Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,997
- 1,161
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ameushtukia mkataba baina ya Serikali ya Kampuni ya Rites ya India kuhusu ukodishwaji wa lililokuwa Shirika la Reli nchini (TRC).
Akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Reli (TRL), iliyoundwa baaya ya kukodishwa kwa TRC, Pinda alisema mkataba huo una mushkeli, kwani kuna mambo ambayo hayaelewi jinsi yanavyoendeshwa.
Akitoa mfano, alisema kuwa wakati TRC ikikaribia kumaliza shughuli zake, ilieleza kuwa ina injini zaidi ya 90, lakini mara baada ya TRL kuanza kazi, ilieleza kuwa kuna injini takriban 50 tu.
Pia, wafanyakazi wa TRL wamesema kuwa mwekezaji huyo hakujali kukarabati vifaa hivyo vilivyopo, badala yake alikwenda kukodi injini nyingine kwenye kampuni yake ya Rites na tayari zimeshaingia injini saba ambazo zinalipiwa capacity charge ya sh 600,000 kila siku hata kama hazifanyi kazi.
Jambo hilo limemfanya Pinda auone mkataka huo kama ile ya umeme ambayop inalikamua Tanesco. Wafanyakazi wa TRL wameshamuomba Pinda kuwa mkataba huo nao upelekwe Bungeni ukachunguzwe.