Mke anaruhusiwa na Sheria ya Ndoa kukopa kupitia jina la Mume na Mume kuwajibika kulipa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
SHERIA YA NDOA, SURA YA 29 KIFUNGU CHA 64(1), (2) and (3).

Sheria ya ndoa chini ya kifungu tajwa hapo juu inamruhusu mwanamke ambaye ameolewa katika ndoa halali inayotambulika kisheria, KUKOPA fedha kwa jina la mumewe, au kuibadilisha mali ya mumewe inayohamishika kuwa fedha na kuitumia katika mazingira ya ulazima wa kufanya hivyo kutokana na mahitaji ya lazima ya mke au watoto halali wa ndoa.

Katika kukopa fedha au kuuza mali, ulazima wa kufanya hivyo ni lazima uthibitike, na kiwango cha mkopo wa fedha lazima kiendane na kipato cha mume.
 
Kwa Kuweka sawa Hii kauli Huo Mkopo au Kuuza hiyo mali ni kwa ajili ya Mahitaji ya Lazima na Kujikimu tu, Sio Auze Mali au Akope Ili akalipe kikoba au Kwenda kununua Sare za Harusi.

Sheria Imempa Mamlaka Mke Kukopa au Kuuza Mali ya Mume Ili Kujikim kwa Mahitaji ya Lazima tu, Kama kula, Maradhi au Ada kwa ajili ya Watoto.

Na Kuuza huko lazima Kuendane na Hitajio sahihi, sio Auze gari eti Kisa Hakuna hela ya Kula ndani hiyo ni kesi amejitakia na Sheria Itamtupa mkono
 
SHERIA YA NDOA, SURA YA 29 KIFUNGU CHA 64(1), (2) and (3).

Sheria ya ndoa chini ya kifungu tajwa hapo juu inamruhusu mwanamke ambaye ameolewa katika ndoa halali inayotambulika kisheria, KUKOPA fedha kwa jina la mumewe, au kuibadilisha mali ya mumewe inayohamishika kuwa fedha na kuitumia katika mazingira ya ulazima wa kufanya hivyo kutokana na mahitaji ya lazima ya mke au watoto halali wa ndoa.

Katika kukopa fedha au kuuza mali, ulazima wa kufanya hivyo ni lazima uthibitike, na kiwango cha mkopo wa fedha lazima kiendane na kipato cha mume.
Nitaenda kuoa kijijini kwetu kule hawajaeleimika bado sio hivi vichwa vilivyosoma Law school vitakuja nitesa
 
Nitaenda kuoa kijijini kwetu kule hawajaeleimika bado sio hivi vichwa vilivyosoma Law school vitakuja nitesa
Hivi ndio vichwa vya kuoa sasa kwa sababu kwanza vinahamasisha na kuchochea maendeleo ya familia pili ukivipa maelekezo ni rahisi kuyafuata na kutekeleza kwa ufanisi mkubwa maana maelekezo mengine konki kaka sio ya kupewa kila kichwa.
 
Na amini hii ni elimu wanawake wanapeana Sasa......hapa wanaume vichwa panzi lazima waliwe tu maana hakuna namna.

Yaani mwanamke katika mambo yote yanayo mzunguka mengi yake yakiwa bado Hana majibu nayo, ameacha hata kusoma jinsi gani ya malezi ya watoto, au ni jinsi gani ya kuanzisha biashara ukiwa na mtaji mdogo ......yaaani vyote hivo hajaviona kaenda kusoma jinsi gani ya kukopa pesa kwa kutumia jina mme

Nyie maromantiki na majentromeni jiandaeni kisaikolojia Kuna kitu kizito kitawashukia vichwani
 
Hivi ndio vichwa vya kuoa sasa kwa sababu kwanza vinahamasisha na kuchochea maendeleo ya familia pili ukivipa maelekezo ni rahisi kuyafuata na kutekeleza kwa ufanisi mkubwa maana maelekezo mengine konki kaka sio ya kupewa kila kichwa.
Womenizer natika ubora wako all the best
 
Back
Top Bottom