Hii kali sasa! Kutumia jina la mume ni uamuzi wa mtu, ni makubaliano. Mke aweza kulitumia au anaweza kubaki na jina la ukoo wake, wala hakna shida. Sasa mwanaume analalamikia nini? Aridhike na penzi analoewa, na maelewano waliyo nayo kati yao. Ndomambo ya maana. Haya ya majina ni mambo ya kigeni tu. Tangu zamani wamama wa kiafrika hata baada ya kuolewa wameendelea kutumia majina yao ya usichana.Ni jirani zangu na nimeisha wasuluhisha sana lakini kila upande unadai uko sahihi..
Jamaa kaoa mwaka watano huu lakini mkewe ambaye ni mfanyakazi serikalini amekataa kutumia jina la mumewe kama ilivyo zoeleka kwa kina mama wengi wakiolewa. K.m vile Mama maria Nyrere, Magret Sitta,Hilary Clinton, Lwiza Mbutu n.k
Yaani Mrs kang'ang'nia tu kutumia jina la baba yake kitendo ambacho mume kinamuumiza mno! na anaona mkewe anampuuza eti kwa vile hana hadhi kubwa kama baba wa mke.
Jamani hii inakuwaje ni lazima mke abadili jina akiolewa na kujiita jina la mumewe?