Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 43,037
- 34,742
- Thread starter
- #41
Mke Wangu Alinifanya Niwe Mchawi-12.........
ILIPOISHIA;
Niliamini kama ningemueleza yale yote niliyoyasikia ningekuwa nimevunja masharti ya kurudi nyumbani bila taarifa japokuwa simu yangu haikupokelewa.
SASA ENDELEA...
KAMA angeamua kuniacha, kwangu lingekuwa pigo kubwa kutengana na mke wangu ambaye pamoja na matatizo yote bado alikuwa mtu muhimu sana katika maisha yangu.
"Au bado una yaleyale?" mke wangu aliniuliza kwa sauti ya unyonge.
"Yapi hayo?" Nilimuuliza kwa kuhofia labda ameshtukia.
"Si kuhusu mgogoro wetu kuwa miye natembea nje ya ndoa?"
"Walaa yote mbona yalishaisha."
"Ndiyo maana nikaja kupanga huku tuishi kwa raha mustarehe, mume wangu tangu tuhamie huku nimewahi kuondoka bila ruhusa yako?"
"Hapana."
"Au nimeishafanya jambo lolote baya?"
"Hapana."
"Au lile la kutoa mimba bado linakutesa?
"Walaa."
"Sasa nini mume wangu?"
"Nina wasiwasi malaria bado haijaisha," ilibidi nidanganye ili kumfanya mke wangu aachane na mimi kwa vile alikuwa kero mbele yangu.
"Basi mpenzi naomba ukaangalie afya yako kwa kweli hali yako ilivyo hata mimi sina raha," mke wangu alisema kwa sauti ya huruma.
"Nina imani nitakuwa katika hali ya kawaida muda si mrefu."
"Fanya hivyo mume wangu."
Maneno ya mke wangu bila kumfumania nisingekubali kama anaihujumu ndoa yetu, alikuwa na maneno matamu yenye kumfanya maskini kujiona tajiri na asiye na nguvu kujiona anaweza kuibeba dunia nzima peke yake.
Nilikubaliana naye ili aondoke karibu yangu lakini nilipokuwa kazini moyo wangu ulikosa raha na kujuta siku niliyokuwa nikiumwa na kurudi nyumbani na kuyakuta yale niliyoyakuta.
Heri ningeendelea kuamini kuwa naibiwa bila kuwa na uhakika kama siku ile nilivyoshuhudia kwa macho yangu.
Kila nilipokuwa peke yangu tukio la kumfumania mke wangu lilijirudia na kuwa mateso mazito moyoni mwangu.
Kila kukicha mwili wangu ulikuwa ukipoteza ubora wake na kila aliyekuwa akinijua aliniuliza nimekumbwa na kitu gani, hata bosi wangu ambaye alifikia hatua ya kunibembeleza ili nimweleze ninasumbuliwa na nini ili aweze kunisaidia hata kwa uwezo wa kifedha lakini sikumwambia.
Moyoni niliapa kufa na siri yangu kwa kutomwambia mtu yeyote tukio lile la aibu.
Hali yangu ya kiafya ilibadilika na mwili kupungua uzito kutokana na mawazo, chakula nilikula lakini sikusikia ladha yake, kuna kipindi nililaani kuwa maskini kwa kuamini kama ningekuwa na uwezo mke wangu asingechukuliwa na mwenye fedha.
Siku moja rafiki yangu wa karibu Simon alinifuata baada ya kunikuta nikiwa nimejisahau huku machozi yakinitoka.
"Kazala," aliita kwa sauti.
"Ee..eeh?" Nilishtuka kama niliyekuwa usingizini.
"Kazala una tatizo gani rafiki yangu?" Aliniuliza akiwa amenikazia macho.
"Sina tatizo," nilimjibu huku nikifuta machozi kwa kiganja.
"Hapana Kazala, una tatizo zito lakini hutaki kulisema."
"Nipo sawa rafiki yangu," nilikataa kwa kuamini kusema linalonisumbua nitakuwa nimejivua nguo hadharani.
"Kalaza unajiona ulivyo?"
"Kwani vipi?" nilijifanya kushtuka japokuwa ukweli niliujua.
"Haupo sawa, usiponieleza mimi swahiba wako utamueleza nani? Kumbuka mimi huku ndiye ndugu yako wa karibu.
Ingawa tangu mlipohamia Uzunguni hutaki nifike kwako kwa kusingizio cha mkeo na kusahau ukifa sisi ndiyo tutakaokuzika."
Kauli ya Simon ilikuwa na ukweli kwani ndiye aliyekuwa mtu wangu wa karibu kwa kuelezana siri zetu za ndani.
Lakini siri ya mke wangu sikuwahi kumweleza hata siku moja ingawaje ilikuwa ikifahamika mtaani lakini hakukuwa na mfanyakazi mwenzangu aliyekuwa akijua kilichokuwa kikiendelea ndani ya nyumba yangu.
Pia, mke wangu baada ya kuhamia makao mapya alipiga marufuku marafiki zangu wote akiwemo Simon asifike kwetu, nami kutokana na mapenzi mazito nilimkubalia.
"Simon nipo sawa," bado niliendelea kufa na siri yangu moyoni.
Itaendelea baadae........