Mke wa mtu ananiomba niigize kama jamaa yake

FYATU

JF-Expert Member
Dec 7, 2011
5,392
4,468
"Hawezi kukufanya chochote bana yule mimi namjua" haya ndio maneno yake anayoyarudiarudia kila mara ninapomsisitizia kuwa siwezi kufanya hivyo...Huyu Dada tuna ukaribu naye kibiashara na sina uhusiano nae wa kimapenzi na wala sitarajii kufanya hivyo.

Mumewe tunafahamiana juujuu tu ila naye ameshajiridhisha kuwa sina hatari yoyote kwa mkewe zaidi ya kazi.

Ingawa Mwana Dada haweki wazi sana ni nini lengo lake la kutaka ionekane hivyo zaidi ya kusema tu anataka ampe jamaa tumbo joto bila kujali madhara gani yanayoweza kunikuta mimi "Muigizaji".

Nikimuuliza anataka nifanye nini husema anataka niwe namrudisha nyumbani kwake usiku na Mumewe ajue kuwa alikuwa na mimi, ingawa yeye atakuwa anamwambia alikuwa na mimi kikazi huku akijua wazi Jamaa atapatwa na jekejeke...na hilo ndio haswa lengo lake.

Ukisikia mtihani ndio huu.
 
Huyo atakuwa kapigwa matukio double double na mmewe sasa anataka kumuonyesha kuwa na yeye mrembo hata wa nje wanampenda ndo anataka akutumie wewe kumrusha mmewe
Ukikubali kitakupata kitu manake wanaume wanapenda wachepuke wao tu na sio wake zao!In short mkimbie huyo bibie
 
Unahonjeshwa sumu kwa kuinywa asee utapigwa fumanizi hadi ushangae
Kwa ninavyoishi na huyu Mdada wala simuoni yeye kufanya set up (mtego) ya kufumaniwa....sanasana nilichomsoma ni kuwa huenda anamfahamu jamaa yake kwa upande mmoja tu na kujiridhisha kwamba labda ndivyo alivyo.

Hofu yangu ni yale yale ya umdhaniaye ndiye siye, hata Ng'ombe uliyemzoea miaka yote kuna siku atakupiga pembe akakuvunja kiuno.
 
Usikubali labda aigize na msaidizi waķo kwa kumpatia gari awe anamrudisha
 
Apo kuna mchezo unachezewa ukijaa tu kwenye mfumo 4-4-2 umeisha mkuu kuwa makini huyo mke wa mtu atakuingiza matatizoni.
Kwa mawazo yangu nadhani inawindwa hiyo biashara yako kwahiyo kuwa makini utatolewa kwenye reli.
 
Back
Top Bottom