Mke kazira kutumia gari: Ushauri please | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke kazira kutumia gari: Ushauri please

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by NyaniMzee, Oct 21, 2011.

 1. NyaniMzee

  NyaniMzee JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 422
  Trophy Points: 80
  Wakuu, naomba ushauri katika mkwamo huu!Nilimpa mke wangu gari atumie kwa ajili ya shughuli zake za biashara ya duka la nguo. Kwa kwenda na kurudi nyumbani na kwa ajili ya kufuatilia mabo ya biashara yake. vile vile kwa shughuli za nyumbani kama kupeleka watoto hospitali n.k. Mimi pia nina usafiri wangu. Mwezi jana aliibiwa side mirror na taa moja ya mbele pale Kariakoo. Akaniarifu na baada ya kuona hana juhudi ya kurudishia huku akiendelea kuendesha gari "chongo" , niliamua kutumia pesa zangu kufanya replacement. Wiki mbili zilizopita nimekuta tena taa moja hakuna. Kumuuliza ikawa zogo. Anasema nisimuulize kitu yeye atarudishia. nikasubiri ikawa kama mwanzo. Baadaye nikaamua tena kununua taa nyingine na nikamwonya kuwa sitaweza kuwa nanunua taa naye anaendelea kutochukua tahadharina kuwa mwangalifu. Heeh! kumbe nimechafua hali ya hewa! Mwanamke wiki mbili hizi hatumii gari anakwenda kazini kwake kwa usafiri nisioujua. Juzi akanitumia sms akasema " sihitaji gari lako masimango yamezidi" Nishaurini wataalam,
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  mwache aendelee kususa. Mke kisirani huyo. Hawezi kupayuka wakati amekosea. Alitakiwa akiri kosa na kuwa mwangalifu. Daladala ilivyo tabu atalitumia tu.

  Pia chunga lugha yako. Kama una masimango acha.
   
 3. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2011
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Acha masimango!!!
   
 4. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,070
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  Utakuwa ulimsimanga sana na kagari kako
  sasa keshapata buzi,
  kazi kwako.
   
 5. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,649
  Likes Received: 4,409
  Trophy Points: 280
  Hicho kisa hakijaanzia kwenye gari, ila ulisha mjengea image kichwani mwake kwamba wewe ni complicator fulani. yaani chako kinauma. kazi rahisi uwe mpole, mjengee jenga imani naye kwanza. Jishushe fanya kila liwezekanalo kuondoa that bad image inside her.
   
 6. Ontuzu

  Ontuzu Member

  #6
  Oct 21, 2011
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 73
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  yeye si mtoto mdogo alijua anachokifanya, ulipomkabidhi hakukuwa na haja ya kumfuatilia mwombe radhi maisha yaendelee
   
 7. M

  Ma Tuma Senior Member

  #7
  Oct 21, 2011
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  gari aina gani? Kama bajaj ana haki ya kususa
   
 8. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #8
  Oct 21, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  1. Inawezekana biashara imekubali sana anakuona wewe huwezi tena kumtishia kitu.

  2. Inawezekana kuna kitu kingine kimejificha tangu siku nyingi alikuwa anakulia timing ili akulipue kwa style hiyo na taa kuibiwa ni mtego tu.

  3. Inawezekana lugha unayotumia kumuuliza au kumweleza kitu haimfurahii kwa hiyo inamkera kiasi cha kutafuta namna ya kukufikishia ujumbe.

  4. Inawezekana biashara ile haiendi hivyo anakuwa stressed sana kiasi cha kuona kuendelea kutumia gari inampa gharama ambazo ni kubwa hawezi kuzimudu.

  5. Inawezekana kuna kitu kingine kikali anakipaki sehemu nyingine tofauti na keshajenga sehemu hivyo hababaishwi tena, na wewe kujifanya kuwa busy na kuacha kutimiza majukumu yako ya ndani kunaendelea kumpa mwanya wa kukuona wewe si lolote wala si chochote.


  NB: Ni mawazo yangu, ukitaka ukweli zaidi jaribu kumchunguza mkeo utajua ukweli.
   
 9. E

  Evergreen Senior Member

  #9
  Oct 21, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unless uwe haujatueleza yote,kama ulimwambia hivyo mara moja tu au ulikuwa unarudiarudia maneno hayohayo,kurudiarudia ndiyo kusimanga vinginevyo huyo ni Mwanamke mwenye Kisarani "bad tempered",yaani katika makuzi yake amefundishwa "kutokukosolewa",Arrogant,"always right"

  Pole sana Mkubwa,ukiwa na rafiki/mke mwenye Haiba hiyo inabidi umkabili kwa Upole sana,ni "handle-with care type"

  Kwanza mwache kwa muda angalau wa Wiki mbili ahenye,halafu siku kaa naye Mweleze kwa Upole "Mke wangu Mpenzi,embu niambie,ukiwa unakosea au una tabia isiyofaa,Mimi mume wako natakiwa nifanye nini?",mwache ajibu hilo swali!!

  Kama ni mwanamke ambaye anakupenda,swali hilo litamchoma na atakuomba radhi!!!! Otherwise,mpotezee mpaka mwenyewe atambue kwamba anakosea!!!
   
 10. MTAMBOKITAMBO

  MTAMBOKITAMBO Senior Member

  #10
  Oct 21, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TATIZO WOTE MNA STRESS!
  Ubaya wa kuwa na stress ni kwamba unaweza kudhani unamjibu ama kumuuliza mtu kitu kwa upole,kumbe kiukweli unamuuliza kwa kumkaripia!JICHUNGUZENI!
   
 11. NyaniMzee

  NyaniMzee JF-Expert Member

  #11
  Oct 21, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 422
  Trophy Points: 80
  ni Toyota Spacio
   
 12. Sokwe Mjanja

  Sokwe Mjanja JF-Expert Member

  #12
  Oct 21, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kina mama ndio walivyo ndugu yangu, kuna kipindi inabidi unajishusha tu hata kama yeye ndio mwenye kosa, kuna siku niliwahi kusema hapa we ukitaka kuishi kwa amani usifuatilie kabisa 'mambo madogo madogo' kama bajeti za nyumbani, matumizi ya magari (hata kama umenunua wewe) au sijui nyumbani panaendaje, wewe cha msingi tafuta hela mkabidhi aamue yeye vyote vya kufanya, apange matumizi na kila kitu kinachohusu hapo nyumbani na wewe ridhika tu au laa umpe ushauri akikataa basi ila wewe fuatilia 'mambo makubwa' tu kama kwanini Gaddafi kafa, CCM mwisho wake lini? Kwanini shilingi yetu inazidi tu kushuka thamani, Obama atashinda next election? Vipi Congo itakuwaje baada ya uchaguzi ujao November? Alafu utaona kama kutakuwa na shida na mpenzi mkeo
   
 13. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #13
  Oct 21, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  ulipomwambia awe mwangalifu ulimaanisha nini? asifanye kazi zake akae kulinda gari lisiibiwe taa/vioo?
   
 14. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #14
  Oct 21, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Jikaze mnunulie Benz.......vibaka wanaziogopa ile mbaya.....au landrover tule tutaa twake nani ataiba?
   
 15. NyaniMzee

  NyaniMzee JF-Expert Member

  #15
  Oct 21, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 422
  Trophy Points: 80
  nilimwambia mara moja na hiyo topic sijairudia tena hadi leo. na kwa alivyo nikiwa mpole sana ananikanyaga.
   
 16. NyaniMzee

  NyaniMzee JF-Expert Member

  #16
  Oct 21, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 422
  Trophy Points: 80
  kuwa mwangalifu kwa ya kuchukua tahadhari unapo park gari, sio kuliangalia Mkuu.
   
 17. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #17
  Oct 21, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Wewe na mkeo hamna good communication. Kuibiwa si tatizo mlipaswa mjue ni kwa nini anaibiwa now and then; mgejua sababu mgetatua tatizo na si kulaumiana; mkeo atakuwa anahisi unamwona mzembe kitu ambacho hamna binadamu anapenda.

  Mgejiuliza tatizo ni nini; je anapark sehemu ambazo ni hatarishi; au labda ungemshauri awe anapark sokoni kariakoo kwa kuwa kuna ulinzi au awe na urafiki na mateja wa kariakoo ni wezi lakini ni walinzi wazuri tu ukiwakatia pesa kidogo.

  Sasa kumlaumu kuwa ni mzembe bila kumpa alternative hata mimi kwa kweli ningesusa. Treat her like a lady utaona kama atakuwa anakununia nunia.
   
 18. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #18
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Samahani brother, kweni kati ya gari na mkeo kipi ni muhimu sana? Naona kama gari ni "material thing" ambayo inachakaa na unaweza kununua na kuibadili upendavyo. Mke ni kitu cha tofauti kabisa, ni mwenzi wa Maisha na faraja ya moyo wako. Ni mama wa watoto wako na pia ndiyo aliyebeba heshima ya familia yako.

  Ningekuwa mimi ni wewe nisingemkasirikia hivyo. Ningemuuliza kwa upole kutafuta namna ya kumsaidia. Na mwishowe ningemnunulia gari yake mwenyewe aligonge atakavyo.

  Brother uko kwenye ndoa, Ndoa ni kitu cha tofauti. Thing wisely!
   
 19. The Magnificent

  The Magnificent JF-Expert Member

  #19
  Oct 21, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 2,669
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  mkuu,niuzie hiyo gari,apande daladala mpaka makalio yayeyuke,ndo atajifunza
  kama upo tayari kwa biashara,ni PM
   
 20. The Magnificent

  The Magnificent JF-Expert Member

  #20
  Oct 21, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 2,669
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  ukisusa tu,mi naliuza kabisa tuone.
   
Loading...