tumeumbwa na miyo ya vyuma ambayo inakuwa haiskii maumivu kwa vitendo vyenu mnavyofanya? hata sisi tuwanadamu tunaumia sana sema huwa Mungu ametupa busara ya uvumilivu.
 
Mtenda akitendewa.........iyo ndo ngangali au jino kwa jino au akuanzae wewe mmalizie

Watu wa kulipiza visasi ni wabaya sana,huwa hawaachi hiyo tabia atalipiza tena na tena na tena,ameshaonja ya cowboy atafuata ya shopkeeper nk.
 
Mimi namuacha hapo hapo.. No rooms for error
 
Isomeni vizuri hiyo story, ni athari za kuangalia bongo movies, nigerian movies na ghana movies....hakuna ukweli humo, zaidi ya imaginations na kuongeza idadi ya threads.......thats just my take......
 
eti girl friend,yaani kuna vichwa maji kweli humu

wanaogopa kusema HAWARA, jamani huo ni msamiati wa kiswahili utumieni! Hata neno UGONI watu wanalikimbia, ooh nimemfumania mume/mke, mnaficha nini, semeni tu nimemkamata ugoni na hawara yake full stop!
 
Kampime huyo shamba boy ukimwi halafu maisha yaendelee, ila usirudie na mkeo asirudie.
 
Duh umesema ushauri wa humu haukukusaidia vile, basi fata roho yako. Mie hata kwa dawa siwezi fikiria kufanya tendo hilo maana ningefanyiziwa mara milioni na hata kuachwa live. ila kachemsha bora angetafuta mwanaume aliyeuzidi ndio angekuacha unababaika kuchukuliwa mke ila kaenda that low mmmh hiyo noma kweli.

haya fata roho yako, ila najua kwa wanaume huwa hawasamehi mke kukamatwa live kihivyo. sasa mkapimane kama mnataka kuendelea kuwa wote hata kama hutaki tena as ndoa yenu imeingia doa basi bado mkapime.

pole, ila sijui umejifunza au ndio unataka kuendelea na huyo girlfriend wako naamini bado haujaachana nae?
 
Kama ningekuwa mimi ndoa ingeishia huko huko shambani.
 
kama wadau walivyosema huyo mke wako alishaanza hako kamchezo siku nyingi, kusema kwamba alikuwa analipiza kisasi ni kujustify tu maovu yake, haiingi akilini kwamba wameanza hiyo kitu very recently. all in all may be a source of the problem (jichunguze)
 
Back
Top Bottom