Mfumo dume, wimbi la shinikizo la mume kuzikwa nyumbani

Dear

Member
Nov 18, 2009
46
3
Watetezi wa haki ya binadamu mko wapi? Watetezi wa wanawake mko wapi? Vyombo husika viko wapi?

Nawasalimu nyote,

Hivi karibuni kumeibuka kama mara mbili hivi kwenye vyombo vya habari vya mitandao, mwanamke akifiwa na mumewe na kama wamechuma mali pamoja au la, au hata kama kuna nyumba imeachwa na mke amekaa naye hadi umauti ufike, unakuta ndugu, majirani au wanawake majirani wanashinikiza marehemu azikwe ndani ili kumkomoa mwanamke asije kuingiza mwanaume mwingine au akiolewa tena asikae kwenye ile nyumba tena au hata hapo mbeleni kama kuiuza.

Mfano, kuna msiba umetokea huko Bagamoyo wa ndugu Masawe, Masawe amefariki na kwa kuangalia ile picha ya marehemu ndugu Masawe alikuwa bado kijana kabisa, ina maana mke wake naye nikijana zaidi ama kulingana naye ( video uko youtube kwa Millard Ayo).

Kwa ufupi ndugu na majirani wanasema ndugu Masawe azikwe kwenye nyumba aliyoicha, na ukitazama nyumba kweli ni nzuri tu.

Na madai ndugu wanasema Masawe alisema kama akifariki basi azikwe kwenye nyumba yake, lakini mke alienda mahakamani kuomba ndugu Masawe asafirishwe kwenda kuzikwa Moshi.

Swali ni kuwa je, marehemu ndugu Masawe ni kweli alisema azikwe kwenye nyumba yake, na ilhali wanasema aliugua kwa muda mfupi, Nimewaza je, ugonjwa wa muda mfupi unaweza kumuwezisha mtu kufa na kuacha wosia wa namna iyo?

Unajua UMASKINI, CHUKI na WIVU vinapelekea haya mambo yote, kwa mtazamo wangu. Je, mke ndiyo angefariki na itokee mke ndiyo alikuwa mwenye uwezo kifedha na ndiyo amejenga nyumba yeye na wala siyo mumewe, je, ndugu wangemlazimisha mke azikiwe ndani ilhali wanajua mume bado kijana na baada ya msiba anaweza kuoa tena?

Wanawake, wanawake, wanawake wa Tanzania nimewaita mara tatu, maana kwenye msiba huu wa ndugu Masawe hadi mliongoza maandamano ya ndugu Masawe azikwe nyumbani kwake hapo Bagamoyo badala ya kusafirishwa au makaburini, ili tu kumkomoa mwanamke mwenzenu.

Na nakawmbia wanawake wataosoma ujumbe huu wengine wengi mtaponda.Why mnamhukumu mwanamke mwenzenu? Why mnaona kama atafaidi kama marehemu mume wake asipozikiwa pale? nanukukuu kuna mwanamke mwingine nilimskia akisema kuwa ataingiza mwanaume mwingine, na wengine ohh nyumba kamuachia mtoto wake mdogo ivyo akikua amuone baba yake.

Hivi wanawake wa Tanzania (baadhi) mmekuwaje, why chuki, WHY? Why WIVU, Why. Haya sasa kwa ivyo yeye kuolewa na mume wake kufariki mapema ivyo hata kama yuko kwenye 20s au early 30s asiolewe tena, ivyo ajifungamanishe na ndoa ya kwanza ya mume aliyefakiri? Biblia inasema mjane asiandwe ispokuwa umri wake amepata miaka 60 1 Timotheo 5:9 a.

Kwenu ndugu,

Masawe ni mchanga, ni mara chache mno hata asimilia 20 kati ya 100 wachaga kuzikiwa mbali na Moshi wengi ya wachaga wanasafiri, so nyumba imewatoa macho hadi kutaka kumzikia kijana wa watu kwenye makazi? ok lengo kumuwekea mtoto mali baba yake alizochuma je mnajuaje kama mama naye kashiriki kwenye fedha au kusimamia tu ujenzi naye si ana haki. na Je kwa mawazo yenu nini kinawauma wakati uyo mtoto ni wa uyo uyo mwanamke.

Vyombo husika, dada alienda kuomba msaada kwenye vyombo vya sheria, je hata viongozi wa mtaa wameshindwa kusaidia, je vipi viongozi wa dini nao pia wameshindwa kusaidia, wote mmekaa mnamhukumu binti wa watu.

Swali la kujiuliza, tugeuze shilingi haya mke sasa ndio angekuwa ametangulia je mngeibuka kumshadadia mume amzike mke ndani? au ndio kwanza mngemwambia safirisha au kazike makaburini wewe ni kijana pumzika hata mwaka then oa tena, na tena cha kushangaza hata hapo mkewe amefariki ana replacement kichwani kabisa.

mwaka jana iitokea kama hili hili tena , wakamzikia mwanaume ndani kwa lengo la asiolewe tena au kuhisi ataleta mwanaume mwingine mle ndani.

Ok sawa basi , Je kama mama hana kipato na nyumba aitumie kupangisha ili apate ada za watoto na matumizi , je ni nani atakubali kupangishwa kwenye nyumba yenye kaburi? tena kwa wivu wenu ndugu na wanawake wenzie mnasema kabisa azikwe mbele ya nyumba (nyie watu nyie why haya mambo).

Mwaka jana tena kuna dada kafiwa na mumewe kwa ajali, na amekaa na mumewe kama miaka 5 au zaidi, na wamejaliwa nyumba na usafiri, yaani the moment ndugu wameskia kifo, wakaenda kumchunga mke asifiche hati za nyumba na magari kisa hakuzaa na kijana wao. hahahaa yaani inachekesha sasa wote wanafanya kazi, mnajuaje kuwa labda mali wamechuma wote na jinsi wanawake walivyo wachakalikaji sasa hivi.

Ombi langu
Wote kwa pamoja tushirikiane, serikali na wanaharakati wanawake, kusaidia hawa wajane, na wanawake PLEASE PLEASE muache kumalizana wenyewe, mwanamke mwenzio akilia mlie naye sio ndio kumfungia kibwebwe na kumzomea au kumkandamiza.

Shule kijana kachapwa uongozi umefika, kwenye fujo kama hizi pia fikine na msaidie wamama wanaozomewa kwenye jamii kisa wivu na tamaa za mali.

Yaani mnaona kama mwanamke mwenzenu na iyo nyumba atawatambishia mtaani, acheni wanawake haya, mambo teteaneni ndio hata serikali itawasikia na jamii itawasikia.
 
Mwanamke anaempenda mumewe KWA dhati hawezi kubali mumewe azikwe Mbali!!!

Atakae awe anamwagilia maua ya kaburi lanmwamba wake siku zote maishani hata kama akiolewa!!

Lakini jamii ya chuma ulete ya wanawake inawaza Maisha Baada ya kufiwa na mume na ndio chanzo Cha kudai ndoa KWA nguvu KWA wanawake wengi wa SIKU hizi Ili tufe mtumbue mali bass!

Binafsi mwenzi wangu akifa anazikwa hapa hapa ninapoishi Ili wajukuu na watoto waone alipo bibi Yao halafu na mimi nishazeeka nikaotwa nawaambia niwe pembeni yake!

Kuna vitu vingine wanawake mnatia aibu!

Mnawaza maslahi kuliko utu!

Mwanamke anaetaka mwili wa mumewe usafirishwe wakati eneo la kuzika lipo huyo ni chuma ulete!!

Nyie ndio mnatia wanawake aibu Hadi wanamme tuogope ndoa!!
 
Mama Massawe umelalamika sana lakini kwanini hutaki mumeo azikwe nyumbani kwake kama alivyotaka?

Una agenda gani na hiyo nyumba yake? Au ulitaka uiuze baada ya kumzika huko Kilimanjaro?

Anyway, mambo ya watu ni magumu sana. Ila kwa mihangaiko yote ya mke mpaka mahakamani inaonyesha ana evil intentions.
 
Back
Top Bottom