Mkataba wa Bandari ya Dar ni kitanzi. Mbaya zaidi shughuli za awali zinaanza kabla ya Bunge kukubali. Je, wananchi tutakuwa na sauti katika hili?

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
670
Screenshot 2023-06-07 at 08.41.14.png


Mkataba kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii kwa ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi wa Bandari za Bahari na Maziwa Makuu ya Tanzania unaibua masuala kadhaa ambayo yanahitaji ufafanuzi kutoka kwa Serikali.

Kwanza DP World mbali na kujipakulia minyama kuwa ni kampuni inayoendesha bandari nyingi duniani katika mabara sita, kampuni hiyo ya Dubai ina kashfa ya ukwepaji kodi. Mbali na suala hilo bado mkataba, katika ibara ya sita umetaka msamaha wa kodi ili kuvutiwa kuwekeza nchini, hali ambayo italeta kilio kwa kupunguza mapato nchini kwa kuzingatia kuwa, suala la kodi sio jambo msingi kwenye kuvutia uwekezaji kama walivyobainisha wataalamu wa uwekezaji.

Ibara ya 25 (1) ya mkataba inaeleza kuwa shughuli za awali za mradi zitaanza mara tu baada ya kusainiwa mkataba. Hata hivyo, shughuli hizo zinatarajiwa kufanyika kabla ya Bunge kuridhia mkataba huo na kabla ya mkataba kuanza kutumika rasmi kwa mabadilishano ya hati za uridhiaji kati ya serikali zote mbili. Shughuli za awali za mradi ni pamoja na upembuzi yakinifu, tathmini ya kimazingira na kijamii, ujenzi wa barabara za muda, na kadhalika, kama ilivyoelezwa katika Ibara ya 1 ya mkataba.

Ni muhimu serikali itoe ufafanuzi juu ya eneo hili, kwani shughuli za mradi zinaanza kabla ya mkataba kuridhiwa na Bunge. Hii ni kwa sababu ya umuhimu wa uwazi na uwajibikaji katika mchakato wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Ibara ya 20 inayohusu usuluhishi wa migogoro inaonyesha kuwa usuluhishi utafanyika Afrika Kusini na kutumia Sheria za Usuluhishi za Kamisheni ya Umoja wa Mataifa juu ya Sheria zinazohusika na Biashara za Kimataifa (UNICITRAL Arbitration Rules). Hii inapingana na maelekezo ya kifungu cha 11 cha Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali na Maliasili ya Mwaka 2017 (The Natural Wealth and Resources [Permanent Sovereignty] Act, 2017). Sheria hii inaelekeza kuwa migogoro inayotokana na matumizi ya rasilimali na maliasili za nchi haitatatuliwa katika mahakama au mabaraza ya nchi za nje, bali itatatuliwa na vyombo vya sheria vya Tanzania na kwa kutumia sheria za Tanzania.

Katika Ibara ya 23 (4), mkataba unaeleza wazi kuwa serikali husika(Tanzania) katika mkataba hawana haki ya kuvunja, kujitoa, kuahirisha au kusitisha mkataba katika mazingira yoyote, ikiwa ni pamoja na uvunjaji mkubwa wa masharti ya mkataba, mabadiliko ya msingi katika mazingira ya utekelezaji mkataba, mgogoro mkubwa wa kidiplomasia, au sababu zozote zinazotambulika katika sheria za kimataifa.

Mkataba haujaweka wazi muda wa utekelezaji, lakini Ibara ya 23 (1) inasema kuwa mkataba utaendelea hadi shughuli za mradi zitakapokamilika. Ibara ya 27 inaweka masharti kwamba, mara mkataba utakapoanza kutumika rasmi, serikali yoyote katika mkataba huo haitaingia au kuwa sehemu ya makubaliano ya ndani au ya kimataifa yanayohusiana na utekelezaji wa mkataba.

Ibara ya 30 inaweka masharti ya uthabiti, uimara, na uhakika wa kutokuyumbisha mkataba. Kutokana na ukosefu wa muda wa ukomo katika mkataba, kuna uwezekano wa kuhitajika kufanya marekebisho ya sheria kulingana na wakati, ambapo mabadiliko hayo yanaweza kuathiri masharti ya mkataba na kuonekana kama ni kuyumbisha mkataba.

Kwa upande wa Tanzania, mamlaka ya kusaini mkataba huu yametolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa upande wa Serikali ya Dubai, haijawekwa wazi mamlaka ya kusaini mkataba huu.

Kwa kweli, mikataba ya ki-chief mangungo, kama tunavyoiita, ni sawa na kutoa taifa letu kama kipande cha ndafu. Hakuna mkataba usio na ukomo na vile vile kifungu hiki ni hatari katika kipindi hiki.

Hili ni jaribio hatari kwa usalama wa kijamii, kiuchumi, na kimazingira wa nchi yetu! Ninahuzunika sana kwa Watanzania wanaotegemea shughuli za uvuvi! Hii ni hatari kubwa kwa maisha ya watu na kwa uchumi wa nchi yetu.

Hatuwezi kukubali kwamba tunaweza kuendelea kuwa tegemezi kwa mataifa mengine na kusababisha uharibifu mkubwa kwa rasilimali zetu za asili.

Ni kusikitisha sana kuona kwamba mikataba kama hii inasainiwa bila kufanya mashauriano ya kina na wadau wote muhimu. Inaonekana kama tuna haraka sana na hatuzingatii maoni ya watu. Tunapaswa kuwapa watu wakati wa kutosha kutoa maoni yao na kushiriki katika mchakato wa kufanya maamuzi. Rushwa haina nafasi katika suala hili.

Kwa kuongezea, ikiwa Rais ameshasaini mkataba, je, maoni ya watu yatafanya tofauti yoyote? Je, kweli maoni yetu yanathaminiwa au ni uzembe tu? Inaonekana kama sisi raia hatuna sauti na maamuzi yanafanywa bila kuzingatia maslahi yetu.

Ni wakati wa kuangalia vizuri mikataba tunayosaini na kuhakikisha kuwa inalinda maslahi ya taifa letu na vizazi vijavyo. Tunahitaji kufanya maamuzi ya busara na kuchukua hatua thabiti kulinda rasilimali zetu na uhuru wetu.

Tunawaomba viongozi wetu wachukue hatua sahihi na kuhakikisha kuwa mikataba inayosainiwa inalinda maslahi ya taifa letu. Tunahitaji mikataba yenye uwazi, uwajibikaji, na inayozingatia maslahi yetu ya kitaifa. Ni wakati wa kuwa na uelewa mkubwa na kuchukua hatua thabiti ili kulinda taifa letu na watu wake.

Tukumbuke daima kuwa sisi ndio wenye dhamana ya kulinda na kukuza nchi yetu. Hatuwezi kuiuza kwa bei ya chini na kuhatarisha mustakabali wetu. Tunapaswa kuwa makini na kuhakikisha kuwa tunafanya maamuzi sahihi kwa faida ya taifa letu.
 

Attachments

  • Dar_Port_Contract_Mkataba.pdf
    2.3 MB · Views: 28
Tunawaomba viongozi wetu wachukue hatua sahihi na kuhakikisha kuwa mikataba inayosainiwa inalinda maslahi ya taifa letu. Tunahitaji mikataba yenye uwazi, uwajibikaji, na inayozingatia maslahi yetu ya kitaifa. Ni wakati wa kuwa na uelewa mkubwa na kuchukua hatua thabiti ili kulinda taifa letu na watu wake.

Tukumbuke daima kuwa sisi ndio wenye dhamana ya kulinda na kukuza nchi yetu. Hatuwezi kuiuza kwa bei ya chini na kuhatarisha mustakabali wetu. Tunapaswa kuwa makini na kuhakikisha kuwa tunafanya maamuzi sahihi kwa faida ya taifa letu.
Yakiitishwa Maandamano utatoka Barabarani? Au unabwekwa tu kwenye social media?
 
Hawa jamaa wanaturejesha utumwani. Napata wasi wasi kuwa Magu alikolimbwa na hawa hawa aliowaamini akidhani kuwa wanawake na watu wa hovyo wasingemfanya kitu.

Angalia kilichotokea Peru ambako makamu wa rais Dina Boloarte alipomdondosha bosi wake Pedro Castillo na kumweka ndani huko Peru.

Haya mambo yapo.
 
Kuna harufu isiyo njema ktk hili..

✅Kwa nini haraka ni kubwa ktk kutekeleza haya makubaliano?

✅Kwa kiwango gani sheria za manunuzi zimefuatwa ktk huu mchakato?

✅Vigezo vipi vimetumika kufanya maamuzi ya kumchukua DPW? Na kwa nini?
-International Bidding
-Single Source
-Restricted Tendering

✅Kwa nini masharti ya mkataba yamekuwa ya kibabe (Dictative)?

✅Ni kweli mkataba hauna kikomo? Kwa nini? Kwa faida ya nani? Kuna tija gani ktk hili?

✅Projections za mapato zipoje tukimpa DPW? Kuna guarantee gani ya yeye kuperform? Je asipo perform?

✅Nini mapana ya uendeshaji wa DPW,gati kadhaa? Bandari nzima?

✅Muktadha wa masharti ya mkataba wa DPW yana tofauti gani na masharti ya wawekezaji wa uliokuwa mradi wa bagamoyo?
 
wacha nibaki huku kijijini..

Naacha kufikiri na kuuliza maswali

Naamini viongozi wetu wana washauri wazuri

Sirudii tena mimi
 
Jioneeni wenyewe jinsi Tz ilivyokuwa na itakavyokuwa shamba la bibi..
Taifa la mazombie.. makubaliano yanatiwa saini na waziri badala ya mwanasheria mkuu wa serikali
 

Attachments

  • AZIMIO LA BANDATI_.pdf
    2.3 MB · Views: 10
Tanzania unfortunately doesn’t have leadership that is the reason for giving a lease of 100 years to the Arabs to manage the port!
These ccm politicians are only concerned about the here and now ; meaning the next general election and not the interests of the next generation!😂😂😂
 
Hivi tutaendelea kulia mpaka lini? hawa jamaa hawabadiliki, walishatuonesha na wanaendelea kutuonesha kwa vitendo hawataki kabisa kubadilika, sasa hawa tutaendelea kuwalalamikia kwa ujinga wao wanaotufanyia makusudi mpaka lini?

Hapo kwenye huo mkataba wa miaka 100 waliotoa kwa hiyo kampuni, maana yake wameirithisha bandari yetu kwa vizazi, kwamba hiki kizazi chetu kipite, mpaka kizazi kitakachofuata kitaukuta huo mkataba wa kinyonyaji bado upo!.

Hivi kwanini Samia asipandishwe mahakamani kwa hili kosa kubwa namna hii? kiongozi asiyetaka kuihangaisha akili yake hata kidogo, kwa chochote, yeye anawaachia wasaidizi wake kila kitu!, ok, she is immune, basi laana yetu iwe juu yake, simply, makosa ya kiongozi tuliyenaye, tunaenda kuyarithisha maumivu yake kwa vizazi, huu sio ujinga tu, hakika ni upumbavu kabisa.
 
wako sawa tu, mitanzania mitumbavu kutwa kushangilia mpira tu huku wanasiasa wanafanya mambo ya kingese bila woga, juzi ajira za walimu zimetoka huku madogo waliosoma masomo ya geography, kiswahili na histori wakikataliwa kuomba bila sababu yoyote hakuna aliyehoji na sasa bandari inapigwa mnada mamtu yapo na yanga na simba. kwao bora nchi ipoteane ila simba na yanga wazione, ***** hii nchi tunaishi tu lakini hakuna maisha.
 
juzi ajira za walimu zimetoka huku madogo waliosoma masomo ya geography, kiswahili na histori wakikataliwa kuomba bila sababu yoyote
Hao madogo ni vilaza utaendaje kusoma masomo ya kidwanzi hivyo, kwanza ualimu ni kazi ya laana na kitumwa hawakuona fani za heshima kama sheria na nyinginezo mpaka waende kwenye ualimu fan la kilofer mpaka ngedere wanawacheka
 
Back
Top Bottom