Mke wangu alinifanya niwe Mchawi -1

Huwa nashangaa sana, kila kukicha mwanamke anasingiziwa mambo mabaya tu. Naomba mtuletee pia 'mume wangu alinifanya kuwa mchawi'.
 
Hii story nilikuwaga naisoma kwa shigongo sijui hata ilipotelea wapi, sikuwahi kuimaliza, ahsante mzizi kwa kuileta huku
Lakini mzizi mwendelezo kutoka sehemu moja kuingia nyingine kuna vitu unaruka, so unaondoa uhondo, angalia sehemu ya 14 kwenda ya 15 kuna maneno umeyaacha hapo
 
Mke Wangu Alinifanya Niwe Mchawi-24...........

ILIPOISHIA;
"Kazala lazima tumtie adabu, mzee mfanyie kama yangu."
Nilishtuka na kujiuliza kama yake ipo vipi? Ilibidi niulize.
SASA ENDELEA..


"Ulimpa adhabu gani?"
"Nilimpoteza kwenye sura ya dunia," Shedu alijibu kwa kujiamini.
"Ha! Unamaanisha ulimuua?"
"Ndiyo! Kanitesa sana yule mshenzi kasababisha mwanangu wa kwanza afe baada ya mke wangu kumuacha na kwenda kwa huyo mwanaume na kusababisha mwanangu afe kwenye beseni la maji."
"Mungu wangu!" nilishtuka na kushika mdomo.
"Kibaya mtu yule hakuishia hapo, alimchanganya mke wangu kiasi cha kudai talaka. Nilimfuata na kumueleza aachane na mke wangu majibu aliyonijibu yalikuwa ya udhalilishaji. Eti aliniambia kama namuona mke wangu anafaidi yeye kuwa naye na mimi niwe mpenzi wake."
"Uwe mpenzi wake alimaanisha nini?"
"Eti niwe mkewe."
"Mungu wangu!" kauli ile ilinishtua sana.
"Kazala wee acha tu, mtu akiwa na fedha ana dharau ndiyo maana jambo lako nililichukua kama langu. Kazala nimeteseka mpaka nilipoletwa huku kwa mzee Kidereko."
"Ina maana ulikuwa humjui tokea awali?"
"Matatizo ndiyo yaliyonifanya nifike huku, we si unajua kabila langu?"
"Nilishangaa pale uliponileta huku na kabila lako, nikajua baba ndiye Mnyamwezi ma mama mtu wa Tanga."
"Walaa."
"Yalikuwa mateso ya muda gani?"
"Miezi nane lakini kwangu ilikuwa miaka mia nane."
"Pole sana.... ikawaje?" nilijikuta nikiwa na shauku baada ya kuona matukio yetu yanafanana sana.
"Baada ya kuletwa huku sikutaka adhabu kali, lakini babu aliniambia mtu huyo nikimchelewesha ataniwahi mimi.
"Kutokana na mateso niliyoyapata na uchungu wa kifo cha mwanangu nilikubali."
"Mmh! Ikawaje?"
"Basi mzee akatengeneza mambo, sikuwepo ila waliokuwepo na kutoa ushuhuda walisema baada ya kwenda nyumba ya wageni na mke wangu ambaye yeye alijimilikisha na kuwa mkewe. Kutokana na maneno aliyoyasema mke wangu, aliyekuwepo kwenye tukio wakiwa faragha.
"Baada ya kumaliza mchezo wao uume haukupoa uliendelea kuwa vile vile, kama chuma na kuuma maumivu makali sana.
"Alipiga kelele za maumivu, ilibidi achukuliwe na kupelekwa hospitali, huko alipigwa sindano za ganzi ili uume upoe lakini wapi, kila dakika maumivu yalikuwa makali alilia mpaka sauti ikakauka. Nasikia alinitaja mimi ili niende akaniombe msamaha.
"Nguvu zilimwisha mateso yale yaliendelea kwa saa nane, jioni uume ulinywea na yeye kufariki dunia."
"Mmh! Aliteseka sana."
"Yeye kwa saa nane mimi miezi minane, kuchanganyikiwa kubaya nakumbuka kuna kipindi nilikuwa natembea nikizungumza peke yangu. Kingine hali yangu ya kimaisha ilikuwa mbaya hapo ndipo nilipozidi kuumia."
"Baada ya hapo nini kiliendelea?" nilijikuta nikivutwa na simulizi ya Shedu.
"Mke wangu alirudi huku mtaani kila mmoja akiniheshimu mpaka leo hakuna mtu wa kumgusa mke wangu. Hata akija mgeni lazima atapewa taarifa za yule jamaa aliyejitia kidume na kulamba udongo. Basi akipata taarifa ile humkalia mbali mke wangu."
"Lakini mbona kama adhabu ni kubwa sana?"
"Kazala acha huruma wanadamu si wa kuwachekea ona anavyoteseka kwa haki yako."
"Sawa lakini kuua!" bado niliona adhabu ya kuua ni kubwa.
"Kijana acha ujinga, siku zote akuanzae mmalize," mzee Kidereko alisema.
"Sawa mzee wangu, mi shida yangu kumrudisha mke wangu tu si kuua."
"Sawa, ila lolote litakalotokea usirudi hapa."
"Kwa nini babu?"
"Inaonekana hujihurumii, kwa hiyo naomba ukiondoka hapa usirudi labda uje na lingine. Mimi hupenda kufanya kazi mara moja ili usirudi hapa kwa kazi hiyohiyo. Kwa akili ya mkeo hata kama atarudi bado ataendelea kukusumbua. Nakueleza utarudi hapa nguo zipo kichwani."
"Kwa nini unasema hivyo?"
"We si mtoto mdogo mambo mangapi kakufanyia mkeo nusra ujiue, kweli au uongo?"
"Kweli."
"Sasa kwa nini mtu aliyetaka kukusababishia ujiue unamuonea huruma. Nataka kukueleza huruma ikizidi hugeuka uchawi wa kukuzuru mwenyewe hasa kwa adui yako."
Nilitulia kwa muda nikiwaza na kuwazua juu ya adhabu wanayotaka kuifanya kwa mwanaume aliyemchukua mke wangu. Kauli za kurudi nguo nimeweka kichwani zilinitisha sana na kujua kurudi pale nitakuwa mwendawazimu.



Itaendelea Baadae............

Hii story huwa naipenda sana ngoja leo niisome
 
Back
Top Bottom