Mke mbishi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke mbishi

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Utingo, Sep 9, 2011.

 1. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Wapendwa

  ndoa ya rafiki na jirani yangu iko hati hati ya kuvunjika, kisa jamaa katafuta mke mdogo (ofcourse anasema dini yake inamruhusu). Niliwahi kumwonya mke hakunisikia...kisa jamaa amechoshwa na tabia ya ubishi aliyo nayo mkewe. Nimeishiwa ushauri wa kutoa maana hata mimi tabia ya mke kuwa mbishi kupita kiasi kwa mume siipendi though I feel pity to those little girls (watoto wao). Naomba kujazwa maneno kwa ajili ya kujaribu kumshauri jamaa na mke pia.

  NB: Jamaa hajaoa bado, amepose idea na hiyo ni baada ya kuitisha vikao vingi vya wazazi wao ili kumwonya mke na mke ndiyo ubishi umezidi na ujeuri umeongezeka
   
 2. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Huyo mke mdogo akiwa mbishi zaidi au mdokozi ataongeza mke mwingine(kwa kuwa dini inamruhusu)?mimi nilidhani unaongeza mke kwa upendo siyo kumwadhibu mke aliyetangualia,lol....binadamu bwana, hamna aliyekamilika na ndoa ni kufunzana/kuwasiliana siyo kukomoana. kama ni mbishi kupita kiasi ina maana alimfahamu tangia wako wapenzi, kwanini alimuoa?
   
 3. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 741
  Trophy Points: 280
  Akina mama wakiolewa huwa wana tabia ya kujisahau.
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  ngoja na mie niache ubishi manake dah! basi nampongeza sana rafiki yako kwa kupata small house.mungu aliyemruhusu kuoa mke mwingine amjaalie apate tabia mpya kwa mke mdogo,walau ya umalaya ili asiteseke na ubishi mara mbili kama anavyohofia BJ. ila awanusuru wote na magonjwa ya kileo kwa hisani ya bi mkubwa.
   
 5. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  kwa maelezo yake na kwa kuwa nimeishi nao kwa ukaribu kwa zaidi ya miaka nane sasa, mwanamke hakuwa hivyo huko nyuma.
   
 6. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 741
  Trophy Points: 280
  Nyumba ndogo inapoza machungu
   
 7. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #7
  Sep 9, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Ameoa kwa sababu dini inamruhusu au kwa sababu mke mbishi?

  UMALAYA TU UNAMSUMBUA JAMAA.
  NO JUSTFCATION ON IT...mwenzako akiwa na mapungufu nd anakupa tiket ya kudigi nje?BADALA YA KUREKEBISHANA?
   
 8. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #8
  Sep 9, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  je yeye hajabadilika miaka yote waliyoishi na mke hakuwa na sababu ya kumtafutia nyumba ndogo ........au leo anamtafutia sababu,kwasababu amemchoka au labda anaendelea kutafuta kilichokamilika ambacho hakipo vile vile ilihali yeye akiwa si mtimilifu.


   
 9. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #9
  Sep 9, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  hajaoa bado, amepose idea na hiyo ni baada ya kuitisha vikao vingi vya wazazi wao ili kumwonya mke na mke ndiyo ubishi umezidi na ujeuri umeongezeka
   
 10. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #10
  Sep 9, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kesi za aina hii huwa nakumbana nazo sana, mara nyingi ushauri wangu, kwa kifupi namshauri mume kutafuta sababu ya mkewe kuwa mbishi, kwa jinsi ninavyofahamu, mabadiliko ya kitabia kwa wanandoa hajaji hivihivi, ni lazima kuna mahali inaanzia, na akishajua sababu, itakuwa ni rahisi kwake kupata tiba ya tatizo hilo. kuoa mke wa pili au kuwa na nyumba ndogo hakusaidii kutibu tatizo, na badala yake kulikuza na wakati mwingine kujitafutia balaa, lisilo na mwisho.
  Zipo sababu nyingi kutegemeana na mazingira yaliyowazunguka wanandoa, ambazo zinaweza kuchochea mke au mume kuwa mbishi........ ninachoweza kuwashauri ni kujikagua upya, hasa mume atafute sababu ya mkewe kuwa mbishi akiijua hiyo.... then itamsaidia kupata suluhu.
   
 11. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,275
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kama hakuwa hivyo mwanzo then obvious kuna sababu zimemfanya abadilike,na zinaweza kuwa ni huyo huyo mume. Na hata kama sio hivyo,kwa nini mume akimbilie tu kusema ataoa mke mwingine kabla ya kutafuta mbinu ya kumbadilisha mkewe? Pengine hata ni huo umalaya wake na hao mabibi wadogo ndo umemfanya mama abadilike. Mume ajipeleleze ndani yake kwanza.
   
 12. Mwanyasi

  Mwanyasi JF-Expert Member

  #12
  Sep 11, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 5,767
  Likes Received: 1,898
  Trophy Points: 280
  Vijana wanaita Shock absover
   
 13. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #13
  Sep 11, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Anatatua matatizo ya kujiongezea tatizo.
   
Loading...