Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,744
Issue ya kubadili jina au kutobadili jina imekaa kidini zaidi. Kwa wanao fuata imani ya Kiislamu Uislam umekataza kubadilisha jina la baba na kutumia jina lolote jengine kama kutumia jina la mume.
Waiteni kwa baba zao, maana huo ndio uadilifu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu
Al-Ahzaab: 5
Na tabia ya mke kubadilisha jina kutumia jina la mume, mfano kuitwa Mrs Juma, ni tabia zisizolingana na maadili na mafundisho ya Kiislam kabisa!
Kufanya hivyo vile vile kuna madhara yake. Kwanza tabu ya kubadiisha pasipoti na vyeti vinginevyo kwa ajili ya utambulisho katika idara za serikali.
Pili, inapotokea kifo cha mume au talaka, inabidi mke arudie kubadilisha pasipoti na vyeti vyake vyote vingine kuweka jina la baba badala ya jina mume, hivyo ni usumbufu unaompotezea mtu fedha na wakati wake.
Kwa hiyo Muislamu ni bora kubakia katika amri na mafunzo ya dini yake ili kupata ridha ya Mola wake na pia kujiepusha na usumbufu mbali mbali.
Ila kwa wale wanao fuata kanuni za kimila na kikristo na kimagharibi ni jambo lililo zoeleka kwa mke kujiita kwa jina la ukoo wa mume wake.
...akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.
Matt 19:5-6
X- Paster, (hapo kwenye Red) kumbuka kanuni za kidini za kiislamu zinaruhusu kutaliki na kuolewa as much as you can. sasa kama wangesema kila mwanamke akiolewa abadilishe jina la ukoo naona ingekuwa balaa, maana kila ukiachwa unabidi jambo la kwanza uwaze kubadili jina. Imagine mwanamke anaolewa x5 katika maisha yake, kila akiolewa anababili jina, akiachwa anabadili, si inakuwa usumbufu?