Mkataba wa TRL (TRC)

MUHINDI ALIYEKUWA AKISIMAMIA HUO MRADI WA KUKARABATI MABEHEWA NA KUISHAURI MANAGEMENT KUPITIA HUO MKOPO WA BANK YA DUNIA KATI YA MWAKA 2002 HADI 2006 KUTOKA KAMPUNI YA RITES ..ANAITWA ENGNEER MUKESH..NA NDIE ALIYEHUSIKA KUANDAA SOME TECHNICALITIES...NA BAADAYE KWA KUSHIRIKIANA NA SUBASH PATEL NA CHANDE ..WAKAISHAURI RITES INUNUE TRC....

KWA SASA ENGENEER MUKESH AMERUDI TENA BAADA YA ZOEZI KUKAMILIKA AKIWA SASA NDIYE MKURUGENZI WA UFUNDI WA TRL...[CHIEF MECHANICAL ENGNEER...]WA TRL...

KWA KIASI KIKUBWA HUJUMA ZA KULIFANYA HILI SHIRIKA LA UMA KIYUMBE NA HATIMAYE KUWA MZIGO KWA SERIKALI HADI KUAMUA LIUZWE ZILIFANYWA NA HAWA WAHINDI WAKISHIRIKIANA NA SUBASH NA ANDY KAMA MWENYEKITI WA BODI NA HAWA KINA MBOMA KWA KUJUA AU KUTOJUA ..HASA PALE WALIPOKATIZA SAFARI ZA RELI ZIISHIE DODOMA ...MZIGO UKAWA MKUBWA KWA SHIRIKA KULIPIA WASAFIRI..NA MIZIGO MABASI HADI DODOMA...WASWAHILI WENZETU WAO WALIFAIDIKA KWA KUPEWA COMMISSION NA MAKAMPUNI YA USAFIRI AMBAYO YALIPATA KAZI KUPELEKA WASAFIRI NA MIZIGO DODOMA....NA HAPO SHIRIKA LIKAZIDI KUYUMBA KWA NAKISI YAO KUWA KUBWA...KUTOKANA NA KULIPA GHARAMA KUBWA HIZO NA ZILE ZA MAFUTA AMBAZO WALIKUWA WAKINUNUA KWA PESA TASLIM[BANKERS CHEQUE]..KUTOKA GAPCO AMBAYO NI KAMPINI YA MWENYEKITI WAO WA BODI ANDY CHANDE.....IKAWA HOOI KIPESA ...IKABIDI SERIKALI YA AWAMU YA NNE ILIPOINGIA IKAKUBALI MKATABA UANZE KAZI..UKISAINIWA NA CHENGE AMBAYE NDIYE PIA ALIYEDRAFT MKATABA UPANDE WA SERIKALI WAKATI AKIWA MWANASHERIA MKUU AWAMU YA TATU...

MKITAKA KUJUA RITES WALIFANYA HUJUMA MAKUSUDI WAKISHIRIKIANA NA MA ENGENEER WAZALENDO KUSHAURI NJIA YA RELI YA DODOMA TO DAR ILIKUWA MBOVU..SHANGAA KUWA NI HAO HAO TENA WIKI MBILI TU BAADA YA KUINGIA TENA BILA UKARABATI WA AINA YEYOTE ..WALIANZISHA SAFARI ZA RELI KUANZIA DAR [MABEHEWA NA ABIRIA].......

TENA MASIKINI RAIS WETU JK NA MAWAZIRI WAANDAMIZI BILA KUJUA AU WAKIJUA WAKAKARIRIWA WAKISIFIA WAHINDI WA RITES ETI ">>>wamefanikiwa kuanzisha safari za treni kutoka dar es salaam kwa abiria na mizigo ndani ya wiki mbili tu......bila hata kujiuliza ...."

Unatamani kulia!....hii mikataba ya kihuni na kisanii isiyo na maslahi kwa nchi yetu tutaendelea nayo mpaka lini? Kutenda kosa siyo kosa lakini kurudia kosa ni kosa kubwa sana!
 
phillemon michael:

In fact 'ume-connect vidoti vyote perfectly...' Very good work.

Kutokana na mabango yaliyokuwa yanaonyeshwa na wafanyakazi waliokuwa wamegoma juzi, ni wazi kwamba ujumbe unajulikana vizuri kabisa.
 
BREAKING NEWS.....

GET YOURSELF A COPY OF CONSESSION AGREEMENT BWT GOVERNMENT AND TRL ON TUESDAY-

PATA NAKALA YAKO (BINAFSI)YA MKATABA ULIOSAINIWA KATI YA SERIKALI NA TRL... JUMANNE

hapa umekusudia mkataba umetiwa saini au tutapata nakala jumanne?


mie sijakupata unakatika katika(mawasiliano)
 
India kwenyewe reli yao imewashinda,nenda huko huone abiria wao wanapanda mpaka kwenye mapaa?

Hili wazo la kuwapa wahindi lilitoka wapi?


....sio wazo ni dili hilo, yaani hapo kuna watu wanakula cha juu ukiona hivyo!!
 

wahariri PICHA NZURI SANA HIZI..caption inayofaa...'" MOJA YA MAGARI MOSHI YA KAMPUNI MAMA YA RITES [INDIA]...AMABAYO NDIO MWEKEZAJI ALIYEPEWA NA SERIKALI KUENDESHA SHIRIKA LETU LA RELI....BAADA YA KUONEKANA ANAYO TEKNELOJIA NA MTAJI UNAOTOSHA KUENDESHA SHIRIKA HILO..."

india1.jpg


india2.jpg


Only in India


Jamani jamani msalie mtume hivi huyu Pinda si ndio alikuwa kwenye mpini huyu wakati tunapiga kelele mkataba huu usitiwe saini?

Nafikriri sasa ni wakati muafaka wale wote walioshiriki kwenye huu mchakato waende kuozea Segerea, huu ujinga utaendelea hadi lini? Pesa ya walipa kodi inapotea na wao kazi ni kukenua tu na kupiga misafara ambayo haina faida kwa walipa Kodi. When will this stop?

Kazi ya Bunge sasa itakuwa ni kuchunguza uozo na Uvundo ulio kwenye Serikali hii.
 

HATUTAENDELEA KWA SABABU HATUJUI KINACHOENDELEA

Hiki kihabari hapo juu ni mfano wa tatizo kubwa la nchi yetu: vyombo vya habari mdosho!

Siwezi kusema lolote kuhusu huu mkataba na kudokeza ni vipi mambo yangetakiwa yaende kwa sababu sielewi mambo yanavyotakiwa yaende sasa hivi, na yalikwendaje.

Pinda alikuwa anatembelea ofisi za TRL wakamuonyesha mafaili au kila mkataba unapita kwa Pinda? Na nini kinafuata, Pinda kaagiza nini, kuna watu watatemwa, au mkataba ufutwe? Pinda, au Kamati za Bunge zina nguvu gani hapa? (Leo tumelipa dola laki moja na elfu hamsini kwa mkataba wa Richmond ambao haukufutika!)

Wafanyakazi wa TRL nao wameulalamikia huu mkataba. Lakini, wafanyakazi wa ngazi za juu wemesema nini kuhusu huu mkataba? Nataka kujua TRL imejibu nini baada ya Pinda kuukosoa huu mkataba. Kampuni nyingine zilizoleta tenda zilikuwa bora kuliko TRL?

Waziri Mkuu katoa mfano kwamba TRL waliwaeleza wana injini 90 halafu baadae wakawaeleza wana injini 50. Lakini hivyo walivyo ambiana kwa nini hawakuviandika? Mkataba unawataka wawe na injini ngapi? Mfano wa Pinda nao una mushkeli.

Hii habari hapa kwanza hatujui inatoka wapi, bahati mbaya Mpita Njia hakuonyesha ni chanzo gani. Nikiisoma naona ni kama ya Tanzania Daima na majarida ya IPP, ambayo yanaandika habari nusu nusu na kishabiki shabiki, wakati watu tunataka pande zote. Huwezi kuchukia ufisadi kishabiki shabiki tu.

Vyombo vya habari ndio kiungo dhaifu kuliko vyote katika mnyororo wa kuvuta gurudumu la maendeleo. Na hatuwezi kufanya mabadiliko kama hatujui kinachoendelea. Tudai ukweli.

Mwana JF mmoja ana saini inasema:"Huwezi kuwa na ufahamu kama hujaasi, na huwezi kuasi kama huna ufahamu."

Unataka tuandike kama waandishi wa habari hapa? Sisi wengine hatukusomea kazi hiyo, kama utatoa kozi fupi nitashukuru
 
Napenda kuwapongeza PM na wengineo, na Nyongeza zaidi si wadanganyika tunatakiwa kuelewa mkakati wa India katika ku-export watu wao katika nchi zinazodanganyika kama Tanzania, ili baadae washikilie nguvu zote za kiuchumi, yaani tunakuwa kama koloni lao, sasa hao viongozi wetu na ulafi wa mdogo mdogo hawajui matatizo wanayo leta kwa watoto wao baadae. Tutakuwa kama Mauritius baadae tusipoangalia au tukiendelea na hawa akina Chenge wanao angalia Hela ya leo bila kuangalia in future itakuwa na thamani gani kwao.
Wakituonea huruma tutakuwa kama SA, kiongozi mweusi lakini uchumi umeshikwa na UNTOUCHABLES
 
Tumesahau kuwa tuliongeza mishahara bila kuwashirikisha waajiri? Sisi wenyewe ndio tumempa loophole Rites! Na bado.
 
Tumesahau kuwa tuliongeza mishahara bila kuwashirikisha waajiri? Sisi wenyewe ndio tumempa loophole Rites! Na bado.

..HAPANA HUO MSHAHARA WALIAHIDI RITES WENYEWE BILA KUSHINIKIZWA NA SERIKALIO........SASA KUMBE NAO WALIKUWA WANAFANYA USANIII.NADHANI WAMEGUNDUA USANII SI KOSA TANZANIA...INGEKUWA NCHI NYINGINE HIYO TU [KUTOA AHADI YA UWONGO]..INGETOSHA KUWAFUKUZISHA..NA KUNYANGANYWA LESENI....
 
Unataka tuandike kama waandishi wa habari hapa? Sisi wengine hatukusomea kazi hiyo, kama utatoa kozi fupi nitashukuru

Nilitegemea utuambie chanzo cha hiyo habari. Ni hilo tu. Siwezi kujadili jambo kutokana na kitaarifa ambacho hakina kichwa wala miguu.

Sikutaka wewe uandike kama mwandishi. Nililaumu gazeti, na nikasema taarifa mbovu ni moja ya sababu za kuzorota kimaendeleo kwa nchi kama Tanzania. Sio wewe, ndugu. Sisi ambao tunawahukumu watendaji wakuu lazima tuwe juu ya lawama kwa kuwa na misingi ya habari za kweli, za pande zote kabla ya kusulubisha wengine.

Ndio hapo tutakapo inua kiwango cha madajiliano hapa JF. Wengi hamtanielewa!
 
Nilitegemea utuambie chanzo cha hiyo habari. Ni hilo tu. Siwezi kujadili jambo kutokana na kitaarifa ambacho hakina kichwa wala miguu.

Sikutaka wewe uandike kama mwandishi. Nililaumu gazeti, na nikasema taarifa mbovu ni moja ya sababu za kuzorota kimaendeleo kwa nchi kama Tanzania. Sio wewe, ndugu. Sisi ambao tunawahukumu watendaji wakuu lazima tuwe juu ya lawama kwa kuwa na misingi ya habari za kweli, za pande zote kabla ya kusulubisha wengine.

Ndio hapo tutakapo inua kiwango cha madajiliano hapa JF. Wengi hamtanielewa!

Wewe ndio unashusha kiwango cha JF na habari zako nyingi zisizothibitishwa na wewe mwenyewe au vyanzo unavyojaribu kuquote. So far leave MpitaNjia alone.
 
..HAPANA HUO MSHAHARA WALIAHIDI RITES WENYEWE BILA KUSHINIKIZWA NA SERIKALIO........SASA KUMBE NAO WALIKUWA WANAFANYA USANIII.NADHANI WAMEGUNDUA USANII SI KOSA TANZANIA...INGEKUWA NCHI NYINGINE HIYO TU [KUTOA AHADI YA UWONGO]..INGETOSHA KUWAFUKUZISHA..NA KUNYANGANYWA LESENI....

Mimi nilidhani mshahara huu ulitokana na viwango vilivyotolewa na serikali mwaka jana? Viwango vilivyopanga vima vya chini vya mishahara kuanzia wafanyakazi wa ndani na wengineo? Kwani hivi viwango vinavyogombewa sasa vilikuwa kwenye contract? kama hali ni hiyo kwa nini serikali iingilie? Sio kwamba inaona ilimuongezea mzigo mwekezaji(?) kwa kuweka viwango vilivyokuwa nje ya makubaliano? Viwango hivi ni lazima vilikuwa na impact katika matarajio yake ya faida na hakuna mfanyabiashara ambaye angekubali kubeba bila kuwa na uwezekano wa kuushusha kwa mtumiaji wa mwisho!
 
Jamani TRC ilishakuwa mzigo kwa serikali na kwa muda mrefu walikuwa wanatafuta muwekezaji lakini hawapati kila mmoja akiangalia majukumu alikuwa anakimbia sasa katika kukata tamaa kabisa wakaona ngoja tu wamsukumie huo mzigo RITES angalau aende nao hivyohivyo maana hali ilishakuwa mbaya.sasa yanayowatokea sasa hivi ni matunda ya serikali kulikatia tamaa shirika hilo ambalo yenyewe imeshindwa kulisimamia likafa.
 
Mwafrika,
Ni wewe Mwafrika uliyesema CCM iondolewe kwenye Katiba?
 
Mwafrika,
Ni wewe Mwafrika uliyesema CCM iondolewe kwenye Katiba?

Yes,

Ni mimi niliyesema kuwa kama ccm na sera za Nyerere zimethibitishwa kuwa ndizo zimeleta umasikini na zinaendelea kuleta umasikini basi inabidi ccm na sera zake vitolewe kwenye katiba na kufutwa kabisaaaaaaa
 
Augustoons,
Mshikaji siamini kuwa TRC ilikuwa mzigo mkubwa kwa serikali isipokuwa serikali (viongozi) ilitaka TRC ife kifo kama cha makampuni mengine yote makubwa kisha yapate kuuzwa kwa bei njugu wakikamata hizo 10%...All these things Tanesco, NBC, IPTL, City water na mashirika yote muhimu ni faida tupu kwa mabillioni ya fedha. Matajiri wote wakubwa duniani wameshika mashirika kama haya kama sio serikali zao..Na ndio ugonvi mkubwa wa IMF na nchi maskini kwani mataifa makubwa target yao ni hizi miundombinu ya uchumi wa nchi...Hivyo siwezi kuamini kwamba TRC ilikosa mwekeshaji kama walivyosema wakati tumeanza kuisikia Richmond.
Hizi habari za kufa ni hadithi tupu tusubiri hiyo Jumanne kisha utaona mwenyewe kuwa Wajerumani walikuwa tayari kuingia mkataba tena basi navyokumbuka mimi ilikuwa contracting ambayo serikali yetu ingeendelea kushika 100% share na wao kulipwa fedha za Kufufua na Uendeshaji wa reli hiyo tena navyosikia waliona heshima kubwa ( honoured) kuitumikia serikali yetu ktk vitu ambavyo wao walivijenga kwetu..
 
Kwa maana nyingine hao wahindi walitoa info za uwongo ili kuweza kuupata mkataba huo wa kuendesha shirika la Reli. Hivyo siri kali ina kila sababu ya kuuvunja kwa kuwa hao wahindi hawakuwa wakweli na hivyo kuepuka hayo malipo ya shilingi 18,000,000 kwa mwezi za hizo injini saba, malipo ambayo yanafanywa hata kama injini hazifanyi kazi. Pia inabidi siri kali iyasimamishe malipo hayo mara moja.

Watanzania wenzangu, nafikiri kuna kitu tusichokijua kuhusu nchi yetu, labda ni tajiri sana kiasi cha kuwa na uwezo wa kulipia migharama mikubwa namna hiyo huku viongozi wetu wameziba masikio na kufumba macho-inachefua hapa naona ni MUNGU tu ndiye atatuokoa, wenzetu Kenya hawawezi vumilia kuona ujinga unaofanywa na hawa wageni-ipo siku wataondoka bila kuaga
 
Wewe ndio unashusha kiwango cha JF na habari zako nyingi zisizothibitishwa na wewe mwenyewe au vyanzo unavyojaribu kuquote. So far leave MpitaNjia alone.


Katika hili mbona namuona yuko sahihi Kuhani Mkuu .Yeye amehoji kuhusu hivyo vyanzo vya habari Havikuweka habari uchi .Kwa kuwa inagharimu maswali mengi kama aliyouliza yeye ili kuchangia maada kikamilifu.Haku mlaumu Mwana JF aliyeleta hiyo habari nadhani mumemusoma vibaya.
Nimesikia kuna muungwana atatoa full data pamoja na huo mkataba ,so let we be good and be cool.
 
Back
Top Bottom