John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,373
Familia ya msanii wa Bongo Fleva, Joseph Haule ‘Profesa Jay’ imejitokeza hadharani na kuelezea juu ya hali ya kiafya anayopitia staa huyo na kuomba msaada wa matibabu yake.
Jay ambaye pia alikuwa ni Mbunge wa Mikumi, alipoanza kuugua alipelekwa katika hospitali mitaa ya Tegeta, akahamishwa kupelekwa Lugalo na baadaye akahamishiwa Muhimbili ambapo ndipo alipo hadi sasa, lakini baadaye kukawa na ukimya wa taarifa.
Wakizungumza katika mahojiano ya Kituo cha Clouds FM, leo Jumatano, familia hiyo ikiongozwa na mke wa Jay, Grace Mgonjo pamoja na mdogo wa Jay, Black Rhino, wameelezea kuwa Profesa ni mgonjwa na wamekuwa wakitumia gharama kubwa katika matibabu yake bila kufafanua zaidi kuhusu ugonjwa unaomsumbua.
“Wakati tunaanza kuuguza hatukutarajia kama itakuwa serious, tulijua ni kitu cha muda mfupi kisha atapona.
“Jay ni mtu wa watu, sababu ya kuamua kuzungumza hadharani ni kwa kuwa ana mashabiki wengi, tukaona hatumtendei haki, tunaomba watu waungane nasi zaidi tumuingize lwenye maombi yetu ili apone, lakini suala la pesa nalo ni muhimu pia,” alisema Grace.
Baadhi ya wasanii na watu maarufu walipiga simu redioni hapo na kuchangia matibabu akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds FM, Joseph Kusaga ambaye alitoa mchango wa Sh milioni 2.
Walitaja namba na njia wanazoweza kutuma michango ya kusaidia matibabu ya msanii huyo kuwa ni:
MPESA: 0757919192 Joseph Haule,
TiGOPesa: 0715919192 Joseph Haule,
CRDB account no: 0112044845200 Joseph Leonard Haule