Mke mkorofi

Mke mkorofi

Habari wanajf. Mimi nimeoa na tuna watoto wawili ila mke wangu ni mkorofi sana mpaka nafikia hali ya kuwaza ameingiwa na nini. Yaani yeye anataka awe ndio muamuzi wa kila jambo ndani ya nyumba na ukiweka idea yako anaona eti una mdharau mnataka kwenda out basi time yake ndio ifuatwe na sio yako. Na Ikitokea mabishano ya hoja na kuona anashindwa basi atavunja kila kitu km TV, pasi, deck au hata simu anairusha ukutani na kuvunjika kwa hasira. Baada ya siku anasema tununue vitu vilivyoharibika. Sasa mm naona kama ni ukichaa huu, jamani wenye mawazo au maoni naombeni kwani nafikilia mambo mengi sana ya hii ndoa

Wewe pamoja na mkeo mtakuwa mna ukichaa wa aina tofauti
 
Binafsi napenda mwanamke kama huyo, yaani wanakua na feelings ambazo ni very intense. Pole lakini kwa kukereka/
 
Asante Kwa Uzi mkuu tuko wengi tunafuatilia maushauri..
 
Kuna siku atavunjia pasi usoni kwako. Weka mguu chini, hasa kwenye kuvunja vitu. Ukimfuga na hiyo tabia utajuta maisha yote. Kha! Na umpeleke.muhimbili kwanza akatibiwe wazimu, mkitoka hapo pitiliza church.

Asante kwa ushauri, ila nadhani km kuna wataalamu wa ku manage hasira watasaidia kumweka sawa. Muhimbili wapo?
 
unaishije na mwanamke anatukana matusi? Na watoto wenu bado hawajaanza kutukana? Na ujue wanajifunza na kuvunja vitu. Siku utasema hakuna kwenda school trip mikumi, watasema na tv!

Najitahidi sana wasione yanayotokea ila km huyu mdogo akikasirika na yy anarusha toys zake au kujirusha chini. Sasa nasema sijui karithi tu tabia au ni kitu ambacho amewahi kuona.
 
Mwambie abadili style badala ya kuvunja vitu awe anajivunja mwenyewe
kwa kujipigiza kama watoto wanavyofanya itakua nzuri zaidi
kama ni kichaa aende milembe
 
Binafsi napenda mwanamke kama huyo, yaani wanakua na feelings ambazo ni very intense. Pole lakini kwa kukereka/

Mmmh hujapata kama huyu. Unaweza kusema hivyo lakini ujue lazima itakukwaza
 
Lara1

Thanks a lot kwa ushauri. And nadhani inaweza kuweka adabu
 
mwanamke anakasirika mpk anavunja vitu?kama sio ukichaa basi bangi:majani7:
 
Na kanisani anaenda sana kusali..na tunaenda wote pia..ila anatukana sana matusi utafikili nn sijui.

aisee pole sn! inaonekana mamsapu wako ana tatizo kubwa. fanya jambo moja. mpeleke kwa pastor wa kiroho amfanyie maombi na councelling! in case of more help usiache kutujuza humu JF.
 
Najitahidi sana wasione yanayotokea ila km huyu mdogo akikasirika na yy anarusha toys zake au kujirusha chini. Sasa nasema sijui karithi tu tabia au ni kitu ambacho amewahi kuona.
watoto wanasense kubwa sana. Na tv anaendaga kuvunjia chumbani? Kwanza hamruhusiwi kugombana wala kurushiana maneno mbele hata ya hausigelo, achia mbali watoto! Hamna ushauri hapo, tough love inahusika. Mkalishe chini, fikia makubaliano hakuna moja mbili tatu, na ikitokea nitafanya moja mbili tatu. Na hakikisha akifanya na wewe unatimiza kweli. Dawa ya jeuri ni kiburi banaa, ebo! Kuwa mwanaume basi!
 
Unajua kuishi na mtu lazima kutakua na mikwaruzano ya hapa na pale lkn kusema mm ndio nimesababisha hivyo hapana. Ila kuna wakati naona inakua km vicious
cycle kwani akifanya hivyo na mm naweza ku-react vyovyote vile. Ila nakumbuka ili kupunguza hayo ma-stress naweza kuanza chatting na beer..
Niko na wewe hapo mkwaruzano kwenye ndoa lazima uwepo.

Je unampend amke wako? Kama unampenda we vumilia tu na huku unatafuta wakati mzuri wakuongea naye, pale hana hasira.

Kwa sasa hivi we kubaliana na yeye tu, kwani vyombo nini si mchina yupo :biggrin1:
 
kwenda kanisani si ishu,kwani hujasoma kwenye Biblia kwamba kuna pepo wanafunzi wa Yesu walishindwa kumtoa.....inawezekana kwa level zako huliwezi hilo pepo,tafuta nawe walio juu Kiroho,watakusaidia

Na kanisani anaenda sana kusali..na tunaenda wote pia..ila anatukana sana matusi utafikili nn sijui.
 
akiharibu vitu msinunue tena, atakuwa anajipiga mwenyewe kwenye ukuta
 
pole sana cha msingi ebu jaribu kwanza kumsoma tabia yake na uangalie ni kitu gani ambacho anakua hapendi ili uweze kurekebisha mapungufu yake cha msingi nenda naye taratibu na unapo pata nafasi akiwa hajakasirika unakua vitu vingine unakua unachombezea kama utani
 
hahahahah nimecheeeka! kila mtu na mzigo wake kwa kweli! sasa pasi na Tv vimemkosea nini? mpeke kwa kakobe
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom