Mke kagoma kujiita jina la Mumewe, mume afanyeje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke kagoma kujiita jina la Mumewe, mume afanyeje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzizi wa Mbuyu, Mar 22, 2010.

 1. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,070
  Trophy Points: 280
  Ni jirani zangu na nimeisha wasuluhisha sana lakini kila upande unadai uko sahihi..
  Jamaa kaoa mwaka watano huu lakini mkewe ambaye ni mfanyakazi serikalini amekataa kutumia jina la mumewe kama ilivyo zoeleka kwa kina mama wengi wakiolewa. K.m vile Mama maria Nyrere, Magret Sitta,Hilary Clinton, Lwiza Mbutu n.k
  Yaani Mrs kang'ang'nia tu kutumia jina la baba yake kitendo ambacho mume kinamuumiza mno! na anaona mkewe anampuuza eti kwa vile hana hadhi kubwa kama baba wa mke.
  Jamani hii inakuwaje ni lazima mke abadili jina akiolewa na kujiita jina la mumewe?
   
 2. Sydney

  Sydney Senior Member

  #2
  Mar 22, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  aaaaaaaaaaah, sio lazima jamani, kwani kubadili jina na kufuata la mumeo ndio kunaongeza nini ama kupunguza nini? Cha muhimu mnapendana, mnaaminiana, na pia kuheshimiana, basi! Jina halisaidii kitu, libadilishwe ama libaki la baba, hakuna kitakachopungua, wala si lazima!
   
 3. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Mie naona halina umuhimu wowote hata ningekuwa mie siwezi kutumia jina la ukoo wa mume,
  Watoto wetu ndo watatumia jina sio mie;)
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  sio lazima
  hilo ni suala la insecurities tu.
   
 5. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,070
  Trophy Points: 280
  Wanao badili majina wanamatatizo gani kama siyo muhimu, au nini kinacho wafanya wabadili?
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  huyo dada yupo sahihi mimi naona coz hapo alipo kapitia shule kibao na pengine vyuo mbalimbali, vyeti vyote vina majina ya baba yake mzazi na wakati anaajiriwa si alipeleka vyeti vya shule vyenye jina la baba mzazi sasa jamaa ana hofu gani na jina? haamini km atakuwa wake km jina lake halitatumika? aache ugomvi bana tena siku hizi wanawake wengi hawapendi sana kuitwa mrs fulani, wanapenda tumia majina yao ya kwanza utasikia miss esther, je ingekuwa namna hiyo jamaa si angerusha ngumi
   
 7. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #7
  Mar 22, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ni makubaliano (maridhiano) tu baina ya wawili hayaongozwi na sheria wala amri amasivyo kingeongezewa kwenye kiapo cha ndoa 'Bibi flani bin Flani, uk tayari kubadili jina la baba yako, uliache/kulikana na kutumia la mumeo?' watu wanacomplicate maisha utadhani hawana shughuli za kufanya ah!!

  Mnapendana, mnaheshimiana na kuaminiana inatosha!! But if he think it is that necessary basi atake trouble ya kubadilisha (maana ile process ya kubadili hadi vyeti inakera).
   
 8. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #8
  Mar 22, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  jamani jaribuni kumuelewa huyo kaka........ huu ni utamaduni, yeye kinachomuumiza ni kuwa wanaume wenzake wake zao wanatumia majna yao ila yeye wake kagoma..... sasa ni saikolojia tu inamtesa, anakosa usalama na amani ya akili/saiklojia.......... unajiuliza kama angekuwa ndiye mfano kikwete mkewe angeng'angania kutumia jina la baba ake? angalia winne mandela, licha ya kutalikiana na mumewe zaidi ya mongo mmoja uliopita bado anajiambulisha kama winnie mandela!!!!!!!!

  inaonekana siku hizi watu wamepuuza uatamaduni na wanaangalia jina gani lnalolipa!!!!!!!!!! sasa hapo mtu anajisikia inferiority fulani anaona kama mkewe yuko kibiashara zaidi naye anataka kuhakikishiwa kuwa anapendwa unconditionally................ kweli dunia ya siku izi vi vurugu tupu............ mke anaona ugumu gani kufanya kitu ambacho hakina madhara yoyote kwake wala kwa familia yake na ambacho kitamrejesa mumewe kwenye ego ake anayopaswa kuwa nayo??.............

  mi nashauri kuwa kama kusingekuwa na tatizo hakuna ulazima, maadam mhusika (mume) anaona liko tatizo basi mama abadili, maisha yaendelee........... nitasikitika sana kusikia wamefika kwnye hatua ya ugomvi ama hata talaka kwa sababu hiyo pekee............ na hapo mke atakuwa na lawama kubwa zaidi................
   
 9. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mbona ni kitu kidogo sana if it is for the good and peace of the family???.............
   
 10. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #10
  Mar 22, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mwambie jamaa agombenia urais na mungu akimsaidia apate utaona ,wife wake atataka kubadili jina
   
 11. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #11
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Huyo dada hampendi mumewe, ndio wale wale wanaoolewa ili kuondoa nuksi. Kama kweli yuko proud of her marriage why is she not ready to be proud of being called ''Mrs Masaki''?
   
 12. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #12
  Mar 22, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,070
  Trophy Points: 280
  Hahaaahaaa kama ulikuwepo!
  Amini usiamini jamaa anasema sasa anarudi shule na anatafuta pesa kwa nguvu kwani anaamini akipata uwezo mkewe atalionea fahari jina lake tu.
   
 13. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #13
  Mar 22, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Ndoa za siku hizi ni balaa sababu za kutokutumia jina la mumeo ni kuwa siku mkiachana yuko kivyake na cut yake in half na pia mke amejishkiza tu kwako au anaona jina la babake linalipa kuliko surname yako ndio ndoa zetu siku hizi maana kuna rafiki yangu mkewe aligoma kutumia jina la mume wake ampaka kidogo waachane. Mume akaamua kuwa mpole lakini leo hii kila wanachofanya mpaka risiti za kununulia vitu kama saruji, mbao n.k mke anaandikisha majina yao wote wawili...Ndoa za leo ni kindoano ndoano tu na kimaslahi zaidi
   
 14. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #14
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Kupendana huko na kuheshiana huko kuheshimiana gani? Kwa upande mmoja tu? Ndoa inahusisha mambo mengi sana likiwemo la kupoteza uhuru katika baadhi ya mambo (si yote) na pia hata ku-sacrifice baadhi ya vitu kwa ajili ya ndoa yako likiwemo jina la baba yako!

  Sasa yeye kinachomshinda kuridhia maombi ya mumewe kubadili jina ni kitu gani? Wanawake wengine wa ajabu sana, eti kisa jina la baba yake linaheshimika mjini basi hataki kubadili na kuweka la mumewe, basi angeolewa na huyo baba yake! [​IMG] She is just stupid!
   
 15. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #15
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Huyo mwanamke ndio wale wenye akaunti mbili za siri ambazo mume hajui! Yaani mnaishi kimachel machale tu ndani ya nyumba!
   
 16. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #16
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Nini urais, hata udiwani tu unatosha sana kumfanya abadili hiyo surname yake! Halafu wanawake wa aina hiyo ni rahisi sana kumegwa na watu wenye majina mjini!
   
 17. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #17
  Mar 22, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Huyo jamaa kinachomsumbua ni Inferiority; maana alishasema kuwa baba wa mkewe ana hadhi kubwa kuliko yeye. sidhani kama baba mkwe wake angekuwa hana hadhi then mkewe akatae kubadili jina angeleta huu ugomvi.
  kubadili jina sio big issue, hata kama natumia jina la babangu bado mimi ni mkewe. cha maana ni kumjali mumeo tu na kutoleta kiburi sababu ya hadhi ya baba.
   
 18. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #18
  Mar 22, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kitamaduni ni muhimu kubadili jina, huyo Mama ana agenda ya siri ndio maana hataki kubadilisha jina... Wengine wanataka waitwe majina ya wazazi wao wajulikane HAWAJAOLEWA kusudi waendelee na HAMSINI zao.
   
 19. RR

  RR JF-Expert Member

  #19
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,720
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Huyu mke anajua akitumia jina la baba labda linamsaidia katika mihangaiko yake, si ana jina kubwa? Jina la baba yake linalipa kuliko la jamaa yako.
  Anatakia aelewe kwamba mkewe yupo kikazi zaidi!
  Kwa mfano uoe mke mwenye surname ya Nyerere halafu abadilishe na kutumia Mkude? Sidhani. Jamaa aelewe tu au apandishe jina lake chati
   
 20. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #20
  Mar 22, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Yeah sure ndoa za siku hizi inabidi uwe mguu ndani mguu nje haziaminiki chochote chaweza tokea wakati wowote na trend yake yaweza kuwa hivi;

  Mwanzoni NDOA= wawili kufunga ndoa
  Halafu inakuwa DOA = wawili kufarakani baada ya (ndoa-n) kuingia doa
  Mwishowe inakuwa OA= kutengana na mmoja kuoa baada ya (doa -d) = oa
   
Loading...