Mke wa Lowassa azindua kitabu

Kuna kitu nashindwa kukielewa sawa ama kupata picha halisi; Mbona sehemu kubwa ya waalikwa ni viongozi wa makanisa?
 
Ha ha haa :):):)Imenikumbusha mbaaali wakati ule kamanda Suleiman Kova alikuwa RPC Mbeya!
Akaita waandishi wa habari wa vyombo vyoote pale Mbeya... Akawaonyesha Kompyuta kuubwa pale mezani kwake,baada ya kuwaeleza madhumuni ya kuwaita pale mojawapo likiwa la kupambana na matukio ya ujambazi Mkoani hapo.Likiwemo la kuzindua Tovuti ambayo itawarahisishia wananchi kuweza kuweka/ripoti maoni yao kuhusiana na masuala ya kipolisi... hilo halikuwa tatizo...tatizo likawa hiyo Tovuti yenyewe sasa (Japo silikumbuki jina tena) Mfano: Polisimbeya[SIZE="6"][B]@yahoo.com[/B][/SIZE] au tuseme malalamikombeya[B][SIZE="6"]@yahoo.com[/SIZE][/B]...LOL:rolleyes::rolleyes::rolleyes:
Tusimlaumu Mama Lowassa kama Afande kova ambaye naye hakujua tofauti ya Tovuti na Email Add.yeye hakujua tofauti ya (Ki)Jarida na Kitabu...
 
Kuna kitu nashindwa kukielewa sawa ama kupata picha halisi; Mbona sehemu kubwa ya waalikwa ni viongozi wa makanisa?

Ni siasa za udini za wanamtandao hizo. Maana JK naye siku hizi kwa maulid hajambo kwi kwi kwi kwi. Lakini lazima wanaJF tuzipige vita.
 
Kuna kitu nashindwa kukielewa sawa ama kupata picha halisi; Mbona sehemu kubwa ya waalikwa ni viongozi wa makanisa?

Nukuu ya Lowassa hiyo hapo chini ndo maana walikuwepo hapo...
Akizunmgumza katika hafla hiyo, Lowassa mwenyewe alisema baada ya kupata matatizo nayo, yeye na familia yake waliamua kumgeukia Mungu na kwamba ndio maana wakaamua kwenda Israel kutembelea maeneo takatifu.
 
Jamani msichanganye mambo hapa. Watumishi wa Mungu wanatakiwa kuwapenda watu wote na hasa wakosefu zaidi ili waweze kujirudi. Nina imani walikaribishwa tu kwenye hiyo hafla kama yote mwingine. Makanisani tunaingia wasafi na wadhambi, majambazi na wauwaji, na wote tunashiriki ibada na kutoa sadaka. Hatumtolei sadaka Pengo, Malasusa, wala Sendoro bali Mungu. Ni mpaka tuwe tayari kukiri wenyewe binafsi kuwa tumekosa mbele ya wanadamu na Mungu, hakuna kiongozi yeyote wa dini mwenye uwezo wa kuingilia nafsi zetu na kutubagua. Unless tufanye makosa ya wazi ambayo kisheria za kanisa yanaruhusu tutengwe. Kumbuka hata tukitengwa, tukiomba msamaha tunarudishwa kundini na haohao waungwana.

La pili ni 'substance' na 'volume' ya kilichokuwa kinazinduliwa - siwezi kulisemea sana maana sijakiona. Kwa haraka haraka tu sina shaka hizi ni karatasi zake za kwanza ever! (Sina hakika kama amewahi hata kuandkika dissertation/thesis?)

La tatu ni hidden agenda ya uzinduzi wa kitabu hicho. Tukumbuke EL is clever (hasa kwenye nyanja ya ufisadi). The fact kwamba hakuna chombo chochote humu nchini kimentia hatiani for any wrong doing other than maneno neno tu ya JF na wengine (ambayo hayavunji mfupa) anajua hana cha kumzuia kushiriki na hawa watu wa Mungu. Na hawa watu wa Mungu hawana sababu ya kupika majungu - maana ni wazi kweli kwamba EL alijiuzulu kwa hiari yake na hajapata kushitakiwa kwa skendo wala wizi wowote - iweje leo mumnyime kuitwa mkristo safi? Siri ya maisha yake ya ukristo anaijua mwenyewe moyoni mwake. Ataendelea kucheza hii michezo mpaka ataingia ikulu - unless vyombo husika vifanye kazi yake (vyombo gani??).

Mimi ningewashangaa mno hawa wachungaji kama wangekataa kuhudhuria au kubwata any hear say. Mwenye ushahidi amekaa nao kimya, hataki kumtia mmasai hatani, huyo ndio mkosaji mkuu. Wa kulia naye ni Kikwete kusafisha system - vipi sijui maaana yeye mwenyewe ni mdau katika hilo! Ukikata matawi tu yatachipua tena na mti utaendelea kunawiri, ukitaka kuuua sharti ungoe hadi mizizi.
 
[quote=Tusker Bariiiidi;422808]Nukuu ya Lowassa hiyo hapo chini ndo maana walikuwepo hapo...
Akizunmgumza katika hafla hiyo, Lowassa mwenyewe alisema baada ya kupata matatizo nayo, yeye na familia yake waliamua kumgeukia Mungu na kwamba ndio maana wakaamua kwenda Israel kutembelea maeneo takatifu
.[/quote]


Hilo lingejenga hoja kama angemwalika mchungaji au askofu wa kanisa lake. Lakini kwa kuwaalika viongozi wa madhehebu makubwa ya kikristo hapo inatubidi tumwangalie kama mwanasiasa wala siyo muumini aliyeongoka. Na siye kama wachambuzi wa siasa hatuangalii hilo tukio moja tu bali tunaanza kumwangalia toka 1995 ambapo yeye na rafiki yake JK walionwa na mwalimu kuwa hawafai.
 
Mke wa Lowassa azindua kitabu

.... Lowassa mwenyewe alisema baada ya kupata matatizo nayo, yeye na familia yake waliamua kumgeukia Mungu na kwamba ndio maana wakaamua kwenda Israel kutembelea maeneo takatifu.


Kumbe hakuwa upande wa Mungu.
 
Mke wa Lowasa atunga kitabu akiwa matembezini kutumbua mali zilizopatikana isivyo halali.....du, tena maeneo matakatifu. Kweli tusihukumiane, alichafanya Lowasa ni sawa na dhambi nyingine tunzozifanya wengine humu duniani...hakuna dhambi kubwa na ndogo, je ni wangapi TUNAZINI nje ya ndoa zetu?, wangapi tumevaa maarizi kiunoni?, wangapi tunaiba na kusengenya hata kufikia hatua yakuua kwa maneno na matendo?....

Mama Lowasa hongera kwa kutunga ki-MEMO cha 15pages, ila je na mashehe walikuwepo?
 
Kuokoka kwa Lowassa ni kiinimacho kwani anaendeleza chokochoko cha Urais 2010 kwa hasira ya kutemwa na JK.Huyu Bwana alifanya mambo ya Zombe kwa mlango wa nyuma.Ili toba yake ikubalike arudishe fedha zote alizoiba na atubu kwa kuomba msamaha kwa watu wote aliowakosea.Makanisa yaache kutumika kuhalalisha na kuwasafisha mafisadi.Wanatumika kwa DECI sasa kwa uokovu wa EL.Uokovu unatangazwa hadharani kwa uwazi si kificho au kutangaza kuokoka kwa kuwatumia wengine.
 


Ni siasa za udini za wanamtandao hizo. Maana JK naye siku hizi kwa maulid hajambo kwi kwi kwi kwi. Lakini lazima wanaJF tuzipige vita.
Hizo ni jitihada za kujisafisha na ni hatari kumchezea Mungu kiasi hicho.Kama unatubu rudisha mali ulizoiba kwa umma na uwaombe msamaha wote uliowakosea na hufai kwenye siasa shauri ya tamaa na hasira baki uitunze familia yako.
 

Akizungumza katika uzinduzi huo, Kardinali Pengo, bila kufafanua, aliwataka Watanzania waache tabia ya kusulubiana. "Yesu alikuja duniani, akasulubiwa na hadi leo watu wanaendelea kusulubiana. Tuache mchezo huo," alisema.

Hapa Pengo anamfananisha Lowasa na Bwana Yesu! kuwa walisulubiwa wakiwa hawana makosa! Mbona asifananishe na wale wengine wawili waliosububiwa pamoja na Yesu?


Christopher Mwakasege, ambaye pia alihudhuria hafla hiyo, alisema ni yeye aliyetoa wazo kwa Lowassa na mkewe kutembelea Israel baada ya matatizo yaliyowakuta.

Ili wakajipime kama maipito yao yalifanana na Bwana Yesu! Je, ilikuwa hivyo?


Akizunmgumza katika hafla hiyo, Lowassa mwenyewe alisema baada ya kupata matatizo nayo, yeye na familia yake waliamua kumgeukia Mungu na kwamba ndio maana wakaamua kwenda Israel kutembelea maeneo takatifu.

Aliamua kumgeukia Mungu baada ya kuukubali ushauri Mwakasege. Je, amefanya nini kuwaonyesha Watanzania wanaomtuhumu kuwa sasa umeiacha njia iliyombaya? Maandiko yanatuambia Lazaro alipompokea Yesu, huyo ambae Lowasa alikwenda kuangalia mapito yake, alitangaza kurudisha mali kwa wale aliowadhulumu, Je Lowasa aliwaambia hili hao maaskofu kuwa sasa ameamua kuwarudishia Watanzania mali yao?

Ni kazi ya viongozi wa dini kuwarudisha kundini wale waiopotea, lakini sio kazi yao kuwasafisha. Yampasa mkosaji kutubu na kuiacha njia iliombaya ndipo atangaziwe msamaha, sijaliona hili katika uzinduzi wa hiki kitabu tofauti na viongozi wa dini kujenga mazingira ya kuwa Lowasa ALISULUBIWA!

Nilivyoelewa, kazi nyingine kubwa zaidi sasa imeanza!
 
15-page BOOK! We may need to go back to the definition of a book! What were all these big folks celebrating! A book? Jokes in all walks of life continue...! A dinner would have done better!

Kweli bwan, hiki siyo kitabu ni ka-Brochure!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Jamani nachokiona hapo ni kutaka sifa,haya na huyo Mwakasege anaposema yeye ndo aliwashauri kuwa wakatembelee Israeli alikua na maana gani? Na hao maaskofu wanasema watu siku hizi wanasulubiana pia ana maana gani?Kwamba EL hakutendewa haki au? Nijuavyo aliyoyapata anastahili,na wala hakusulubiwa na mtu ni yeye mwenyewe aliyoyafanya ndo yalomsulubisha alijitundika mwenyewe,kingine nachokiona hapo ni kama vile kupigana vijembe kwa sababu anaposema watu wanasulubishana ina maana kuna watu fulani hapo wanasemwa ki-aina fulani,na huo ni usengenyaji kwa nini usimfate mtu live na kumwambia kuwa wewe acha kusulubisha wenzako kuliko kuanza kurusha maneno kwenye zinduzi kama hizo,Swali,walienda kuzindua kitabu au ndo walipata sehemu ya kutoa madukuduku yao?

Natatizika na kauli zao.
 
Treasure[SIZE="3" said:
Fred[/SIZE];422760]Salaam Wana JF
Ninacho shangaa badala ya kumpa KUDO'S huyu mama kwa kuwa mmoja wa waandishi angalau kazi ambayo wasomi wetu pale HILL wameshindwa na kubaki kufuga kuku na kufungua Glosary mitaani watu wanaanza kubeza kuwa mara kijarida,mara kajitabu.

A book,or kitabu can not be defined kwa kuangalia Number of pages alone,but wana JF mm kilichonifanya nichangie hapa hasa ktk mada hii ni DELEGATION, NA UJUMBE HASA WA MUHASHAMU POLLY.

The mesaje waz veri clia huyu mzee kasema na hapa amenikumbusha kumbe huu mtindo wa kusulubiana orijin yake ni mateso alofanyiwa yesu,na a good mesaje hapa ni kuwa HATA YESU ALIPOSULUBIWA HAKUWA NA DHAMBI but as per christian teaching alisulubiwa kwa dhambi za wengine,na hapa tunapata fundisho na kwa Mwenye MACHO,NA MASIKIO ameelewa LOWASA ALISULUBIWA KWA DHAMBI ZA WENGINE.

Whoever aliekuwa anafatilia mchakato kama si ushabiki basi aliliona hilo na dhambi hii haitaisha italitafuna taifa hili mpaka hapo watu watakapo tubu.

Ebwana Fred, wewe ni Fred Lowassa?..
 
A HOME OF GREAT THINKERS - Let it remain that way.

"WALK THE PATH WITH MY DIARY IN ISRAEL, THE HOLY LAND" . Whether tunataka kuita ni kijarida au kitabu, it doesnt matter, whatever the definition. Polycarp Pengo alikwenda kuzindua a publication with that title.

Habari ya kujisafisha au kusafishwa is actually nonsense here. Pamoja na mapungufu yetu kwenye imani zetu, Polycarp Cardinal Pengo anaweza kuwa Pope wa wakatoliki wote duniani saa yoyote, ndiyo heshima aliyonayo DUNIANI, siyo Tanzania tu, yeye kuamua kutoka ofisini kwake kwenda NYUMBANI kwa Lowassa, ni ujumbe mkubwa sana kwetu, kila mtu autafakari kivyake kwa imani yake. Tusithubutu kutukana na kuvunja heshima ya Cardinal, Mungu atatuadhibu.
 
[/I][/COLOR]

Na inaonekana kabisa aliyewavuta viongozi wa kikristo kwenye mtandao ni EL (hii ni assumption yangu). Wanamtandao wameingia na JK anaonekana kama yuko upande wa waislamu zaidi (hilo pia ni assumption yangu-lakini imejengwa kutokana na matamshi mbalimbali yaliyotoka kupinga baadhi ya maamuzi ya serikali ya JK kama vile OIC na mahakama ya Kadhi). Kwa hiyo hicho kimkutano kwangu mimi nakitafsiri kama ni warning kwa JK kuwa kama wewe unaendelea na hao wa dini zako, basi sisi tuliokusupport 2005 kwa sababu ya EL tutaendelea kumsupport EL. Kwa hiyo badala ya kusema sijui Lowasa anajisafisha au nini mimi kwangu nazitafsiri hizi kama ni siasa za udini ambazo zimeletwa na wanamtandao.

Kwangu mimi wito naoutoa kwa wanaJF ni lazima tukatae hizi siasa ambazo zinataka kuenea hapa nchini.

Tukatae assumptions ama?.
 
A HOME OF GREAT THINKERS - Let it remain that way.

Habari ya kujisafisha au kusafishwa is actually nonsense here. Pamoja na mapungufu yetu kwenye imani zetu, Polycarp Cardinal Pengo anaweza kuwa Pope wa wakatoliki wote duniani saa yoyote, ndiyo heshima aliyonayo DUNIANI, siyo Tanzania tu, yeye kuamua kutoka ofisini kwake kwenda NYUMBANI kwa Lowassa, ni ujumbe mkubwa sana kwetu, kila mtu autafakari kivyake kwa imani yake. Tusithubutu kutukana na kuvunja heshima ya Cardinal, Mungu atatuadhibu.

Ni mtizamo wako. Tukifikia hapo pa kutohoji lolote wafanyalo kwa kuwa tu wao ni viongozi wa dini, basi hata uumbaji aliyoifanya Mungu utakuwa hauna maana. Yafaa nini basi kujitofautisha na ng'ombe au hayawani mwingine?
 
Pengo na maaskofu wengine wanahitaji kujifikiria kabla ya kupokea mialiko ya namna hii, maana huenda wakawa wanajisulubisha wenyewe!! This is absurd!!!
 
Back
Top Bottom